TRA NA SHIRIKISHO LA FILAMU VYAAPA ADHALANI
habari, mpya, slide, udaku 10:31 PM
Shirikisho la Filamu nchini(TAFF) kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) pamoja Kampuni za usambazaji wa
filamu na kazi za wasanii ‘zimeapa’ kupambana na maharamia wote wa kazi hizo
ili kulinda maslahi ya wasanii.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar
es salaam jana, umoja huo kwa pamoja ulisema umefika wakati tatizo la wizi wa
kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya yote ambayo ni kero
kwa muda mrefu.
Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati
hiyo pia aliiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa
kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii huku
wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.
“Umefika wakati kwa Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii
na kuweka mbinu kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa
masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi zao”
“Tuna imani kuwa kama kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri,
tutaweza kuongeza pato la Taifa kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa sanaa hii
kwa sasa hapa nchini imeonyesha mafanikio isipokuwa kuna watu wachache ndiyo
wananufaika nayo” alisema Mwakifwamba.
Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa
inaweza kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato
linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja na utalii.
Alisema Serikali inapswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata
wahusika wote wa wizi wa kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa
nchini walioamua kujitoa mughanga kufanya kazi zao.
Kwa upande wake Meneja usimamizi kutoka TRA Msafiri Ndimbo
alisema Mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari
Mwakani hasa baada ya Serikali kupitia Bunge lake kukubalina kuweka mikakati ya
kupamba na suala hilo.
Ambapo wasanii na wasambazaji wa kazi zao wameungana pamoja
kwa ajili ya kuhakikisha kazi zao zinakwebnda kwa haki ili wasanii wapate na
wao wawe ni watu wa kusaidi wasanii kusambaza kazi zao
Na mdau wetu; markus Mpangala