UANDISHI WA FILAMU NA MAIGIZOUANDISHI WA FILAMU NA MAIGIZO
JIFUNZE NAMNA YA KUANDIKA NA KUANDAA SCRIPTS
MUUNDO WA HADITH
SEHEMU YA PILI
 2. MUUNDO WA ENEO ZIMA (SCENE) KAMILIFU LA NJAMA
Haijarishi wazo ulilonalo ni zuri kiasi gani kwa ajili ya filamu, lakini kama hauwezi kupata njia ya namna ya kusimulia hilo wazo lako, basi ni kazi bure, atakama wazo ulilonalo linakufurahisha kila ukilifikiria. Ukiwa kama mwandishi wa Script, unatarajiwa kuwa na Mfumo ambao utakusaidia kuwa na uwezo wa kuamisha wazo lako kutoka katika Usingizi wako na kuwa hadithi kamili.
Endelea…!
Jana nilitoa tafsiri ya maana ya njama katika Mtiririko wa somo ngoja nirudie tafsiri yake,
Njama ni nini?

Ni Tukio linalotengeneza hadithi,kawaida huwa ni Mkusanyiko wa mambo yanayohusiana,kwa kiingereza huitwa Plot,ikiwa na maana ni kitu kinachoitaji kitu kingine ili kukamilisha jambo zima, na katika Filamu zipo nyama nyingi ambazo zote ni lazima zihusiane ili kutengeneza hadithi kamili, na nilazima itafutwe kitu ambacho kitaunganisha nyama moja mpaka nyingine ili kuikamilisha Hadithi katika mtiririko,.
Baada ya kupata kuelewa Maana ya Njama, sasa tuendelee...!
Leo, Tutajifunza Mambo Muhimu na ya kuzingatia ili Njama kuwa kamilifu, kwa kuwa njama ni tukio moja linalotegemewa na tukio jingine, ni vyema, ukazingatia Mazingira mazima ambayo yataunganisha Njama moja mpaka nyingine ili kuleta Scene iliyo kamilifu
 Nambo ya Msingi unayotakiwa kuyaweka akilini unapotengeneza Script kwa ajiri ya kuunganisha Movie zima kwanza ni lazima uwe na wazo fupi, ambalo utalitumia kuchota Matukio ndani ya hilo wazo, kama ifuatavyo;

Wazo Fupi
Wazo lako Fupi, ni lazima lielezewe katika sentesi moja au mbili. Mfano wa wazo la filamu: “Nyerere kama Baba wa Taifa”, hili ni wazo fupi na ukilichambua, utakutana na taarifa nyingi sana, na kama Mwandishi wa Script ni lazima uwe na mfumo ambao utakusaidia kuchambua hilo wazo na kuwa katika hadithi, Mfano wa Wazo jingine; “Rose Muhando Malkia wa Muziki wa Injili”, hili nalo ni wazo, lakini je ukilipeleka kwa watu na kulitamka kama lilivyo kwa lengo la kutaka kutengenezwa Filamu, wazo hili litashughuliwa?, Jibu ni “Hapana” kwamaana ndani ya hiyo sentesi kuna mwisho tu, je mwanzo huko wapi, na katikati kukoje?. Ndiyo maana ni Vyema kama Mwandishi wa script kuwa na Mfumo ambao, wazo likija kwako uweze kuligawa katika Vipengere ambavyo Vitakusaidia kutengeneza Hadithi ya keleweka, na Bila wazo hakuna Hadithi, wazo ni kama mbegu ndogo ya Haradani, ikifanyiwa kazi huweza kuzaa simulizi kubwa na Ya kusisimua. Kwahiyo ili usijeku-ishiwa kama Mwandishi ni vyema ukawa na kitabu chako cha kumbu-kumbu ambamo utakuwa ukitunza kila wazo linalokujia. Kila sehemu unayokuwa kama Mwandishi umezingirwa na wazo kwa ajiri ya Filamu, iwe kwenye Dara-dara, uwanja wa Mpira, kijiwe cha kunywea kaawa.n.k.
Mara nyingi unapokwenda kulipeleka wazo lako kwa watengeneza filamu,lazima huwe na maelezo ya kuambatana na hilo wazo, kuna wazo ambalo ukilitamka tu, linainua hisia za watu na kuwafanya watake kujua kuna nini ndani yake.hili ndilo linalo tendeka katika Hollywood, unapopeleka script yako au kuituma ni lazima Mbele ya ganda (Cover), au kurasa ya kwanza ndani ya ganda (Cover), liwe na hilo wazo, sentensi moja au mbili, ili kuwaweka mguu sawa. Na ili kuendelea kuheshimu wazo lako kwa kutoacha kusoma kumbuka kufuata Muundo tuliojifunza jana “MIUNDO MITATU YA UIGIZAJI”

Baada ya Kuwa na wazo fupi, ndani ya Hadithi yako ambayo utaichambua kutoka katika wazo lako fupi, jitahidi, kuingiza mambo yafutayo ili kuwepo Ukamilifu wa Sceneu kutoka wa Njama moja mpaka nyingine;

Simulizi zilizopita (Backstory)
Simulizi zilizopita ni Maisha ya zamani ya Wahusika ambayo yanasaidia hadhira kuelewa namna Wahusika walivyo (wao ni nani haswa) na hadithi yenyewe inahusu nini, hii hufanyika kwa Muhusika kuwaza, Taarifa za namna hii zinatakiwa kuwasilishwa kupitia Tabia ya Wahusika na Mazungumzo. Na pia unaweza kutumia mbinu ya moja kwa moja (Narration) au mbinuo (Flashback), lakini kuna Imani kwa baadhi ya watu kwamba utumiaji wa mbinu hizi unaonesha uandishi wa kivivu, hizo ni Imani tu za watu wachache, lakini katika soko la Uandishi wa script hizi ni za Muhimu sana, kutegemeana na Filamu yenyewe.Utoaji wa taarifa za nyuma kidogo-kidogo katika Filamu ni muhimu sana kuliko kuwasilisha Simulizi zilizopita kiujumla,utoaji wa Jumla unapoteza hamu ya kuangalia Filamu kwasababu, lengo la kutoa kidogo-kidogo, ni ili kumfanya msomaji kutamani kuendelea kutafuta jibu zaidi. Msingi mzuri wa kutoa simulizi zilizopita ni kwa kutoa maisha yaliyopita taratibu, kinyume na hapo script yako itakosa nguvu na itachukuliwa kuwa hafifu.

Utambulisho wa Ukweli uliofichwa (Exposition)
Ukweli uliofichwa , hii ni taarifa ambayo ipo katika hadithi yenyewe ambayo hadhira inaitaji kuifamu kwa ujumla wake na kufichwa kwake ndiyo kusudio la Hadithi, na lengo ni kuifichua taratibu. Kwa mfano katika Filamu ya Jim Carrey itwayo “The Truman Show” ambapo.Jim Carrey kama Muhusika Mkuu anajaribu kuchukua Merikebu (boat) ili atoke nje ya mji lakini hawezi kwasababu ya hofu ya maji, Hofu inakuja kutokana na historia ya Kufa maji kwa baba ye kipndi akiwa Mdogo wakiwa pamoja katika Merikebu, ukipata nafasi ya kuiangalia filamu hii utakuta siri nyingi ambazo taratibu zinaanzakufunguliwa na mwisho kama hadhira unaanza kuelewa kwamba Jim Carrey alikuwa akiishi maisha ambayo si ya Ukweli japo kuwa yeye alidhania ya ukweli, na katika eneo hilo kama mtazamaji unaanza kuchukuliana na Jim Carrey, na kwa pamoja mnaanza kutafuta njia ya kuujua Ukweli. Kwa hiyo kama mwandishi wa script Jaribu kutambulisha huu ukweli kwa utaalamu,kimatendo na pia kupitia migogoro, wakati wa kufichua ukweli huu jaribu sana kutumia Vitendo kuliko maneno “Onyesha,usisimulie”, Hapa napenda niongee kitu kimoja kuhusu Filamu zetu za KIBONGO, huwa tunakosa hii sehemu, kwamaana ukweli sikuzote huwa tunautambulisha kwa maneno kuliko matendo, hii inapoteza utamu wa Movie, Japokuwa zipo baadhi ambazo zinajitahidi kuitumia mbinu hii, Kuna filamu moja ya Kibongo ambayo ninaomba uitafute kwa maana katika eneo hili imefanya Vizuri sana nayo inaitwa “SIMU YA KIFO”

Kima (Pace)
Soma Script yoyote na utaona tendo moja linafafanua umbali wa hadidhi ulivyo, hii huitwa kima (Pace). Kima ni namna ambavyo utamfanya msomaji aone kwamba hadithi bado inaendelea au imewkisha,Chukulia mfano wa zile treni za milimani, zinazo kaa angani kutoka mlima mmoja kwenda mwingie kwa kutumia kitu mfano wa chuma ambacho kimeshikilia ile treni,treni hizi zipo pia huko Urusi zinaitwa kwa kiingereza Roller Coster, Sasa fikiria kwamba inapopanda juu huenda kwa kasi na inaposhuka hupunguza mwendo, Hadithi ipo kama hivyo, ikiwa na maana hadithi ni Treni ya Hisia, Vikwazo vinapozidi kuwa vizito, ndipo scene huwa fupi, hii hali huifanya hadithi yako kuwa na mvuto zaidi kwa maana humfanya msomaji kutokuchoka. Ni kama vile ronaldo yupo na mpira yeye na gori kipa dakika za lala salama, kisha Tanesco wanazima umeme. Kima ni Muhimu kufikiliwa ili kuleta attention kwa wasomaji, usimalize kila kitu kwenye scene moja, bali kila scene utakayoitengeneza iache nafasi kwa scene nyingine. Scene moja inaweza kusema hadithi bado inaendelea au tumekaribia mwisho au Imeisha
.
 Mapumziko/Sehemu ya Marejeo (Turning Points)
Kwakweli Mapumziko au Sehemu ya Marejeo yanaitajika sana katika huandaaji wa Script, kwamaana movie yoyote inasehemu ya Marejeo, ambayo inatoa mwanya kwa hadithi kupanda viwango zaidi, sehemu hii itampa wazo jipya Muhusika au wahusika, na kuwageuza katika Mwelekeo mpya, kila wakati hadithi inapoonekana kumpotezea tumaini Msomaji, ni lazima uingize kitu ambacho kitarejesha tumaini, katika hadithi, tambua kwamba, Muhusika utakaye mjenga, wasomaji watapenda wamtetee au kutamani kumuambia ajiepushe na jambo lililo-mbele yake ambalo msomaji ameliona lakini Muhusika hajaliona, hali hii ikiendelea, inampoteza Msomaji kwa hiyo ni vyema ukatengeneza kitu ambacho kitaleta haueni kwa Mhusika na kwa njia hiyo, unaleta haueni pia kwa Msomaji. Japo kuwa hadithi itakuwa haijaisha ila bado mapambano yanaendelea lakini atapumua kwa Muda kidogo.njia hutumiwa sana katika Maigizo ya Masafa marefu (Tamthiria(TV Serie-Soap)

Vipingamizi
Vipingamizi  ni nguvu za upinzani kutoka  ndani au nje ya Muhusika ambavyo vinampinga Muhusika Mkuu kufikia malengo yake, unaweza kutengeneza kikwazo,kwa mfano, wanamgambo wa jiji wanaokuja kubomoa kibanda cha Muhusika wako ambaye wakati huo ametumia fedha nyingi ili kununua hizo bidha walizo ziharibu, unaweza kumfanya muhusika ajitete lakini kila akijitetea ndiyo makubwa yanazidi. Kwa hiyo Vipingamizi ni muhimu ili kutengeneza kisa kizuri.kinachofuata

Kejeri;
Hapa ni pale,Mwandishi anapo ruhusu Hadhira wafahamu kitu ambacho Muhusika hakijui, kwa mfano, Muhusika anapo tembea na msicha ambaye hadhira inafahamu kuwa ni Mwingi wa habari, japokuwa Muhusika mkuu hafahamu hilo. Na nyumba aliyoipanga wanaume hawaishi, hi ni kejeri.  Na pindi mwanaume anapofahamu inamfanya hajione mjinga hali inatengeneza scene nyingine.

Kilele
Hiki ni kipande kikubwa katika Filamu, ambapo wema unapambana kinyume na uovu, katika eneo hili ndipo hadithi nzima hufunganishwa, Muhusika Mkuu nilazima apambane vita vya mwisho, iwe kimisuli au kihisia.

Utatuzi
Kipande cha mwisho cha Filamu kinaitaji kuonesha kwamba kila kitu kimerudishwa katika utulivu, na aliyekuwa hajiwezi sasa amejiweza, katika sehemu ya mwisho majibu yote ambayo Muhusika alikuwa nayo nilazima yajibiwe, Filamu isijaribu kujibu swali ambalo halikuwepo katika Filamu tangia mwanzo, Kwamfano katika Filamu zetu utakuta mwishoni, Muhusika anapambana na adua kwa kungfu, wakati takingia mwanzo hapakuwa hata na mazingira ya wazi hau ya kuficho ya kuwepo jambo hilo, unakuta katika maisha yake kama Muhusika haijawai kuoneshwa hakiwa na moyo huo wa kujifunza kungfu na wala kungfu haipo sasa unajiuliza hizi kungfu amezitoa wapi, kwa hiyo filamu ni lazima hijibu swali sahihi.chanzo;global publisher na  FREDY SULEIMAN OKUKU
Asante!

Posted by Bongo Film Data Base on 8:29 PM. Filed under , , , , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

2 comments for UANDISHI WA FILAMU NA MAIGIZO

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign