ARUSHA FILM FESTIVAL 2013 SCHEDULED FOR 25 NOV-1 DEC
Posted by bongofilmdatabase habari, mitandao, mitandaoni, slide, udaku, workshop 8:29 AM
MAANDALIZI ya tamasha kubwa la filamu lijulikanalo kwa jina la Arusha African Film Festival yanaendelea vizuri na kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa, tamasha hilo ambalo linategemegea kuonyesha zaidi ya filamu 70 kutoka nchi 20, litambatana na utoaji wa semina ya utengenezaji wa filamu kwa watengeneza filamu ambao watajisajili kwa ajili ya Semina hiyo ambayo ni muhimu sana kwa watayarishaji na tasnia ya filamu kwa ujumla.
Akiongea na FilamuCentral mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Mary Birdi amesema kuwa ni tamasha ambalo linaleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya filamu Swahiliwood, kwani watengeneza filamu kutoka sehemu mbalimbali watafika na kubadilisha mawazo na watengezaji wa filamu wa Tanzania, ni muhimu kila mdau akajipanga na kushiriki tamasha hili linalojenga.
“Ni tamasha ambalo linajenga tasnia ya filamu nchini hasa pale watu wetu wanavyopata workshop kwa ajili ya kazi wanazofanya, siku hizi teknorojia inakwenda kwa kasi ni vema kupata shortcourse mara kwa mara, lakini ni nafasi pia ya kutangaza Utalii wetu,”anasema Mary.
Tamasha la AAFF litazinduliwa tarehe 29.November.2013 Mount Meru Hotel Jijini Arusha wakati Semina itaanza rasmi tarehe 25. Novemba
November. 2013 sambamba na maonyesho ya filamu katika sehemu zifutazo Alliance Francaise, Via Via, Mount Meru Hotel, Mango Tree, na New Arusha Hotel tamasha hili kiingilio ni bure kabisa, Siku 7 USIKOSE KUSHUHUDIA FILAMU KALI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI.
Vyanzo:Swahiliworld planet na filamucentral
asante!
AY NA FA WAKAMILISHA VIDEO YA CHEZA BILA KUKUNJA GOTI
Posted by bongofilmdatabase slide, udaku 9:35 AMSIFA ZA KIJINGA ZINAVYOWAGHARIMU WASANII
Posted by George Iron kinyemi, mitandao, mitandaoni, mpya, slide, udaku 9:25 AMSIFA ZA WASANII ZINAVYOFICHA DONDA LA UMASIKINI LINALOHITAJI TIBA.
Unahitaji kumjua msanii wa filmu Tanzania? Unahitaji kujulikana kuwa na wewe ni msanii Tanzania?? Unataka upate sifa mtaani na jina lako likaririwe katika midomo ya watu!!
Kama jibu ni ndio basi na njia ni nyepesi.
Hakikisha unaandikwa magazetini!!! Hiyo ndiyo siri ambayo ipo wazi.
Utaandikwa kwa mabaya ndiyo usifiwe? HAPANA. Lazima yaandikwe mazuri.
Jawabu hili la kuandikwa mambo mazuri huwalazimisha wasiokuwa na mazuri ya kuandikwa wajibumbie visa vyao vya uongo ilimradi jamii iwatazame mara mbilimbili.
Sio jambo jipya kukutana na maandishi yakimnukuu msanii wa filamu akisema “ Sanaa imeniwezesha kujenga nyumba kijijini kwetu na hapa mjini nina kiwanja”
“Filamu zinaniingizia milioni mia tatu kwa mwaka!!”
“Kwa kawaida kila Scene nacheza kwa laki mbili.”
Haya ni baadhi tu ya maneno kutoka kwa wasanii wenyewe. Maneno ambayo yana ukweli kwa asilimia kumi tu!!! Wasanii ni waongo na wanauunda uongo kujipatia sifa zisizokuwa na tija.
Sifa hizi zinaifanya jamii kuwachukulia wasanii wote kuwa ni watu wa daraja fulani lisilofikika kirahisi, na wasiohitaji msaada tena.
Wasanii wa filamu Tanzania, wamekuwa wakitukuza sana sifa kuliko maendeleo. Hili ni jambo ambalo linatutofautisha sisi na wenzetu wa Afrika magharibi! Wao wanatanguliza mbele maslahi binafsi katika fani hiyo, kisha sifa hujileta zenyewe bila kutafutwa. Hii hali ni tofauti na Tanzania ambapo msanii kwa pesa yake ananunua sifa za kijinga.
Kuna wakati elimu dunia ndogo waliyonayo wasanii inachangia haya kutokea. Elimu ambayo ingewawezesha kuithamini kesho yao kuliko LEO wanayoipigania kila siku.
Mwisho wa mapigano haya ya kuihangaikia LEO badala ya kuitazama KESHO. Wasanii wengi wakishaupoteza ule umaarufu wa kununua enzi ambazo nyota zao zinang’ara sasa yule ndugu yetu aitwaye umasikini anawaumbua. Licha ya kujificha sana hawawezi kujificha milele. Shida zikiwaumbua ndipo hukiri kuwa sanaa hailipi. Huyo anayekiri hivyo anasahau miaka kadhaa nyuma alijitapa kuwa hakuna muigizaji ana gari la thamani kama la kwake, ama hakuna msanii wa filamu anayemiliki nguo za bei ghali kama yeye. Sasa analia tena!!! Donda linakuwa komavu na sasa halina tabibu!! Lazima liendelee kuchimbika mwishowe anakufa maskini na tunabaki na neno moja tu. Alikuwa muigizaji mzuri sana!!
Neno hilo lina maana gani kwa marehemu???
LAITI KAMA: Wasanii wangetambua kuwa maisha ya msanii ni kujifunza kila siku ili uwe bora. Basi wangejifunza kwa wenzao ambao walizichezea nafasi mwishowe donda likawaumbua lilipokomaa.
LAKINI wasanii wa jana na wale wa leo, afadhali wa JANA walikuwa na kisingizio kuwa sanaa ilikuwa burudani pekee. Wa sasa atasingizia nini iwapo sanaa ya sasa ni KAZI??
ZIJUE SERIES ZILIZOTAMBA NA ZINAZOBAMBA KWA SASA UKIANZIA NA YA ARROW ( Eps 1 )
Posted by bongofilmdatabase habari, series, udaku 4:10 AMKatika nyumba tano hapa mjini kwa sasa iishiyo vijana wapendao filamu zitokazo hollywood basi nyumba mbili kama sio tatu katika ya hizo tano wanafuatilia series au ziite filamu zenye mwendelezo wa mikasa na matukio yaani tamthilia kwa lugha ya kawaida, kuna series nyingi sana zimewahi tayarishwa huko marekani mpaka sasa ila miongoni mwa series zilizopata wafuatiliaji wengi sana hapa mjini na Tanzania yote kwa ujumla wake wakiwemo na hao vijana niliyowazungumzia hapo awali ni series kama Prison Break, 24hours, Lost , Vampare Diary na nyingine nyingi tu.
Leo katika Big Screen yetu tutaizungumzia series inayokwenda kwa jina la ARROW kama top cover yake unavyo iona hapo juu. filamu hii ni moja ya filamu ninaimani ukithubutu kuianza kuitizama tu sehemu yake ya kwanza kiukweli huwezi kuacha kutafuta sehemu ya pili na nyingine zote zifuatiazo na kukaa chini kuzitizama na hata mwisho wake kuwa shabiki moja mkubwa miongoni mwa wafuatiliaji ambao hupanga foleni katika internet cafe kuzidownload kila mwisho wa wiki kwa mwajibu wa taratibu wa watayarishaji kuzitoa kila jumatano baada ya kuzionesha kwenye television zao za kibiashara huko marekani na kuziachia kwenye kurasa za mitandaoni kila alhamisi kuwapa fursa wadau wengine kuzidowload kila ijumaa.
ARROW ni filamu ambayo inamzungumzia kijana mmoja aitwae Oliver kutoka katika moja ya familia tajiri kwenye mji wa Starling aliyokuwa akiishi humo nchini marekani ambaye alinusulika kupoteza maisha kwenye ajali ya boti waliyokuwa wakisafilia aliyokuwemo na watu wengine watatu ambao ni baba yake mzazi,msaidizi wa baba yake na mwongozaji boti ile na rafiki wa kike kipenzi.
Oliver hakupata mawasiliano na familia yake aliyoicha huku mjini kwa taklibani miaka mitano kitendo kilicho wafanya ndugu, jamaa na marafiki wote kuamini wote waliyokuwemo kwenye ile boti katika safari ile walikufa maji. ila Oliver alinusulikia na kuvuka mpaka kisiwa kimoja kilichopo huko Pacific, baada miaka mitano kupita iliyokuwa imetawaliwa na mateso makali na shuluba ya kuwindana na watu waliyokuwa hawana utu kabisa akijitahidi kupigania maisha yake Oliver ana bahatika kupata upenyo na kutoloka kisiwani humo na kurejea mjini.
kijana Oliver anarudi mjini na mbinu nyingi sana alizojifunza huko kisiwani atakazozitumia kurekebisha na kusahihisha makosa yaliyofanywa na familia yake uhususani baba yake na watu wengine waliyokuwa wamefanya na kufanya vitu visivyokuwa sawa na kuukosea mji wa Starling, ila swali la kujiuliza ni kwamba atasahihishaje makosa yote hayo?! ndipo Oliver anaamua kutengeneza na kujenga uhusika mpya feki wa bwana mmoja alijulikana kama VIGILANTE kwa maana ya mtu ambaye anajichukulia maamuzi mkononi yaani anavunja sheria pale anahitaji fanya vitu vyake, Vigilante huyo alikuwa anatumia silaha ya aina ya mishale.
Leo Big Screen yetu tumeanza na utambulisho na maelezo mafupi juu ya sreies hii ya Arrow ambayo mpaka sasa ipo ungwe ya kwanza tu onesho la kumi na tisa, Big Screen(Bs) ifuatayo tutaangazia wahusika mmoja baada ya mwingine kisha kuendeleza simulizi hili tamu la Series ya ARROW
OLIVER- STEPHEN AMELL
Staa na muhusika mkuu wa series ya Arrow wambaye tutamwelezea zaidi kwenye simulizi lifuatalo ambapo tutaangazia maisha yake ya nje ya sanaa na ni kazi ngapi amewahi na kutarajia kuzifanya mpaka sasa. Tafadhali wafahamishe washikaji tusiwaache nyuma kwenye simulizi hili la kusisimua na kama utapenda kujiunga na jopo la kusimulia maonesho mengine ya ndani ya series hii na kuambatanishwa kwenye Big Screen yetu usisite kutucheck kupitia 0719 71 93 16 sasa.
STEVEN KANUMBA MEMORIAL DAY NI LEO
Posted by bongofilmdatabase mpya, udaku 2:18 PMFAMILIA YA MAREHEMU STEVEN CHARLES KANUMBA KWA KUSHIRIKIANA NA BONGO FILM DATA BASE ILIYOPO CHINI YA KAMPUNI YA POINT INC IMEKAMILISHA ZOEZI LA UTENGENEZAJI TUNZO ZA APPRECIATION KWA WADAU KADHA WA KADHA LEO HII ZITAKAZOTOLEWA KESHO 7/4/2012 AMBAYO NI SIKU AMBAYO ALIFARIKI DUNIA KANUMBA NA NI MWAKA MMOJA SASA UMETIMIA TANGU AIAGE DUNIA.
APPRECIATION
AWARD
In Memory of a great Tanzanian Film Actor of his age
''STEVEN KANUMBA''
HAYO NDIYO MANENO YALIYOPO KWENYE HIZO TUNZO WADAU WENZANGU FILAMU HAPA NCHINI.
KANUMBA MEMORIAL DAY NI KESHO..
R.I.P BROTHER
BISHOP: KWANINI NIGERIA IWE KIPIMO CHA FILAMU ZETU?
Posted by bongofilmdatabase udaku 8:58 PM
Sekta ya filamu Tanzania kwa sasa inajulikana duniani licha ya matatizo
yake, licha ya mtayarishaji wa filamu wa Tanzania kuendelea kuishi
maisha yasiyo tofauti na mtu mwingine wa kawaida! Hali halisi ya soko la
filamu nchini inabana sana uwezekano wa kuibuka kwa wasanii,
watayarishaji au waongozaji wapya...
Sidhani kama kuna mtu
atabisha kuwa filamu za kibongo ‘hazitesi’ katika ukanda wa Afrika
Mashariki na maeneo ya Maziwa Makuu. Filamu hizi zimesaidia kwa kiwango
fulani kuitangaza nchi hii, kuwatangaza wasanii wa nchi hii, lakini vipi
kuhusu maisha ya wasanii hawa? Je, wanapata stahili yao na wanaishi kwa
kutegemea filamu pekee?
Kinachosikitisha zaidi: utoaji wa hizi
filamu zetu imekuwa kama mchezo wa soka bila refa, sawa na mkutano bila
mwenyekiti, darasa bila mwalimu, au nyumba (familia) bila mzazi…
Wafanyabiashara wanaahidi milioni kumi na tano hadi ishirini na ushee
kwa sinema; watoaji sinema wanalipua kazi; waigizaji hawalipwi vizuri;
utengenezaji sinema unafanywa haraka haraka. Sinema zinatengenezwa kwa
wiki moja na zinatolewa ndani ya mwezi mmoja tu. Haraka haraka…
Wasanii wa filamu wanaigiza bila script wala mazoezi, watengenezaji
filamu wengi wanatumia mwanya huo kula uroda na wasichana wazuri wazuri
(ndiyo maana siku hizi kuwa miss ni kigezo kikubwa cha kupata nafasi ya
kucheza filamu, haijalishi kama una kipaji cha kuigiza au la), sinema
zinazotolewa nchini eti zinalinganishwa na za Wanaijeria! Tangu lini
sinema za Wanaijeria zikawa kipimo cha filamu?
Kwa nini tufuate
nyayo za Nollywood katika kuzalisha sinema zetu? Kwa kipi hasa? Hii
inatufanya kusimulia hadithi zao; angalia sinema zetu zinavyosimulia
uchawi, zinavyosimulia mapenzi au mikasa ya kijamii utagundua hilo.
Tunaiga hadithi zao, namna yao ya uchezaji, sinema zao ambazo nyingi
zimekuwa zikiigwa kutoka mataifa ya Magharibi na India.
Hivi
Watanzania tumelogwa? Hii ni kwa Watanzania wote. Kwanini hatupendi/
hatununui sinema zinazotolewa na Watanzania wenzetu? Kisa? Hazituvutii.
Moja ya sababu ni kwamba zinatengenezwa vibaya kwa kulipuliwa. Lakini
kwa nini hata sinema zinazotengenezwa vizuri bado hatuzinunui? Kwa nini
hatuzifurahii? Kwa nini hatuzitolei maoni na kuzitangaza? Tunachoweza ni
kuziponda tu! Hivi hatudhani kuwa hiyo ndiyo njia kuu itakayotufanya
tuendelee kama wenzetu, tunaowaona Miungu kutuzidi?
Kwa upande
wa waandaaji wa filamu tukumbushane kwamba sinema ni sanaa inayochukua
muda. Hatuwezi kutengeneza sinema ikakamilika ndani ya mwezi mmoja tu.
Tujipe muda katika kuifanya kazi kwa ufanisi zaidi. Ingawa wapo
wanaosema kuwa sababu ya kufanya kazi haraka haraka ni kutokana na
matatizo ya pesa ambapo mtu huhitaji kupata pesa haraka ili atatue
matatizo yake. Lakini tunasahau kuwa ukitoa kazi nzuri yenye ubora hukaa
na huuzika miaka nenda miaka rudi, tofauti na kazi zetu ambazo baada ya
wiki mbili zinakuwa hazina tena soko.
Tukumbushane kujipa muda
katika uandaaji wa filamu zetu: Mwezi mmoja wa mikutano kupanga mambo
(wapi itapigwa picha, nani atafanya nini, waigizaji watatoka wapi,
watafanya nini), mwezi mwingine kupanga usanii (mazoezi ya waigizaji,
mazingira yao), mwezi mwingine wa kupiga picha. Baada ya miezi mitatu,
mingine miwili ya kuhariri na kusahihisha makosa.
Ndipo sasa
kifuate kipindi cha kuitangaza kusudi iuzwe. Ukichunguza sana utagundua
kuwa sinema haiwezi kumalizika chini ya miezi sita kwa mazingira ya
Tanzania. Ndiyo maana wenzetu wanatoa sinema moja tu kwa mwaka lakini
pesa wanazopata wanakula kwa miaka kibao. Sisi tunatoa sinema kila mwezi
lakini pesa yake ni ya kujikimu tu.
Ni wakati sasa umefika tushirikiane, tuzichangamkie na tuangalie sinema zetu, tuzifurahie na tupeane moyo…
Sekta ya filamu Tanzania kwa sasa inajulikana duniani licha ya matatizo yake, licha ya mtayarishaji wa filamu wa Tanzania kuendelea kuishi maisha yasiyo tofauti na mtu mwingine wa kawaida! Hali halisi ya soko la filamu nchini inabana sana uwezekano wa kuibuka kwa wasanii, watayarishaji au waongozaji wapya...
Sidhani kama kuna mtu atabisha kuwa filamu za kibongo ‘hazitesi’ katika ukanda wa Afrika Mashariki na maeneo ya Maziwa Makuu. Filamu hizi zimesaidia kwa kiwango fulani kuitangaza nchi hii, kuwatangaza wasanii wa nchi hii, lakini vipi kuhusu maisha ya wasanii hawa? Je, wanapata stahili yao na wanaishi kwa kutegemea filamu pekee?
Kinachosikitisha zaidi: utoaji wa hizi filamu zetu imekuwa kama mchezo wa soka bila refa, sawa na mkutano bila mwenyekiti, darasa bila mwalimu, au nyumba (familia) bila mzazi…
Wafanyabiashara wanaahidi milioni kumi na tano hadi ishirini na ushee kwa sinema; watoaji sinema wanalipua kazi; waigizaji hawalipwi vizuri; utengenezaji sinema unafanywa haraka haraka. Sinema zinatengenezwa kwa wiki moja na zinatolewa ndani ya mwezi mmoja tu. Haraka haraka…
Wasanii wa filamu wanaigiza bila script wala mazoezi, watengenezaji filamu wengi wanatumia mwanya huo kula uroda na wasichana wazuri wazuri (ndiyo maana siku hizi kuwa miss ni kigezo kikubwa cha kupata nafasi ya kucheza filamu, haijalishi kama una kipaji cha kuigiza au la), sinema zinazotolewa nchini eti zinalinganishwa na za Wanaijeria! Tangu lini sinema za Wanaijeria zikawa kipimo cha filamu?
Kwa nini tufuate nyayo za Nollywood katika kuzalisha sinema zetu? Kwa kipi hasa? Hii inatufanya kusimulia hadithi zao; angalia sinema zetu zinavyosimulia uchawi, zinavyosimulia mapenzi au mikasa ya kijamii utagundua hilo. Tunaiga hadithi zao, namna yao ya uchezaji, sinema zao ambazo nyingi zimekuwa zikiigwa kutoka mataifa ya Magharibi na India.
Hivi Watanzania tumelogwa? Hii ni kwa Watanzania wote. Kwanini hatupendi/ hatununui sinema zinazotolewa na Watanzania wenzetu? Kisa? Hazituvutii. Moja ya sababu ni kwamba zinatengenezwa vibaya kwa kulipuliwa. Lakini kwa nini hata sinema zinazotengenezwa vizuri bado hatuzinunui? Kwa nini hatuzifurahii? Kwa nini hatuzitolei maoni na kuzitangaza? Tunachoweza ni kuziponda tu! Hivi hatudhani kuwa hiyo ndiyo njia kuu itakayotufanya tuendelee kama wenzetu, tunaowaona Miungu kutuzidi?
Kwa upande wa waandaaji wa filamu tukumbushane kwamba sinema ni sanaa inayochukua muda. Hatuwezi kutengeneza sinema ikakamilika ndani ya mwezi mmoja tu. Tujipe muda katika kuifanya kazi kwa ufanisi zaidi. Ingawa wapo wanaosema kuwa sababu ya kufanya kazi haraka haraka ni kutokana na matatizo ya pesa ambapo mtu huhitaji kupata pesa haraka ili atatue matatizo yake. Lakini tunasahau kuwa ukitoa kazi nzuri yenye ubora hukaa na huuzika miaka nenda miaka rudi, tofauti na kazi zetu ambazo baada ya wiki mbili zinakuwa hazina tena soko.
Tukumbushane kujipa muda katika uandaaji wa filamu zetu: Mwezi mmoja wa mikutano kupanga mambo (wapi itapigwa picha, nani atafanya nini, waigizaji watatoka wapi, watafanya nini), mwezi mwingine kupanga usanii (mazoezi ya waigizaji, mazingira yao), mwezi mwingine wa kupiga picha. Baada ya miezi mitatu, mingine miwili ya kuhariri na kusahihisha makosa.
Ndipo sasa kifuate kipindi cha kuitangaza kusudi iuzwe. Ukichunguza sana utagundua kuwa sinema haiwezi kumalizika chini ya miezi sita kwa mazingira ya Tanzania. Ndiyo maana wenzetu wanatoa sinema moja tu kwa mwaka lakini pesa wanazopata wanakula kwa miaka kibao. Sisi tunatoa sinema kila mwezi lakini pesa yake ni ya kujikimu tu.
Ni wakati sasa umefika tushirikiane, tuzichangamkie na tuangalie sinema zetu, tuzifurahie na tupeane moyo…
- Goddy Semwaiko Asante kwa mawazo mazuri na mchango mkubwa wa ushauri.
Kuhusu kutonunua Video za Bongo (Hata siku moja sintaziita Filamu, kwani si filamu)
Bishop inakuwa ngumu kununua kitu kisichokuwa na ubora, na hata ikitokea mojawapo ina ubora, inakuwa ngumu kuigu...See More - Goddy Semwaiko Kama Music Video ya dakika 4 inatengenezwa kwa ubora, wasanii wanahangaika mpaka wanasafiri nje ya nchi kutafuta ubora, inakuwaje Video za maigizo za dakika 90-120 zisitengenezwe kwa ubora?
Nadhani wanaweza kupiga mahesabu vizuri tu na kujipanga.
WEMA SEPETU AFUNGUA OFISI YAKE RASMI LEO
Posted by bongofilmdatabase udaku 5:01 PMKWA MAVAZI HAYA BASHIRI NI SCENE GANI ALIKUWA ANAJIAANDA KUCHEZA MSANII HUYU?
Posted by bongofilmdatabase habari, mpya, slide, udaku 8:30 PM
Mamtei-mwigizaji
Enyi wajumbe wa TAFF na Bongo Movie kwenye kamati za maadili jipangeni na kemeeni hili kwa nguvu zenu za ziada wala sio utani maana washirika wenu hawana nidhamu ya mavazi kabisa ila leo karamu yetu itaangazia juu ya somo la mavazi kwa wasani wetu hapa nchini.
Somo la mavazi pindi mtokapo mitoko yenu na kwenye kufanya kazi zenu linatakiwa litolewe kwa msanii mmoja baada ya mwingine na sio kuzungumza jambo hili kwenye majukwa kama wanasiasa na kwenye mahojiano(interview) na kulijibu kwa juu juu tu ili muda uende pindi muulizwapo kwani mnawakera sana wadau wenu wanaowafuatiliya kila siku.
Hebu tizameni hili vazi la dada huyu ambalo lina tia mshangao kidogo tukilinganisha na mazingira ya kibongo kwa jinsi yalivyo na joto la kawaida tu ambalo sidhani linamlazimu mtu avae nguo yenye mtindo wa chandalua tena yenye matundu makubwa kiasi hiki kama nyavu ya kuvulia dagaa au samaki na cha kushangaza kwa dada huyu ni namna alivyo changanya mavazi haya yanayovaliwa katika mazingira tofauti tofauti ambapo vazi moja huvaliwa kwenye mazingira ya joto na hilo koti lenye manyoya huvaliwa kwenye mazingira ya baridi...
1.sasa swali kwa msani huyu ni kwamba, alikuwa amezamilia kujikinga na baridi au joto hapa mjini?!
2.Somo la namna ya kuvaa wasani ni kazi ya wanamitindo wa hapa nchini au ni wasani wenyewe?
WASANII HII SI YAKUACHA KUSOMA KWANI INAWAHUSU SANA
Posted by bongofilmdatabase kinyemi, slide, udaku, workshop 5:39 PM
MAKALA NA TRIM SALEEM (Trim Saleem)
Suala la usambazaji wa films za kitanzania ni moja ya vitu vinavyolalamikiwa sana kuwa limejaa upendeleo kwa wasanii wenye majina makubwa na wachanga kupuuzwa, vile vile hata hao wenye majina nao wananyonywa kama kawa licha ya
kwamba uharamia nao unaonekana kuota mapembe bila juhudi thabiti za kuuteketeza ingawa upo duniani kote. ila inatakiwa wasanii kuungana na pia kuishinikiza serikali ili ijenge majumba ya cinema maana haya huwa ndiyo chanzo kikubwa cha mapato ya films na hata kuamuliwa kama film ni hit or flop kutokana na kuwa wazi zaidi hasa katika suala la uuzaji wa tiketi kuliko uuzaji wa dvd, vcd, net au tv broadcast ingawa vyote hivi ni vyanzo vikuu vya mapato ila majumba ya sinema ndo hutegemewa zaidi.
Hapa nchini kuna majumba machache ya sinema lakini ukiyaangalia sana ni kama hayapo Tanzania maana mara nyingi yanaonyesha films za hollywood na bollywood/ india ingawa pia watengenezaji wa films za kitanzania wanaonekana kukosa ufahamu au weledi wa kutumia majumba haya, ila ikiwa wasanii wataungana na kufanya harambee za kukusanya pesa kwa kuanzia hata na majumba 2 au 3 kwa msaada wa serikali na wao wenyewe hili linawezekana na ni moja ya njia ya kuwashikisha adabu baadhi ya wasambazaji waliojaa unyonyaji huku wakikosa ubunifu wa namna ya kutangaza films ambazo sio za kimapenzi ili ziuzike yaani wasambazaji hawa ni kama hawana nia ya dhati ili films zetu zifike mbali ila mapenzi tu ndio films! suala hili linawezekana ikiwa wasanii wataacha kufanya sherehe au party zisizo na kichwa wala miguu kila siku na kuchangishana pesa nyingi kwenye harusi halafu ndoa zenyewe nyingi hazidumu zikiwa na lengo la kujionyesha tu mbele za watu ,na ikumbukwe kuwa kuna wafanyabiashara wazalendo wengi tu ambao wanaweza kuwa interested na hata kuwekeza kwenye project kama hizi ikiwa wataona wasanii wenyewe wana maono ya mbali ili kufanikiwa, na ikiwa hili litatiliwa maanani basi hata ndani ya miaka 5 ijayo tayari njia nzuri itakuwa ishaanza kuonekana kuliko hali ilivyo sasa msambazaji ndio huamua kuwa film imeuza au haijauza hata kabla haijaingia sokoni wakati wa kuliamua hili ni wanunuzi au mashabiki wenyewe baada ya kuona film sokoni .
Ukweli ni kuwa Tanzania ina nafasi kubwa sana ya kufanya vizuri kuliko hata Nigeria maana Nigeria yenyewe imeanza muda kidogo ila kuna films nyingi ukiziangalia zina makosa kibao kama za kibongo na hii ndiyo sababu licha ya Nigeria kuzalisha utiriri wa films kibao kila siku lakini nyingi zinashindwa kushindana na chache kutoka south Afrika ambazo zinatamba mpaka nje ya bara la afrika wakati za Nigeria nyingi zimeishia barani afrika. Ikiwa tutaendelea kutegemea uuzaji wa dvd na vcd kama chanzo kikuu cha mapato wakati india na hollywood huwa chanzo kingine baada ya majumba ya cinema hatuwezi kuwa mabilionea kupitia films hata siku moja na amin usiamini majumba ya sinema yakijengwa wasambazaji watakuwa na nidhamu kwa maproducer na hata kuwashobokea ili wafanye biashara kuliko sasa, pia haya majumba machache yaliyopo yataacha kasumba zao na kugeukia films za kitanzania. ila hili litawezekani kwa asilimia kubwa huku tukiwa tunazidi kuziboresha films zetu ili huko kwenye cinemas tusije kuwachosha watu kama ilivyo sasa mtu hata nyumbani kwake film ya kibongo inamboa . suala la kuwa sisi ndo kwanza tumeanza lisiwe kigezo cha sisi kuchukuwa miaka kibao ili kufika mbali maana walioanza zamani mazingira yao yalikuwa magumu kuliko ulimwengu wa leo. pichani ni THEA 1 wa waigizaji wetu wachache wenye viipaji halisi ambavyo vinatakiwa ili kuifikisha tasnia hii anga za kimataifa
MWANDISHI WA LILE GAZETI NA STORY YA KUFUMANIWA DADA HUYU UNAJISIKIA VIPI PINDI UIONAPO HII PICHA?
Posted by bongofilmdatabase habari, mitandao, mitandaoni, mpya, slide, udaku 7:08 AM
MWANDISHI WA GAZETI LILE LILILOSEMA BIBI HARUSI MTARAJIWA AFUMANIWA BAADA TU YA SEND OFF AKIIONA HII ATAJISIKIA VIPI?
UKURASA HUU NA WADAU WA MWIGIZAJI HUYU WALAANI SANA KITENDO CHA HIKI CHA KUANDIKA VIBAYA WASANII, CHINI NI MOJA YA WADAU MWIGIZAJI HUYU AKILAANI JUU YA HILI KUPITIA UKURASA WAKE WA FACEBOOK
STATUS:
OOOH KAFUMANIWA OOOH SIKU MOJA BAADA YA SEND OFF ACHENI HIZO HII NINI SASA.... WANAMEREMETA BWANA.............. LONG LIFE
- Myovela Mfwaisa, Daudi Michael Mpya and 8 others like this.
- Ladyd Lumelezy KWELI NDUGU ZANGU WATU WANAPENDA KUONGEA SIJUHI WANAONA SIFA AUNTY HUYOOOOOOOO MWAAAAA
CHANZO CHA STATUS NA PICHA;
Deo Mutta Mwanatanga
TRAILER HII YA MAGIC MONEY INAFAA KUUZIWA NA KASHA LIPI KATI YA HAYA?!
Posted by bongofilmdatabase habari, mpya, slide, udaku 8:43 PM
''PESA SHETANI ASIYE EPUKIKA KATIKA DUNIA YA SASA NA USIOMBE ABISHE HODI NDANI YA FAMILIA KABISA''
...KUMKANYWA NA KUPEWA TAHADHALI KWA MTU NDIYO KUMTIA HAMASA NA MUWASHAWASHA KUITIKIA KIU YA NAFSI YA TAMAA YA PESA .
MAISHA YA KUKIMBIA NDIYO MATOKEO YAKE KAMA SIO KUKOSANA NA NDUGU AU MPENZI/MUME/MKE WAKO... BASI MTIZAME BINTI HUYU NAMNA NDOA YAKE INAVYO TIBULIWA NA SHETANI HUYU (PESA).
HILI NDILO KASHA JIPYA LA FILAMU YA MAGIC MONEY ITAKAYOINGIA SOKONI MWEZI HUU
HILI NDILO LILIKUWA KASHA LA FILAMU HII YA MAGIC MONEY KABLA YA KUINGIA SOKONI
TIZAMA TRAILER YA FILAMU HII HAPA CHIINI YENYE DAKIKA TATU TU NA UTUMBIE NI KASHA LIPI LILISTAHILI KUTOKA NA FILAMU HII
{EXCLUSIVE} MPENZI NA MDAU WA STEVEN KANUMBA ISIKILIZE NYIMBO YAKE MPYA .
Posted by bongofilmdatabase mpya, slide, udaku 7:08 PM
moja ya nyimbo za marehemu steven kanumba aliyoimba maalumu kwa Mama yake mzazi, Flora Mutegoa.
BOFYA KIUNGA HICHO HAPO CHINI KUSIKILIZA NYIMBO HII.
BOFYA KIUNGA HICHO HAPO CHINI KUSIKILIZA NYIMBO HII.
TRA NA SHIRIKISHO LA FILAMU VYAAPA ADHALANI
Posted by bongofilmdatabase habari, mpya, slide, udaku 10:31 PM
Shirikisho la Filamu nchini(TAFF) kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) pamoja Kampuni za usambazaji wa
filamu na kazi za wasanii ‘zimeapa’ kupambana na maharamia wote wa kazi hizo
ili kulinda maslahi ya wasanii.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar
es salaam jana, umoja huo kwa pamoja ulisema umefika wakati tatizo la wizi wa
kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya yote ambayo ni kero
kwa muda mrefu.
Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati
hiyo pia aliiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa
kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii huku
wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.
“Umefika wakati kwa Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii
na kuweka mbinu kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa
masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi zao”
“Tuna imani kuwa kama kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri,
tutaweza kuongeza pato la Taifa kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa sanaa hii
kwa sasa hapa nchini imeonyesha mafanikio isipokuwa kuna watu wachache ndiyo
wananufaika nayo” alisema Mwakifwamba.
Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa
inaweza kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato
linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja na utalii.
Alisema Serikali inapswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata
wahusika wote wa wizi wa kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa
nchini walioamua kujitoa mughanga kufanya kazi zao.
Kwa upande wake Meneja usimamizi kutoka TRA Msafiri Ndimbo
alisema Mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari
Mwakani hasa baada ya Serikali kupitia Bunge lake kukubalina kuweka mikakati ya
kupamba na suala hilo.
Ambapo wasanii na wasambazaji wa kazi zao wameungana pamoja
kwa ajili ya kuhakikisha kazi zao zinakwebnda kwa haki ili wasanii wapate na
wao wawe ni watu wa kusaidi wasanii kusambaza kazi zao
Na mdau wetu; markus Mpangala
MKONO MWINGINE WA UPANGAJI PICHA ZA MAKASHA YA FILAMU
Posted by bongofilmdatabase kinyemi, mpya, slide, udaku 1:24 PM
Katika pita pita tumekutana na kava moja matata sana inayoashiria ni Movie ya kibongo iitwayo A LONDON GIRL! Moja kwa moja kutokana na ubunifu mzuri wa kava ya filamu hiyo tukapata jibu kuwa hii kitu ikiingia street lazima iuze.
Kava hiyo imetengenezwa na kampuni changa ya Kibongo iitwayo I-Dentity Designs. Kwa kutaka kujua zaidi kuhusiana na movie hiyo ambayo kava lake linaashiria kuwa ni high-budget movie kibongobongo tukaipigia simu kampuni hiyo kutaka kujua zaidi kuhusiana na project hiyo.
Hata hivyo taarifa ya mbunifu wa kazi hiyo ikatuambia kuwa kumbe amedesign tu kama sample ili kuonesha uwezo wake. Hakika ni kwamba kama kweli kukiwa na idea ya movie kama hii Bongo tunahisi itafanya vizuri sana hasa kama story ikiwa kwa mfano msichana huyo wa London labda kaja Bongo na kukimbiza sana kitaa then kunakuwa na story ya mapenzi inayomzunguka binti huyu.
Ama inaweza kuwa mbongo ameenda London na akakutana na msichana mrembo wa London ambaye anajikuta akimzimia kinomanoma! Sounds like a catchy synopsis right?
Chanzo;Leotainment
LETS HOOK UP
.

.
slide
