ZIJUE SERIES ZILIZOTAMBA NA ZINAZOBAMBA KWA SASA UKIANZIA NA YA ARROW ( Eps 1 )


Katika nyumba tano hapa mjini kwa sasa iishiyo vijana wapendao filamu zitokazo hollywood basi nyumba mbili kama sio tatu katika ya hizo tano wanafuatilia series au ziite filamu zenye mwendelezo wa mikasa na matukio yaani tamthilia kwa lugha ya kawaida, kuna series nyingi sana zimewahi tayarishwa huko marekani mpaka sasa ila miongoni mwa series zilizopata wafuatiliaji wengi sana hapa mjini na Tanzania yote kwa ujumla wake wakiwemo na hao vijana  niliyowazungumzia hapo awali ni series kama Prison Break, 24hours, Lost , Vampare Diary na nyingine nyingi tu.

Leo katika Big Screen yetu tutaizungumzia series inayokwenda kwa jina la ARROW kama top cover yake unavyo iona hapo juu. filamu hii ni moja ya filamu ninaimani ukithubutu kuianza kuitizama tu sehemu yake ya  kwanza  kiukweli huwezi kuacha kutafuta sehemu ya pili na nyingine zote zifuatiazo  na kukaa chini kuzitizama na hata  mwisho wake kuwa shabiki moja mkubwa miongoni mwa wafuatiliaji ambao hupanga foleni katika internet cafe kuzidownload kila mwisho wa wiki kwa mwajibu wa taratibu wa watayarishaji kuzitoa kila jumatano baada ya kuzionesha kwenye television zao za kibiashara huko marekani na kuziachia kwenye kurasa za mitandaoni kila alhamisi kuwapa fursa wadau wengine kuzidowload kila ijumaa.

ARROW ni filamu ambayo inamzungumzia kijana mmoja aitwae Oliver kutoka katika moja ya familia tajiri kwenye mji wa Starling aliyokuwa akiishi humo nchini marekani ambaye alinusulika kupoteza maisha kwenye ajali ya boti waliyokuwa wakisafilia aliyokuwemo na watu wengine watatu ambao ni baba yake mzazi,msaidizi wa baba yake na mwongozaji boti ile na rafiki wa kike kipenzi.

Oliver hakupata mawasiliano na familia yake aliyoicha huku mjini kwa taklibani miaka mitano  kitendo kilicho wafanya ndugu, jamaa na marafiki wote kuamini wote waliyokuwemo kwenye ile boti katika safari ile walikufa maji. ila Oliver alinusulikia na kuvuka mpaka kisiwa kimoja kilichopo huko Pacific, baada miaka mitano kupita iliyokuwa imetawaliwa na mateso makali na shuluba ya kuwindana na watu waliyokuwa hawana utu kabisa akijitahidi kupigania maisha yake Oliver ana bahatika kupata upenyo na kutoloka kisiwani humo na kurejea mjini.

kijana Oliver anarudi mjini na mbinu nyingi sana alizojifunza huko kisiwani atakazozitumia kurekebisha na kusahihisha makosa yaliyofanywa na familia yake uhususani baba yake na watu wengine waliyokuwa wamefanya na kufanya vitu visivyokuwa sawa na kuukosea mji wa Starling, ila swali la kujiuliza ni kwamba atasahihishaje makosa yote hayo?! ndipo  Oliver anaamua kutengeneza na kujenga uhusika mpya feki wa bwana mmoja alijulikana kama VIGILANTE kwa maana ya mtu ambaye anajichukulia maamuzi mkononi yaani anavunja sheria pale anahitaji fanya vitu vyake, Vigilante huyo alikuwa anatumia silaha ya aina ya mishale.

Leo Big Screen yetu tumeanza na utambulisho na maelezo mafupi juu ya sreies hii ya Arrow ambayo mpaka sasa ipo ungwe ya kwanza tu onesho la kumi na tisa, Big Screen(Bs) ifuatayo tutaangazia wahusika mmoja baada ya mwingine kisha kuendeleza simulizi hili tamu la Series ya ARROW


OLIVER- STEPHEN AMELL 
Staa na muhusika mkuu wa series ya Arrow wambaye tutamwelezea zaidi kwenye simulizi lifuatalo ambapo tutaangazia maisha yake ya nje ya sanaa na ni kazi ngapi amewahi na kutarajia kuzifanya mpaka sasa. Tafadhali wafahamishe washikaji tusiwaache nyuma kwenye simulizi hili la kusisimua na kama utapenda kujiunga na jopo la kusimulia maonesho mengine ya ndani ya series hii na kuambatanishwa kwenye  Big Screen yetu usisite kutucheck kupitia 0719 71 93 16 sasa.

Posted by bongofilmdatabase on 4:10 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for ZIJUE SERIES ZILIZOTAMBA NA ZINAZOBAMBA KWA SASA UKIANZIA NA YA ARROW ( Eps 1 )

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign