KWA MAVAZI HAYA BASHIRI NI SCENE GANI ALIKUWA ANAJIAANDA KUCHEZA MSANII HUYU?

Mamtei-mwigizaji
Enyi wajumbe wa TAFF na Bongo Movie kwenye kamati za maadili jipangeni na kemeeni hili kwa nguvu zenu za ziada wala sio utani maana washirika wenu hawana nidhamu ya mavazi kabisa ila leo karamu yetu itaangazia juu ya somo la mavazi kwa wasani wetu hapa nchini.

 Somo la mavazi  pindi mtokapo mitoko yenu na kwenye kufanya kazi zenu linatakiwa litolewe kwa msanii mmoja baada ya mwingine na sio kuzungumza jambo hili kwenye majukwa kama wanasiasa na kwenye mahojiano(interview) na kulijibu kwa juu juu tu ili muda uende pindi muulizwapo kwani mnawakera sana wadau wenu wanaowafuatiliya kila siku.

Hebu tizameni hili vazi la dada huyu ambalo lina tia mshangao kidogo tukilinganisha na  mazingira ya kibongo  kwa jinsi yalivyo na joto la kawaida tu ambalo sidhani linamlazimu mtu avae nguo yenye mtindo wa chandalua tena yenye matundu makubwa kiasi hiki kama nyavu ya kuvulia dagaa au samaki na cha kushangaza kwa dada huyu ni namna alivyo changanya mavazi haya yanayovaliwa katika mazingira tofauti tofauti ambapo vazi moja huvaliwa kwenye mazingira ya joto na hilo koti lenye manyoya  huvaliwa kwenye mazingira ya baridi... 

1.sasa swali kwa msani huyu ni kwamba, alikuwa amezamilia kujikinga na baridi au joto hapa mjini?!


2.Somo la namna ya kuvaa wasani ni kazi ya wanamitindo wa hapa nchini au ni wasani wenyewe?

Posted by Oscar TheCityDriver on 8:30 PM. Filed under , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for KWA MAVAZI HAYA BASHIRI NI SCENE GANI ALIKUWA ANAJIAANDA KUCHEZA MSANII HUYU?

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign