SIFA ZA KIJINGA ZINAVYOWAGHARIMU WASANII


SIFA ZA WASANII ZINAVYOFICHA DONDA LA UMASIKINI LINALOHITAJI TIBA.


Unahitaji kumjua msanii wa filmu Tanzania? Unahitaji kujulikana kuwa na wewe ni msanii Tanzania?? Unataka upate sifa mtaani na jina lako likaririwe katika midomo ya watu!!
Kama jibu ni ndio basi na njia ni nyepesi.
Hakikisha unaandikwa magazetini!!! Hiyo ndiyo siri ambayo ipo wazi.
Utaandikwa kwa mabaya ndiyo usifiwe? HAPANA. Lazima yaandikwe mazuri.
Jawabu hili la kuandikwa mambo mazuri huwalazimisha wasiokuwa na mazuri ya kuandikwa wajibumbie visa vyao vya uongo ilimradi jamii iwatazame mara mbilimbili.
Sio jambo jipya kukutana na maandishi yakimnukuu msanii wa filamu akisema “ Sanaa imeniwezesha kujenga nyumba kijijini kwetu na hapa mjini nina kiwanja”
“Filamu zinaniingizia milioni mia tatu kwa mwaka!!”
“Kwa kawaida kila Scene nacheza kwa laki mbili.”

            Haya ni baadhi tu ya maneno kutoka kwa wasanii wenyewe. Maneno ambayo yana ukweli kwa asilimia kumi tu!!! Wasanii ni waongo na wanauunda uongo kujipatia sifa zisizokuwa na tija.
Sifa hizi zinaifanya jamii kuwachukulia wasanii wote kuwa ni watu wa daraja fulani lisilofikika kirahisi, na wasiohitaji msaada tena.

Wasanii wa filamu Tanzania, wamekuwa wakitukuza sana sifa kuliko maendeleo. Hili ni jambo ambalo linatutofautisha sisi na wenzetu wa Afrika magharibi! Wao wanatanguliza mbele maslahi binafsi katika fani hiyo, kisha sifa hujileta zenyewe bila kutafutwa. Hii hali ni tofauti na Tanzania ambapo msanii kwa pesa yake ananunua sifa za kijinga.
Kuna wakati elimu dunia ndogo waliyonayo wasanii inachangia haya kutokea. Elimu ambayo ingewawezesha kuithamini kesho yao kuliko LEO wanayoipigania kila siku.
Mwisho wa mapigano haya ya kuihangaikia LEO badala ya kuitazama KESHO. Wasanii wengi wakishaupoteza ule umaarufu wa kununua enzi ambazo nyota zao zinang’ara sasa yule ndugu yetu aitwaye umasikini anawaumbua. Licha ya kujificha sana hawawezi kujificha milele. Shida zikiwaumbua ndipo hukiri kuwa sanaa hailipi. Huyo anayekiri hivyo anasahau miaka kadhaa nyuma alijitapa kuwa hakuna muigizaji ana gari la thamani kama la kwake, ama hakuna msanii wa filamu anayemiliki nguo za bei ghali kama yeye. Sasa analia tena!!! Donda linakuwa komavu na sasa halina tabibu!! Lazima liendelee kuchimbika mwishowe anakufa maskini na tunabaki na neno moja tu. Alikuwa muigizaji mzuri sana!!
Neno hilo lina maana gani kwa marehemu???

LAITI KAMA: Wasanii wangetambua kuwa maisha ya msanii ni kujifunza kila siku ili uwe bora. Basi wangejifunza kwa wenzao ambao walizichezea nafasi mwishowe donda likawaumbua lilipokomaa.
LAKINI wasanii wa jana na wale wa leo, afadhali wa JANA walikuwa na kisingizio kuwa sanaa ilikuwa burudani pekee. Wa sasa atasingizia nini iwapo sanaa ya sasa ni KAZI??
Posted by George Iron on 9:25 AM. Filed under , , , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for SIFA ZA KIJINGA ZINAVYOWAGHARIMU WASANII

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign