KIMORA THE LONDON GIRL(facebook) preview .1


KIMORA THE LONDON GIRL(facebook)
Hongera kwa kava kuwa poa kwa yule aliyetia mkono kwenye kulifanikisha hilo...japo wizi bado upo pale pale, we Geofrey ndo nini kutupiga changa la macho kwenye kava namna hii? Muhusika mkuu nambari mbili baada ya kimora kutoonekana hata kwenye kava hata moja? Nakumweka muhusika kivuri Benny kinyaiya...niachane na hilo kava kwanza na niingie ndani 

MAUDHUI; maudhui mazima kwa yale ulikusudia kutuonesha kaka, hongera kwa ujasiri wakuthubu kufanya filamu katika nchi ya ugenini kwanza...lakini braza mpaka namaliza tizama kazi yako sikupata funzo lolote kwani mafunzo huja na utufikia sisi watizamaji kwa kuoneshwa maonyo ama madhara na hatimaye fundisho la namna gani mtu afanyapo jambo ambalo si sawa katika jamii hupata madhara na kutuonesha majuto na njia mbadala kuepuka hili...na hatimaye hadithi yako ilibaki hewani tu bila kuona hatima yake..

LOCATION; location ulipata nzuri za kufanyia kazi yako japo hukuzitendea haki kwa makosa yakiufundi na wepesi wa hadithi yako kutokana na ugeni wako ama crew nzima kwa ujumla katika fani hii..

MAVAZi na MAKEUP; Kaka ilikuwa ni suala la ajabu sana kuona mwendelezo wa matukio ulikuwa ni mbovu sana katika kazi yako..ndani namwona KIMORA katika scene hii hapa halafu ndani ya mwenendo wa scene hiyo hiyo kimora anaonekana tofauti kuanzia nywele mpaka mwonekanö wa sura yaani makeup ya awali tofauti ya sasa..na bwana Deziel naye mwendelezo wa matukio unatofautiana sana, mara D anaonekana ana nywele na ndevu ndefu mara amezipunguza yaani alikuwa ananichanganya sana...Makeup na mavazi kaka ulichemka...

SCRIPT; kwa ujumla kwenye script kaka alichemka kwani maneno yanajirudia sana yaani sijui hapakuwa na mfuatiaji mzuri katika editing..

SOUND; sound ilikuwa mbaya sana kwani palikuwa na voice over nyingi sana tena ni ambazo hazikutakiwa kusikika kabisa mfano sauti ya director anaelekeza wasanii haikutakiwa kusikika kabisa na nikosa moja kubwa linapelekea kazi ya huyu bwana izuiliwe kuingia sokoni na chama husika...kiukweli mie sikuelewa kabisa mwanzo mwisho ama ilikuwa ni kwa cd nilizotizama mie tu,basi mdau mwenzangu tafuta filamu hii ujione nawe..

WADAU KUNA MAMBO MENGI YALIYO KUWA HIVYO SANA KWENYE FILAMU HII YA KIMORA THE LONDON GIRL (facebook) ila kwa leo inatosha mpaka tena siku nyinge na kitu kipya kwenye fani.

Kutoka ubunifu,guder Am out!

Posted by Bongo Film Data Base on 7:46 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for KIMORA THE LONDON GIRL(facebook) preview .1

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign