ARNOLD MZIGONI TENA NDANI YA THE LAST STAND
habari, kinyemi, mpya, slide 10:14 AM
kama unavyofahamu Mwigizaji ni mtu mmoja ya watu muhimu sana kwani wao ndiyo huibeba filamu aichezapo vizuri kwa ushirikiano wa karibu zaidi na jopo zima la utengenezaji wakiwemo waongozaji, wapigaji picha watunzi na waandishi miswada.
Katika ulimwengu wa uundaji filamu duniani huwezi kuacha kutaja watu kadhaa waliyochangi kwa kiasi kikubwa sana kukua kwa tasnia hii tangu enzi hizo yaani itakuwa ni ngumu sana kwa wapenzi wa filamu za kivita waliyokuwa wakifuatilia filamu za namna hiyo kwenye miaka ya tisini kuacha kumtaja kamanda Arnold Schwarzenegger.
sasa kamanda huyu anakuja tena na filamu nyingine inayokwenda kwa jina la THE LAST STAND ila Je! filamu hii huenda ikawa ndiyo filamu yake ya mwisho kuigiza katika maisha yake kama ilivyo batizwa kwa jina lake la THE LAST STAND?
Mwongozaji na mwandishi filamu toka korea ya kusini bwana Kim Jee Woon mwenye filamu taklibani kumi na tisa [19] tangu mwaka 1998 mpaka sasa. Kim na jopo lake wapo kwenye matayarisho ya utengenezaji filamu yake nyingine mpya aliyomshirikisha mmoja ya viongozi wa kubwa na maarufu sana nchini marekani Mh. Arnold Schwarzenegger. filamu hiyo inayokwenda kwa jina la THE LAST STAND inatarajiwa kuwa mtaani tarehe 18 mwezi wa kwanza mwaka 2013.
Peter Stomare.
Mwigizaji na mtayarisha filamu ambaye alitumia jina la Burrell kwenye filamu ya The Last Stand
Rodrigo Santoro[Frank Martinez]
moja ya waigizaji wenye kipaji kikubwa nchini Brazil aliyeng'ara kwenye jukwaa la filamu mwaka jana ambaye anatumia jina la Frank Martinez
Zach Gilford
Jina alilotumia ni Jerry Bailey
[Jerry Bailey]
Jaimie Alexander
Jina alilotumia kwenye filamu hii ni Saraha Torrance
Na hii hapa chini ndiyo resume ya director Kim Jee Woon tangu aanze kujishughulisha na mambo ya utayarishaji filamu mpaka sasa.
DIRECTORS
Kim Jee-Woon | Director |
CAST
Arnold Schwarzenegger | Ray Owens |
Peter Stormare | Burrell |
Rodrigo Santoro | Frank Martinez |
Zach Gilford | Jerry Bailey |
Jaimie Alexander | Sarah Torrance |
Eduardo Noriega | Gabriel Cortez |