VIOJA VYA MREMBO WA FACEBOOK IPO TAYARI
mpya, mtandao, slide, udaku 10:23 PM
MREMBO WA FACEBOOK filamu iliyotungwa mahususi kabisa kuwaelimish kwa watumiaji mitandao ya kijamii kama facebook na twitter ,ndani ya filamu hii yamezungumzwa mengi ila kubwa ni yale madhara ya facebook na namna yalivyowakuta watu wengi ambao wanatumia ukurasa huu.
Mkasa mkuu ni huu wa watu kutoweka picha zao halisi kwenye profile picture kama sio album yake yote na kuweka picha za watu wengine zilizokuwa na mvuto na mwonekano mzuri zaidi, kitu hiki kimewaghalimu watumiaji wengi wa mtandao huu wa kijamii [facebook] kwa kila mtu kwa namna yake kulingana na nyakati na mazingira ya mtuaji aingiavyo mkenge wa kudanganywa na hatimaye kutapeliwa fedha, mapenzi, n.k
Filamu hii imeandaliwa kwenye mahadhi ya vichekesho[comedy] na ilimeghalimu laki sita tu mpaka kukamilika kwake na ilirekodiwa kwa siku moja tu.na huyo hapo juu ndiye mrembo mwenyewe wa facebook.
STAR CAST;
SENGA,
PEMBE,
DIFENDA,
DANNY
SAMOFI,
FETTY
STORY
GODLOVE ANTHON
DIRECTOR
GODLOVE ANTHON
PRODUCER
SAMOPHI PRODUCER/EX PRODUCER