WASANII HII SI YAKUACHA KUSOMA KWANI INAWAHUSU SANA




MAKALA NA   TRIM SALEEM (Trim Saleem)
Suala la usambazaji wa films za kitanzania ni moja ya vitu vinavyolalamikiwa sana kuwa limejaa upendeleo kwa wasanii wenye majina makubwa na wachanga kupuuzwa, vile vile hata hao wenye majina nao wananyonywa kama kawa licha ya 

kwamba uharamia nao unaonekana kuota mapembe bila juhudi thabiti za kuuteketeza ingawa upo duniani kote. ila inatakiwa wasanii kuungana na pia kuishinikiza serikali ili ijenge majumba ya cinema maana haya huwa ndiyo chanzo kikubwa cha mapato ya films na hata kuamuliwa kama film ni hit or flop kutokana na kuwa wazi zaidi hasa katika suala la uuzaji wa tiketi kuliko uuzaji wa dvd, vcd, net au tv broadcast ingawa vyote hivi ni vyanzo vikuu vya mapato ila majumba ya sinema ndo hutegemewa zaidi.

Hapa nchini kuna majumba machache ya sinema lakini ukiyaangalia sana ni kama hayapo Tanzania maana mara nyingi yanaonyesha films za hollywood na bollywood/ india ingawa pia watengenezaji wa films za kitanzania wanaonekana kukosa ufahamu au weledi wa kutumia majumba haya, ila ikiwa wasanii wataungana na kufanya harambee za kukusanya pesa kwa kuanzia hata na majumba 2 au 3 kwa msaada wa serikali na wao wenyewe hili linawezekana na ni moja ya njia ya kuwashikisha adabu baadhi ya wasambazaji waliojaa unyonyaji huku wakikosa ubunifu wa namna ya kutangaza films ambazo sio za kimapenzi ili ziuzike yaani wasambazaji hawa ni kama hawana nia ya dhati ili films zetu zifike mbali ila mapenzi tu ndio films! suala hili linawezekana ikiwa wasanii wataacha kufanya sherehe au party zisizo na kichwa wala miguu kila siku na kuchangishana pesa nyingi kwenye harusi halafu ndoa zenyewe nyingi hazidumu zikiwa na lengo la kujionyesha tu mbele za watu ,na ikumbukwe kuwa kuna wafanyabiashara wazalendo wengi tu ambao wanaweza kuwa interested na hata kuwekeza kwenye project kama hizi ikiwa wataona wasanii wenyewe wana maono ya mbali ili kufanikiwa, na ikiwa hili litatiliwa maanani basi hata ndani ya miaka 5 ijayo tayari njia nzuri itakuwa ishaanza kuonekana kuliko hali ilivyo sasa msambazaji ndio huamua kuwa film imeuza au haijauza hata kabla haijaingia sokoni wakati wa kuliamua hili ni wanunuzi au mashabiki wenyewe baada ya kuona film sokoni . 

Ukweli ni kuwa Tanzania ina nafasi kubwa sana ya kufanya vizuri kuliko hata Nigeria maana Nigeria yenyewe imeanza muda kidogo ila kuna films nyingi ukiziangalia zina makosa kibao kama za kibongo na hii ndiyo sababu licha ya Nigeria kuzalisha utiriri wa films kibao kila siku lakini nyingi zinashindwa kushindana na chache kutoka south Afrika ambazo zinatamba mpaka nje ya bara la afrika wakati za Nigeria nyingi zimeishia barani afrika. Ikiwa tutaendelea kutegemea uuzaji wa dvd na vcd kama chanzo kikuu cha mapato wakati india na hollywood huwa chanzo kingine baada ya majumba ya cinema hatuwezi kuwa mabilionea kupitia films hata siku moja na amin usiamini majumba ya sinema yakijengwa wasambazaji watakuwa na nidhamu kwa maproducer na hata kuwashobokea ili wafanye biashara kuliko sasa, pia haya majumba machache yaliyopo yataacha kasumba zao na kugeukia films za kitanzania. ila hili litawezekani kwa asilimia kubwa huku tukiwa tunazidi kuziboresha films zetu ili huko kwenye cinemas tusije kuwachosha watu kama ilivyo sasa mtu hata nyumbani kwake film ya kibongo inamboa . suala la kuwa sisi ndo kwanza tumeanza lisiwe kigezo cha sisi kuchukuwa miaka kibao ili kufika mbali maana walioanza zamani mazingira yao yalikuwa magumu kuliko ulimwengu wa leo. pichani ni THEA 1 wa waigizaji wetu wachache wenye viipaji halisi ambavyo vinatakiwa ili kuifikisha tasnia hii anga za kimataifa

Posted by bongofilmdatabase on 5:39 PM. Filed under , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for WASANII HII SI YAKUACHA KUSOMA KWANI INAWAHUSU SANA

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign