
Monalisa mmoja wa wasanii wakubwa wa filamu Swahiliwood.
WAKATI Bajeti ya Wizara ya Fedha ikisomwa na Waziri Dkt. William A.
Mgimwa Bungeni iligusia kuhusu kazi za Wasanii tena ikionyesha kutambua
jinsi gani wasanii na wadau wote wanaofanya kazi halali wanavyoibiwa
kazi zao na kubaki maskini huku watu wengine wakifaidika na jasho la
wasanii hao, binafsi naungana na mwandishi wa makala haya Ignas Mkindi
KWA HABARI NA PICHA ZAIDI INGIA NDANI…..

Monalisa akiwa na tuzo yake aliyoshinda katika tamasha la ZIFF mwaka 2010.
Mara nyingi kumekuwa kukitolewa takwimu fulani kuhusu kundi husika
bila utafiti, leo sisi tunapenda kuongelea tasania ya filamu Swahiliwood
ambayo si rasmi huku taasisi zinazohusika na tasnia hiyo zikiwa makini
tu kuhakikisha zinavuna fedha bila kutengeneza mazingira ya kufaidisha
upande unaozalisha kazi hiyo.
Kwa mfano hivi sasa tasnia ya filamu inajikuta inakabwa katika taasisi
tatu ambazo ni Bodi ya Ukaguzi wa filamu ambayo ipo kisheria, kuna
COSOTA ambayo ni tatizo kubwa kwa wasanii, kuna hawa BASATA nao eti
wanahusika na filamu, tatizo la taasisi hizi ni pale yanapotekea
matatizo maamuzi yao yanatia shaka, hivi kweli mwizi wa kazi za wasanii
hajulikani?
Ignas Mkindi ni mkubwa mdau wa filamu kutokana na kuwemo katika
tasnia kwa zaidi ya miaka kumi kama Mwongozaji (Director), Mwandika
mswada (scriptwriter), Mtayarishaji (Producer) na Mkuu wa sakafu
(Production Manager) katika filamu zaidi ya ishirini na tano zikiwemo
AUGUA (2001), FIKIRI (2004), SANDA NYEUSI(2008), BESTMAN (2009), WRONG
DECISION (2010), ASALI CHACHU (2010) na DIANA (2012).
Pia ni mwanaharakati katika maendeleo ya tasnia ya filamu kwa muda
wote huo zikiwemo harakati za kutoa mafunzo kwa waigizaji DDC Magomeni
Kondoa (2000 – 2004), Mafunzo ya uandishi wa miswada katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (2007) na harakati za mchakato wa marekebisho ya
sheria ya filamu na uanzishwaji wa shirikisho la filamu kupitia Bodi ya
Ukaguzi wa Filamu (2009).
Usimamizi wa tasnia ya filamu
Hadi muda huu sheria inayosimamia tasnia ya filamu ni Sheria ya Filamu
na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 1976 (namba 4) iliyosainiwa na Rais wa
kwanza wa Jamhuri ya Muungano Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambayo
iliunda Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza.
Hata ilipoundwa sheria namba 23 ya mwaka 1984 iliyoanzisha BARAZA LA
SANAA LA TAIFA (BASATA) kwa kuunganisha Baraza la Sanaa la Taifa na
Baraza la Muziki la Taifa na kuitambua Sheria ya Baraza la Sanaa la
Taifa ya mwaka 1974, haikuifuta sheria ya filamu na michezo ya kuigiza
ya 1976 wala haikuwa na lengo la kuipa BASATA nguvu ya kusimamia filamu
kama wanavyojaribu kufanya hivi sasa.
Pamoja na tafsiri nyingine za kazi za sanaa katika sheria iliyounda
Basata kipengele cha 2(a)(iv), kazi ya sanaa inayosimamiwa na BASATA
imetafsiriwa kama ‘Picha ambazo hazikutengenezwa kwenye mashine ya picha
za filamu’
Filamu ni zaidi ya sanaa, ni suala mtambuka ambalo linahusisha
taaluma nyingi, na waigizaji ambao ni wasanii ni sehemu ndogo tu ya
tasnia ya filamu ila huwa wanaonekana kuwa na nguvu sana kwa kuwa ndiyo
wanaoonekana. Wasanii wengine katika tasnia ya filamu ni wabunifu wa
mavazi, warembaji na wapambaji wa sehemu za kuchukulia picha.
Kwa kuwa wakati inatengenezwa sheria hiyo ya Filamu na Michezo ya
kuigiza ya mwaka 1976 hakukuwa na televisheni, wasambazaji wala maduka
ya kukodisha mikanda ya video, sheria hiyo imejikita zaidi katika
utengenezaji wa filamu na maonyesho ya filamu hadharani (kwenye majumba
ya sinema).
Kwa juhudi za Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na dhamira aliyokuwa nayo
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo kwa wakati huo, Mheshimiwa
Kapteni Mstaafu George Mkuchika, wizara ikaanzisha mchakato wa
marekebisho ya sheria hiyo iliyopitwa na wakati ili iwe SHERIA YA
MAMLAKA YA FILAMU.
.

Waziri wa Fedha Dkt. William A. Mgimwa akiingia Bungeni kusoma hotuba ya Bajeti 2012/2013

Mwenyekiti wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza, Rose Sayore alipigania kuanzishwa kwa shirikisho la Filamu.
zoezi hilo lilisimamiwa vema na Mama Rose Sayore akishirikiana na
katibu wa Bodi ya Ukaguzi wa filamu kwa wakati ule Lily Beleko,
mwanasheria wa Wizara Patrick Kipangula pamoja na wafanyakazi wa Bodi
tena wakisisitiza kwa wasanii wawaite wasanii wengine kwa ajili ya
mchakato huo.
Huo ndiyo ulikuwa ufumbuzi wa kweli wa matatizo katika tasnia ya filamu.
Nini kilitokea?
Sisi kama wadau tuliitwa mwezi Mei, 2009 kujadili marekebisho ya sheria
hiyo kwa siku mbili na kutoa mapendekezo yetu. Hatua iliyofuatia ilikuwa
iwe ni majadiliano ya wadau wa ndani ya serikali kisha ipelekwe katika
baraza la mawaziri kabla ya kupelekwa bungeni.
.

Mh. Capt. Mstaafu George Huruma Mkuchika aliyeanzisha harakati kuhusu chombo kitakachotambua wasanii wa filamu Tanzania.
Pia siku ya tatu tulifanya uchaguzi wa kamati ya wadau kuangalia
namna ya mchakato wa kuunda Shirikisho la Filamu Tanzania (SHIFITA)
kauli mbiu ikitwa ‘Swahiliwood’ ili liweze kuwaunganisha wadau wa filamu
kusukuma upatikanaji wa sheria hiyo.
Sitazungumzia mvurugano uliotokea kati ya BASATA, Bodi ya Ukaguzi wa
Filamu na Michezo ya Kuigiza pamoja na wasanii wa filamu kuhusu mchakato
wa uanzishwaji wa shirikisho kwa kuwa siyo muhimu kwa sasa kutokana na
ukweli kuwa tayari kuna Shirikisho la Filamu Tanzania.
Siku ya siku kwa kuwatumia wasanii hao hao ambao hata hawakuwa na muda
wa kuangalia sheria ya awali ilikuwa inampa nani mamlaka ya kusimamia
filamu kisheria waliingia mkenge na hatimaye shirikisho liliundwa chini
ya BASATA, lakini katika jambo la ajabu kushinda yote BASATA hao hao
wameshindwa kumaliza mgogoro unaoendelea kati ya Shirikisho hilo TAFF na
Bongo Movie Clubhiyo siyo siri tena ugomvi upo tena mkubwa.
Ila kikubwa ninachokiona ni kuwa, kuna baadhi ya watendaji wa
serikali wananufaika na mvurugano wa kisheria uliopo katika usimamizi wa
tasnia ya filamu ndiyo maana wanakwamisha marekebisho ya sheria ya
filamu na kuishauri serikali mambo ambayo hayawasaidii asilimia kubwa ya
wadau wa filamu.
Waathirika ni kina nani?
Wasanii mastaa siyo waathirika sana wa hali iliyopo kwa maana huwa
hawaigizi mpaka walipwe fedha wanazotaka, na hata wakiandaa filamu,
wengi wao wanakuwa washauza haki miliki kwa wasambazaji ila wao ndiyo
wanapata fursa ya kusikilizwa sana na viongozi wa juu wa serikali kwa
kuwa ndiyo wanaoonekana sana kwenye vioo (screen). Siyo vibaya kutokana
na uelewa wa viongozi wa juu kuhusu filamu ila je, wataalamu wa filamu
walioajiriwa na serikali wanafanya nini?
Waathirika wakubwa ni watayarishaji waliowafanya hawa mastaa wawepo
kisha wakawekwa pembeni na mfumo wa wasambazaji kuwapa fedha moja kwa
moja waigizaji wawatengenezee filamu ambazo wamiliki wanakuwa
wasambazaji. Siwalaumu wasambazaji kwa sababu wanafanya biashara
kutafuta faida, lawama ni kwa watendaji wa serikali ambao wanawafumba
macho wasanii wasioelewa kuwa maadui zao ni wasambazaji kumbe wao ndiyo
maadui.
Ukitaka kuuthibitisha ukweli huu kaangalie COSOTA kama kuna zaidi ya
asilimia kumi za filamu za mastaa zinazomilikiwa na waliozitengeneza au
ongea na watayarishaji wakongwe kama Amri Bawji wa Tanga, Sultani Tamba
na Jimmy Mponda (Jimmy Master).
Waathirika wengine ni maelfu ya wasanii wachanga wanaohangaika kutoka
na kuigizishwa kwa malipo kidogo katika filamu hizo za wasambazaji
zinazotengenezwa na wasanii mastaa.
.

Gonche Materego katibu Mtendaji wa BASATA.

Rais wa TAFF Simon Mwakifwamba.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Serikali ya Tanzania Mh. Dr. Jakaya Mrisho
Kikwete akiwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Club Jacob Stephen(JB) katika
picha ya pamoja Dodoma.

Hwa
ni wasanii wachanga wasiojua hatimaya yao kuhusu tasnia ya filamu
ambayo kwao ilikuwa ni ajira mbadala baada ya kukosa ajira zingine.

Wadau
na Wasanii kama JB, Thea, Mama abdul , Dude, David Jr., Mboto
walioudhuria mchakato kwa ajili ya uanzishwaji wa SHIFITA Uwanja wa
Taifa 2009.
Hitimisho
Tunaishauri Serikali na watendaji wao kufanya utafiti wa kina kwa kuwa
na wadau wenye uzoefu na uelewa wa tasnia hiyo kwa undani kuliko
kuwatumia wasanii kwa muonekano wao katika filamu wakaamini kuwa
wanaweza kupata taarifa sahihi kuhusu mustakabali wa tasnia ya filamu na
maslahi kwa wahusika.
Ulimwenguni kote wizi wa kazi za wasanii upo lakini unamalizwa na
mfumo makini na thabiti kupitia vyombo husika vinavyolinda haki za
wamiliki wa halali wa kazi hizo si kama ilivyo kwa COSOTA na BASATA
inapotokea wizi kusimama kwa aliye nacho, hali ambayo ujenga chuki na
watu kukosa imani na taasisi husika.
Sehemu kama Hollywood filamu haiingii sokoni kwa kuuzwa Dvd! Lazima
kazi hiyo ionyeshwe katika majumba ya Sinema na Dvd au kitu chochote
utolewa kwa maagizo maalumu ya kibiashara, hapa kwetu hatuna wasambazaji
wa filamu bali kuna wanunuzi wa haki za wasanii na watayarishaji jambo
ambalo Serikali wanatakiwa kuliona.
Leo hali ya ngoma za asili ipoje hapa nchini? Na msimamizi wa
utamaduni ni nani? Tunakimbilia filamu tutaiweza wakati kama taasisi
imeshindwa kusimamia utamaduni ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa ngoma
za asili na utamaduni unalindwa kwa gharama yoyote, hivi sasa matangazo
mengi yanatumia muziki kutoka nje hawa wasanii mnaotaka kodi yao
wanaipataje hiyo fedha? BASATA mpo kweli?
Kutokana na hali hiyo nadhani mtakubaliana nasi kuwa SERIKALI
KUANZISHA STEMPU NI NJIA YA KUJIONGEZEA MAPATO YENYEWE NA SIO KUWASADIA
WASANII.
CHANZO; FILAMU CENTRAL
ASANTE!