KULIKONI ZANZIBAR FILM FESTIVAL (ZIFF) WADAU KIZIKOSOA TUNZO ZENU?!
habari, mpya 4:57 PM
Monalisa msanii wa kimataifa katika filamu.
MWANADADA Nyota katika tasnia ya filamu Bongo Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ ameshindwa kuamini kwa kile alichokiona katika utoaji wa tuzo za ZIFF kwani tuzo zilizotolewa na hazikuwa na hadhi ya tuzo kutokana na maandalizi yake, tukio hilo lilitokea jumapili iliyopita katika ukumbi wa kimataifa wa Maisha Club Masaki, anasema pamoja na wasanii kuwahi kufika sehemu ya tukio lakini hakukuwa na maandalizi kwa ajili ya tukio hilo usiku wa manane walipofanya tukio hilo.
“Ni kweli wasanii tunahitaji tuzo au motisha kutoka kwa wadau wowote ambao wanaguswa na kazi zetu, lakini jambo hili nalo linahitaji maandalizi na tukio hilo kupewa hadhi ili kujenga maana halisi ya tuzo hizo, hii kwangu naona kama tamasha tu ambalo halina utofauti na matashama mengine ambayo yanafanyika kila siku”, anasema Monalisa.
.
Inasemekana kuwa utoaji wa tuzo hizo ambazo zilikuwa zinajulikana kama Min Ziff Red Carpet uliingia dosari pale muda uliopangwa yaani saa mbili usiku kufika na tukio hilo kushindwa kufanyika kwa muda huo ahadi midaa ya saa nane usiku, hali ambayo baada ya wasanii kuwa wapweke na kupelekwa Casino kwa ajili ya kushangaa wanaocheza huko.
Aidha Monalisa ameomba wanaohusika na utoaji wa vibali kuwa na umakini kuliko kutoa vibali kwa watu wasio na sifa za uandaaji na kuwaacha watu wenye uwezo wa kuandaa tuzo za kueleweka, kwani mara nyingi wamekuwa wakitokea watu wanaotaka kuandaa tuzo bora lakini taasisi husika zimekuwa zikitoa masharti magumu kwa kisingizio cha kuwa tayari kuna mwandaaji mwenye haki ya kuandaa tuzo bila mafanikio.
Katika tuzo hizo wasanii waliobahatika kutuzwa alikuwa ni Jacob Steven ‘Jb’ ambaye filamu yake ya Senior Bachelor ilikuwa bora, Muongozaji Bora Issa Mussa ‘Cloud’, Steps Entertainment kama kampuni ya bora ya usambazaji, Steven Kanumba filamu yake ya Devil kingdom ikishinda kwa ubora wa sauti na Vincent Kigosi ‘ Ray’ pamoja na wasanii wengine.
CHANZO;FILAMU CENTRAL
Asante!