RAY; KUUZA SURA NA DOLA 2,500 HANILIPI KUCHEZA MATANGAZO YA KIBIASHARA HAPA BONGO

Nyota katika tasnia ya filamu Bongo Vincent Kigosi ‘Ray’ amesema kuwa matangazo ya biashara hayalipi, ndio maana hashiriki katika kutengeneza matangazo hayo kwa sababu hayana faida kwake, anaendelea kusema kuwa mara nyingi inawalazimu kuwatumia watu wa kawaida au warembo na waigizaji nyota kama yeye kwa sababu malipo yao huwa madogo.
“Siyo kama sipati matangazo ya biashara kwa ajili ya kutangaza bidhaa zao, fedha wanayotoa ni ndogo sana kiasi cha kukatisha tamaa, siwezi kutumika katika matangazo kwa pesa ndogo wakati nikitengeneza filamu napata fedha zaidi ya hiyo, kwa wale wanaopenda sifa za kuonekana bila faida waache wafanye, lakini mimi msimamo wangu upo kimaslahi zaidi,” anasema Ray.
Aidha msanii huyu anasema kuwa tatizo la matangazo hayo pamoja na kuwa malipo ni kidogo lakini hayana ukomo wa muda maalum, mwenye bidhaa husika ana uwezo wa kulitumia tangazo hata milele bila kuendelea na malipo mengine.
Vincent Kigosi

“Mara nyingi baadhi ya makampuni yananifuata lakini kila linapofika suala la malipo na ukomo wa tangazo wanakimbia, kuna tangazo ilitakiwa nilifanye mimi lakini baada kuambiwa kuwa nitalipwa dola 2,500 na kutumika milele bila malipo ya kila muda nilikataa na kuna mtu akalifanya, kama kuonekana naonekana sana katika filamu zangu sina sababu ya kuonekana kwa malipo mbuzi,”
Msanii anasema kama kuna kampuni ambayo inataka kufanya naye kazi atafanya nayo tu, iwapo itatimiza masharti yake kwa kuwa na mkataba unaeleweka na si wa kuuza sura, pia anaamini kuwa katika bidhaa wakitumika wasanii nyota bidhaa hiyo itafika mbali kimasoko.
HABARI NA PICHA KUTOKA FILAMU CENTRAL...Asante!

Posted by Bongo Film Data Base on 1:03 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

3 comments for RAY; KUUZA SURA NA DOLA 2,500 HANILIPI KUCHEZA MATANGAZO YA KIBIASHARA HAPA BONGO

  1. sasa kama ni hivyo mbona Steps ananunua filamu za kwa mkataba wa milele ambapo watoto wao watakuja kuangalia macover ya filamu walizo igiza wao bila kuona faida zake.. yeye aseme ukweli tu anamuonea donge kanumba kapiga pesa ndefu na Star times hahahahaha

  2. wasambazaji wananunua filamu zao kwa mikataba ya milele na hawana haki yoyote wa malipo ya baadae katika filamu zao sasa anashangaa nini katika matangazo ya biashara?

  3. wadau wa kurasa hii si ninyi tu hata kwa upande wetu tumeingiwa na mshangao wa ajabu sana juu ya hili suala kwani dola 2,500 iliyosawa na pesa taslim ya kitanzania kwa bei ya pesa hiyo ya kigeni katika maduka ya kubadirishia fedha za aina hii ni kama milioni nne laki tatu na sabini na tano(4,375,000)...mpaka sasa tunajitahidi kumtafuta kaka vicent aliweke wazi zaidi hili suala kwa washabiki na wadau wa filamu hapa bongo...asante!

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign