JINSI YA KUANDIKA MISWADA (SCRIPT) YA FILAMU

Unapoandika mswada[script] kuna vitu vitatu vya msingi kuzingatia:
• Muhusika (character)
• Muundo (plot)
• Dhamira (theme)

1. TUKIMZUNGUMZIE MUHUSIKA KWANZA
Mswada wa filamu una sehemu kuu nne ambazo kila mwandishi lazima azipitie ili mswada wake uwe nzuri, kwanza kabisa ni hadithi yenyewe kwa ujumla yaani lazima iwe na wazo [idea] kamili kwenye kila mstari mmoja inayoonyesha nani ni muhusika mkuu na nini malengo yake ambayo katika hadithi [story] yako amepanga kuyafikia,kwa mfano unaweza kuwa na hadithi[story concept] kuwa Lucy ni msichana mwenye miaka 21 na malengo yake ni kuja kuwa mwanasheria ili aweze kumsaidia baba yake ambaye yupo gerezani miaka kumi sasa kwa kesi ya kusingiziwa na hadi sasa bado hajahukumiwa.huyu ni muhusika mkuu wa filamu yako sasa ili aje afikie malengo yake kuna vikwazo vingi sana anavyopitia.
Wahusika pia ni hatua [stage] nyingine katika kuandika mswada[script], hawa ni watu wanaosaidia hadithi kufikia pale mwandishi anapotaka ifike,yaani wanaijaza hadithi [story] na kuwa yenye mvuto.
Wahusika katika filamu wanahitaji, moja ni vitendo, pili ni malengo tatu wanahitaji muelekeo, hii ina maana kuwa ni lazima kuwe na sababu ya kwa nini huyu mhusika anafanya au kufanyiwa jambo fulani,kwa mfano katika malengo pale mhusika anapokwama na kuendelea kuhangaika inasaidia mtazamaji naye kuhusika katika filamu na inafikia kipindi mtazamaji sasa anatamani aingie akamsaidie kwenye hiyo hadithi [story] yako. unapomshirikisha mtazamaji katika namna moja au nyingine anafurahia sana filamu hiyo na kuona kama inamgusa kabisa.
Na ili mhusika mkuu aweze kucheza nafasi yake vizuri ni lazima awe na wahusika wengine watakao msaidia au kumpinga yeye.[Antagonistic]



MUUNDO
Muundo wa hadithi [story] yenyewe pia ni suala la msingi sana la kuzingatia hapa ,muundo wa hadithi ndiyo unaoonyesha matukio na uhusiano baina ya wahusika na nini kinachotokea kwenye hadirhi [stori] na vile vile inaonyesha nini kinatokea kwenye hadithi hiyo.
Mtindo wa maneno na vitendo ulivyopangwa hupangwa vizuri ili kuongeza matukio katika hadithi.
Muundo kwa kawaida uwa umegawanyika katika sehemu tatu yaani mwanzo,kati na mwisho.inategemea na mwandishi mwenyewe ameamuaje kuna hadithi zinazoanzia mwisho kwenda mwanzo kama wenzetu wahindi wafanyavyo katika kiwanda chao walicho kiita[ BOLLYWOOD] au pengine huanza kati, mwanzo alafu mwisho au wakati mwingine kwa muundo wa moja kwa moja yaani mwanzo hadi mwisho.na vile vile matendo yanaweza kuelezea hadithi au muhusika anaelezea hadithi hiyo kama inavyokuwa kwenye riwaya.
Mara zote unapoandika hadithi yako ni lazima uanze na swali ‘’itakuwaje’’ (what if) na kila filamu huwa inafuraha na huzuni.
DHAMIRA
Kabla ya kuanza kuandika mswada[script] kuna maswali unayotakiwa kujiuliza na kutoa majibu yake ili pale unapoandika uwe na mtiririko mzuri wenye kuvutia kwa kila atakayesoma hadithi au tizama filamu yako,mfano wa maswali yaliyo ya wazi kabisa ni kama yafuatayo;
• Muhusika mkuu wako ni yupi [who is your main character?]
[What is he/she trying to accomplish?]
• Kuna vizuizi gani anavyopata kutoka kwa muhusika mwingine? ( who is trying to stop her/him )
• Kitatokea nini endapo atashindwa kufikia malengo yake? (What happens if she/he fails?)
• Scene inaanzia wapi na scene itaishia wapi? [Where do I start the scene and end the scene?]
• Je kuna uhusiano wowote kati ya tukio [scene] moja na nyingine? [Is there any relationshinship between one scene and another?]
• Je matukio [scene] yako yame pooza [flat] na kujirudia rudia,na kutokuwa na mvuto?
• Na je!mtazamaji atafurahia kuangalia filamu?
Hayo ni maswali ya msingi sana na kama mwandishi akiyazingatia mwisho wa siku ataandika mswada [script] mzuri na kila mtu atavutiwa nao.

Vile vile katika uandishi wa mswada [script] ubunifu ni kitu cha msingi sana cha kuzingatia, na ubunifu huo unapaswa uendane na mlolongo wa hadithi yako na kukumbuka hasa nini uweke kwenye hadithi yako na nini usiweke kwenye mswada huo .
Mbali na hayo pia unapoandika mswada [script] jambo la msingi katika hadithi ni mgogano (conflict)
Unapoandika msawda [script] wako mfano kuhusu kijana anayetaka kuwa dokta hivyo anamuomba baba yake amsaidie fedha zitakazo msaidia katika masomo yake na anamatarajio makubwa sana ya kupata msaada kutoka kwa baba yake matokeo yake baba anamkatalia na kumwambia fedha aliyonayo ni ya kumsomesha uhasibu ili aje asimamie miradi ya familia hapo tayari kunatokea mgongano baina ya baba na mtoto,hivyo basi unashauriwa kuonyesha mgongano mapema iwezekanavyo,kama nilivyosema mwanzo,mgongano ndiyo unabeba hadithi,usipoweka mgongano hadithi haiwezi kuvutia,kama nilivyoonyesha huo mfano hapo juu endapo baba angempa ada na kusoma akamaliza na kuwa daktari hakuna kitu ambacho kingeweza kumvutia mtazamaji.Hivyo hakikisha mgogoro unakuwa mkubwa kabla ya kufikia kwenye suluhisho.kwa kutumia mfano wa juu huyu kijana anasimamia msimamo wake na baba nae anasisitiza mwanae asome uhasibu ,mwisho baba anamfukuza mtoto wake nyumbani ,anaondoka na kuanza kuishi maisha ya kutanga tanga ambayo ni bora angekubali matakwa ya baba yake.
Ni vizuri sana mgogoro ukipata ufumbuzi ambapo ndiyo hatua ya mwisho kabisa ya hadithi na katika mfano wetu huo huo kijana anaondoka na kwenda mbali akiwa kule maisha yanambana sana na kuamua kurudi nyumbani kuongea na baba yake kuwa yupo tayari kwenda kusoma uhasibu lakini akiwa na nia akipewa tu ada anaenda kusoma udaktari anafika nyumbani na kuongea na baba yake anayemsamehe na kuahidi kumpa ada lakini kwa bahati mbaya siku inayofuatia baba anadondoka bafuni na kupoteza maisha,linakua pigo jingine kwa kijana hivyo anashindwa kwenda kusoma kwa muda huo inabidi asimamie miradi ya baba yake na baada ya miaka mitatu mbele anafanikiwa na kwenda kusoma udaktari.
Huu ni mfano mmoja wapo wa mgogoro ingawa kuna migogoro mingine ambayo inaweza kuwa wa nafsi (internal conflict),mtu na mtu kama huu wa baba na mtoto,ipo mingine ya kijamii na mtu na jamii.
Hadi kufikia mwisho hadithi au mswada[script] inatakiwa kuwa katika mfumo huu kama mchoro unavyoonyesha.



1.MWANZO[START]



2.MIGOGORO[CONFLICT]


3.SHULUHISHO[RESOLUTION]




BEGINNING/MWANZO END/MWISHO



Na vile vile kuna software nyingi zinazoweza kusaidia katika kuandika script mfano final cut,celtix na nyingine nyingi.







Kwa kawaida unapoanza kuandika mswada [script] wako kwa mara ya kwanza unapomtambulisha mhusika ni lazima uandike kwa herufi kubwa jina lake na ikiwezekana weka na umri wake.
Kwa kuzingatia kanuni za uandishi unatakiwa kuanza na kuandika namna tukio litaanza [transition] ambayo inafaa na mara nyingi unatakiwa kuanza na FADE IN ambayo inaandikwa kulia kwa ukurasa.
Pia ni lazima kuanza na kuonyesha eneo kama ni nje au Ndani ambayo inaandikwa kwa kifupi. INT/EXT na kufuatiwa na nukta kisha andika sehemu gani kama ni sebuleni,chumbani kwa kufuatiwa na muda,hapa kwenye muda unaandika kama ni mchana au usiku.na lazima iandikwe kwa herufi kubwa na kuanzia mwanzo wa ukurasa wako.
Usiandike aina za shots zitakazotumika ili director aweze kuweka mawazo yake au ujuzi wake inaweza kuwa shot uliyoandika hapo yeye haipendi.


Mfano;


FADE IN


1 INT. JAVED'S SAFE-HOUSE. BATHROOM. NIGHT.

An expensive bathroom suite. Excess of marble and gold taps. Into the bath, a hand is scattering rupee notes.
Hundreds and hundreds of notes, worth hundreds of thousands of rupees. The sound of a fist thumping on the bathroom door, furious shouting from the other side.

JAVED O/S
Salim! Salim!


2 INT. STUDIO. BACKSTAGE. DAY.

Darkness. Then, glimpses of faces. In the half-light,shadowy figures move with purpose.
An implacable voice announces.

TALKBACK V/O
Ten to white-out, nine, eight,
seven...

PREM
Are you ready?

Silence,A handshakes a shoulder a little too roughly.

PREM (CONT'D)
I said are you ready?

JAMAL
Yes…


3 INT. JAVED'S SAFE-HOUSE. BATHROOM. NIGHT.

The thumping at the door continues.
The sound of mumbled Indian prayer.
Dull gleam of a pistol.
A hand cracks the chamber open. Loads a single bullet into the chamber, snaps the chamber shut.

TALKBACK V/O
...three, two, one, zero. CuePrem,
cue applause...

Suddenly, the door splinters as it is smashed through.A burst of gun-fire and white light as suddenly...


4 INT. STUDIO. NIGHT.

...we are back in the studio, the gun-fire morphing Into rapturous applause.

Kuna vipupisho vya muhimu sana vinavyotumiwa kwenye miswada [script] kama vile:
• CONT'D-ikiwa na maana ya continue
• V/O-Voice over
• O/S-Off screen
• Int. inamaanisha interior ( Ndani)
• Ext-Exterior ( nje)
• MOS-Kimya

ALRIGHT STUDENTIIIIIIIII NASIKIA KENGELE INAGONGA SASA. MPAKA SIKU NYINGINE TENA, NI MIMI KIRAJA WENU KUU WA DARASA LA LEO. na KAMA UTAKUWA NA MASWALI KWA SOMO LA LEO USISITE KUNIANDIKIA KWENYE EMAIL YETU (bongofilm@hotmail.com) AU YAACHE HAPO CHINI KWENYE COMMENTS BOX YETU NA WENGINE WAPATE KUYAONA PIA NA MAJIBU YATATOKA KABLA YA DARASA LIJALO...

shukrani nyingi zimwendee dada Tina...

Posted by Bongo Film Data Base on 9:34 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

1 comments for JINSI YA KUANDIKA MISWADA (SCRIPT) YA FILAMU

  1. Excellent blog you have here but I was curious if you knew of any user
    discussion forums that cover the same topics talked about
    here? I'd really like to be a part of group where I can get feed-back from other experienced people that share the same interest. If you have any suggestions, please let me know. Thank you!

    Here is my homepage krankenkassen vergleichsrechner

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign