UANDISHI WA FILAMU NA MAIGIZO
JIFUNZE NAMNA YA KUANDIKA NA KUANDAA SCRIPTS
MUUNDO WA HADITH
SEHEMU YA PILI
2. MUUNDO WA ENEO ZIMA (SCENE) KAMILIFU LA NJAMA
Haijarishi
wazo ulilonalo ni zuri kiasi gani kwa ajili ya filamu, lakini kama
hauwezi kupata njia ya namna ya kusimulia hilo wazo lako, basi ni kazi
bure, atakama wazo ulilonalo linakufurahisha kila ukilifikiria. Ukiwa
kama mwandishi wa Script, unatarajiwa kuwa na Mfumo ambao utakusaidia
kuwa na uwezo wa kuamisha wazo lako kutoka katika Usingizi wako na kuwa
hadithi kamili.
Endelea…!
Jana nilitoa tafsiri ya maana ya njama katika Mtiririko wa somo ngoja nirudie tafsiri yake,
Njama ni nini?
Ni Tukio linalotengeneza hadithi,kawaida huwa ni Mkusanyiko
wa mambo yanayohusiana,kwa kiingereza huitwa Plot,ikiwa na maana ni kitu
kinachoitaji kitu kingine ili kukamilisha jambo zima, na katika Filamu
zipo nyama nyingi ambazo zote ni lazima zihusiane ili kutengeneza
hadithi kamili, na nilazima itafutwe kitu ambacho kitaunganisha nyama
moja mpaka nyingine ili kuikamilisha Hadithi katika mtiririko,.
Baada ya kupata kuelewa Maana ya Njama, sasa tuendelee...!
Leo, Tutajifunza Mambo Muhimu na ya kuzingatia ili Njama kuwa
kamilifu, kwa kuwa njama ni tukio moja linalotegemewa na tukio jingine,
ni vyema, ukazingatia Mazingira mazima ambayo yataunganisha Njama moja
mpaka nyingine ili kuleta Scene iliyo kamilifu
Nambo ya Msingi unayotakiwa kuyaweka akilini unapotengeneza Script
kwa ajiri ya kuunganisha Movie zima kwanza ni lazima uwe na wazo fupi,
ambalo utalitumia kuchota Matukio ndani ya hilo wazo, kama ifuatavyo;
Wazo Fupi
Wazo lako Fupi, ni lazima lielezewe katika sentesi moja au mbili. Mfano wa wazo la filamu:
“Nyerere kama Baba wa Taifa”,
hili ni wazo fupi na ukilichambua, utakutana na taarifa nyingi sana, na
kama Mwandishi wa Script ni lazima uwe na mfumo ambao utakusaidia
kuchambua hilo wazo na kuwa katika hadithi, Mfano wa Wazo jingine;
“Rose Muhando Malkia wa Muziki wa Injili”,
hili nalo ni wazo, lakini je ukilipeleka kwa watu na kulitamka kama
lilivyo kwa lengo la kutaka kutengenezwa Filamu, wazo hili
litashughuliwa?,

Jibu
ni “Hapana” kwamaana ndani ya hiyo sentesi kuna mwisho tu, je mwanzo
huko wapi, na katikati kukoje?. Ndiyo maana ni Vyema kama Mwandishi wa
script kuwa na Mfumo ambao, wazo likija kwako uweze kuligawa katika
Vipengere ambavyo Vitakusaidia kutengeneza Hadithi ya keleweka, na Bila
wazo hakuna Hadithi, wazo ni kama mbegu ndogo ya Haradani, ikifanyiwa
kazi huweza kuzaa simulizi kubwa na Ya kusisimua. Kwahiyo ili
usijeku-ishiwa kama Mwandishi ni vyema ukawa na kitabu chako cha
kumbu-kumbu ambamo utakuwa ukitunza kila wazo linalokujia. Kila sehemu
unayokuwa kama Mwandishi umezingirwa na wazo kwa ajiri ya Filamu, iwe
kwenye Dara-dara, uwanja wa Mpira, kijiwe cha kunywea kaawa.n.k.
Mara nyingi unapokwenda kulipeleka wazo lako kwa watengeneza
filamu,lazima huwe na maelezo ya kuambatana na hilo wazo, kuna wazo
ambalo ukilitamka tu, linainua hisia za watu na kuwafanya watake kujua
kuna nini ndani yake.hili ndilo linalo tendeka katika Hollywood,
unapopeleka script yako au kuituma ni lazima Mbele ya ganda (Cover), au
kurasa ya kwanza ndani ya ganda (Cover), liwe na hilo wazo, sentensi
moja au mbili, ili kuwaweka mguu sawa. Na ili kuendelea kuheshimu wazo
lako kwa kutoacha kusoma kumbuka kufuata Muundo tuliojifunza jana “
MIUNDO MITATU YA UIGIZAJI”
Baada ya Kuwa na wazo fupi, ndani ya Hadithi yako ambayo utaichambua
kutoka katika wazo lako fupi, jitahidi, kuingiza mambo yafutayo ili
kuwepo Ukamilifu wa Sceneu kutoka wa Njama moja mpaka nyingine;
Simulizi zilizopita (Backstory)
Simulizi zilizopita ni Maisha ya zamani ya Wahusika ambayo yanasaidia
hadhira kuelewa namna Wahusika walivyo (wao ni nani haswa) na hadithi
yenyewe inahusu nini, hii hufanyika kwa Muhusika kuwaza, Taarifa za
namna hii zinatakiwa kuwasilishwa kupitia Tabia ya Wahusika na
Mazungumzo. Na pia unaweza kutumia mbinu ya moja kwa moja (Narration) au
mbinuo (Flashback), lakini kuna Imani kwa baadhi ya watu kwamba
utumiaji wa mbinu hizi unaonesha uandishi wa kivivu, hizo ni Imani tu za
watu wachache, lakini katika soko la Uandishi wa script hizi ni za
Muhimu sana, kutegemeana na Filamu yenyewe.Utoaji wa taarifa za nyuma
kidogo-kidogo katika Filamu ni muhimu sana kuliko kuwasilisha Simulizi
zilizopita kiujumla,utoaji wa Jumla unapoteza hamu ya kuangalia Filamu
kwasababu, lengo la kutoa kidogo-kidogo, ni ili kumfanya msomaji
kutamani kuendelea kutafuta jibu zaidi. Msingi mzuri wa kutoa simulizi
zilizopita ni kwa kutoa maisha yaliyopita taratibu, kinyume na hapo
script yako itakosa nguvu na itachukuliwa kuwa hafifu.
Utambulisho wa Ukweli uliofichwa (Exposition)
Ukweli uliofichwa , hii ni taarifa ambayo ipo katika hadithi yenyewe
ambayo hadhira inaitaji kuifamu kwa ujumla wake na kufichwa kwake ndiyo
kusudio la Hadithi, na lengo ni kuifichua taratibu. Kwa mfano katika
Filamu ya Jim Carrey itwayo “
The Truman Show” ambapo.Jim Carrey
kama Muhusika Mkuu anajaribu kuchukua Merikebu (boat) ili atoke nje ya
mji lakini hawezi kwasababu ya hofu ya maji, Hofu inakuja kutokana na
historia ya Kufa maji kwa baba ye kipndi akiwa Mdogo wakiwa pamoja
katika Merikebu, ukipata nafasi ya kuiangalia filamu hii utakuta siri
nyingi ambazo taratibu zinaanzakufunguliwa na mwisho kama hadhira
unaanza kuelewa kwamba Jim Carrey alikuwa akiishi maisha ambayo si ya
Ukweli japo kuwa yeye alidhania ya ukweli, na katika eneo hilo kama
mtazamaji unaanza kuchukuliana na Jim Carrey, na kwa pamoja mnaanza
kutafuta njia ya kuujua Ukweli. Kwa hiyo kama mwandishi wa script Jaribu
kutambulisha huu ukweli kwa utaalamu,kimatendo na pia kupitia migogoro,
wakati wa kufichua ukweli huu jaribu sana kutumia Vitendo kuliko maneno
“Onyesha,usisimulie”, Hapa napenda niongee kitu kimoja kuhusu Filamu
zetu za KIBONGO, huwa tunakosa hii sehemu, kwamaana ukweli sikuzote huwa
tunautambulisha kwa maneno kuliko matendo, hii inapoteza utamu wa
Movie, Japokuwa zipo baadhi ambazo zinajitahidi kuitumia mbinu hii, Kuna
filamu moja ya Kibongo ambayo ninaomba uitafute kwa maana katika eneo
hili imefanya Vizuri sana nayo inaitwa
“SIMU YA KIFO”
Kima (Pace)
Soma Script yoyote na utaona tendo moja linafafanua umbali wa hadidhi
ulivyo, hii huitwa kima (Pace). Kima ni namna ambavyo utamfanya msomaji
aone kwamba hadithi bado inaendelea au imewkisha,Chukulia mfano wa zile
treni za milimani, zinazo kaa angani kutoka mlima mmoja kwenda mwingie
kwa kutumia kitu mfano wa chuma ambacho kimeshikilia ile treni,treni
hizi zipo pia huko Urusi zinaitwa kwa kiingereza Roller Coster, Sasa
fikiria kwamba inapopanda juu huenda kwa kasi na inaposhuka hupunguza
mwendo, Hadithi ipo kama hivyo, ikiwa na maana hadithi ni Treni ya
Hisia, Vikwazo vinapozidi kuwa vizito, ndipo scene huwa fupi, hii hali
huifanya hadithi yako kuwa na mvuto zaidi kwa maana humfanya msomaji
kutokuchoka. Ni kama vile ronaldo yupo na mpira yeye na gori kipa dakika
za lala salama, kisha Tanesco wanazima umeme. Kima ni Muhimu kufikiliwa
ili kuleta attention kwa wasomaji, usimalize kila kitu kwenye scene
moja, bali kila scene utakayoitengeneza iache nafasi kwa scene nyingine.
Scene moja inaweza kusema hadithi bado inaendelea au tumekaribia mwisho
au Imeisha
.
Mapumziko/Sehemu ya Marejeo (Turning Points)
Kwakweli Mapumziko au Sehemu ya Marejeo yanaitajika sana katika
huandaaji wa Script, kwamaana movie yoyote inasehemu ya Marejeo, ambayo
inatoa mwanya kwa hadithi kupanda viwango zaidi, sehemu hii itampa wazo
jipya Muhusika au wahusika, na kuwageuza katika Mwelekeo mpya, kila
wakati hadithi inapoonekana kumpotezea tumaini Msomaji, ni lazima
uingize kitu ambacho kitarejesha tumaini, katika hadithi, tambua kwamba,
Muhusika utakaye mjenga, wasomaji watapenda wamtetee au kutamani
kumuambia ajiepushe na jambo lililo-mbele yake ambalo msomaji ameliona
lakini Muhusika hajaliona, hali hii ikiendelea, inampoteza Msomaji kwa
hiyo ni vyema ukatengeneza kitu ambacho kitaleta haueni kwa Mhusika na
kwa njia hiyo, unaleta haueni pia kwa Msomaji. Japo kuwa hadithi itakuwa
haijaisha ila bado mapambano yanaendelea lakini atapumua kwa Muda
kidogo.njia hutumiwa sana katika Maigizo ya Masafa marefu (Tamthiria(TV
Serie-Soap)
Vipingamizi
Vipingamizi ni nguvu za upinzani kutoka ndani au nje ya Muhusika
ambavyo vinampinga Muhusika Mkuu kufikia malengo yake, unaweza
kutengeneza kikwazo,kwa mfano, wanamgambo wa jiji wanaokuja kubomoa
kibanda cha Muhusika wako ambaye wakati huo ametumia fedha nyingi ili
kununua hizo bidha walizo ziharibu, unaweza kumfanya muhusika ajitete
lakini kila akijitetea ndiyo makubwa yanazidi. Kwa hiyo Vipingamizi ni
muhimu ili kutengeneza kisa kizuri.kinachofuata
Kejeri;
Hapa ni pale,Mwandishi anapo ruhusu Hadhira wafahamu kitu ambacho
Muhusika hakijui, kwa mfano, Muhusika anapo tembea na msicha ambaye
hadhira inafahamu kuwa ni Mwingi wa habari, japokuwa Muhusika mkuu
hafahamu hilo. Na nyumba aliyoipanga wanaume hawaishi, hi ni kejeri. Na
pindi mwanaume anapofahamu inamfanya hajione mjinga hali inatengeneza
scene nyingine.
Kilele
Hiki ni kipande kikubwa katika Filamu, ambapo wema unapambana kinyume
na uovu, katika eneo hili ndipo hadithi nzima hufunganishwa, Muhusika
Mkuu nilazima apambane vita vya mwisho, iwe kimisuli au kihisia.
Utatuzi
Kipande cha mwisho cha Filamu kinaitaji kuonesha kwamba kila kitu
kimerudishwa katika utulivu, na aliyekuwa hajiwezi sasa amejiweza,
katika sehemu ya mwisho majibu yote ambayo Muhusika alikuwa nayo
nilazima yajibiwe, Filamu isijaribu kujibu swali ambalo halikuwepo
katika Filamu tangia mwanzo, Kwamfano katika Filamu zetu utakuta
mwishoni, Muhusika anapambana na adua kwa kungfu, wakati takingia mwanzo
hapakuwa hata na mazingira ya wazi hau ya kuficho ya kuwepo jambo hilo,
unakuta katika maisha yake kama Muhusika haijawai kuoneshwa hakiwa na
moyo huo wa kujifunza kungfu na wala kungfu haipo sasa unajiuliza hizi
kungfu amezitoa wapi, kwa hiyo filamu ni lazima hijibu swali sahihi.
chanzo;global publisher na
FREDY SULEIMAN OKUKU
Asante!