DINO: NAPENDA SANA KUFANYIWA MASAJI

Dennis Sweya ’Dino’. WIKI hii tunaye msanii wa filamu anayekwenda kwa jina la Dennis Sweya ’Dino’. Naye anajibu na kufafanua maswali mliyomuuliza, shuka nayo.
Filamu imefika wapi?
Unaionaje tasnia ya filamu kwa sasa, tunapanda, tuko palepale au tunashuka? Mama Swaumu, Dar, 0768579513
DINO: Kwa kweli tunapanda kwa sababu tulikotoka ni tofauti na tulipo.
Asilewe sifa
Napenda uigizaji wako na pia hauna skendo chafu, songa mbele kaka usilewe na sifa. Mwaipopo, Dar, 0653317354
DINO: Asante, nashukuru kwa kunipa moyo.
Kwa nini sinema za ngumi?
Dino wewe ni mkali wa kuigiza muvi za mapigano, kwa nini unapenda sehemu hizo tu? Elia, Iringa, 0718085308
DINO: Siyo kwamba napenda sehemu hizo tu, kama unafuatilia muvi zangu, nimecheza sehemu nyingi tofauti pia sehemu za mapigano nazipenda kutokana na mashabiki wangu kupenda hivyo.
Skendo ya ujambazi
Inatajwa wewe ni jambazi wa kimyakimya na unahusishwa na tukio la uvamizi wa Benki ya NMB Mwanga, je, ni kweli? Amani Ngossi, Zanzibar, 0757113834
DINO: Mimi ni mtu niliyekulia kwenye maadili, sijawahi kuwa mdokozi, kibaka wala jambazi na hilo tukio unalolizungumzia siyo kweli umeamua mwenyewe kuliongelea kutokana na jinsi ninavyocheza lakini siko hivyo.

Huyu anamjua
Anaishi Sinza, ana msichana amezaa naye watoto wawili. Beatrice, 0713931270
DINO: Kweli, lakini siyo msichana ni mke wangu na nimezaa naye watoto wawili.

Ushawishi wa mademu
Dino nakukubali sana mtu wangu, je, unajiepusha vipi na mademu katika fani yako? Salim Liundi, Dar, 0719319190
DINO: Najitaidi kuwaepuka kwa sababu namheshimu mke wangu na huwa nawaeleza ukweli kuwa ni vigumu kuwa nao kwani nina familia.

Ameoa?
Kaka Dino wewe ni kifaa, vipi umeoa? Naomba namba yako ya simu kwa maongezi zaidi. Rehema, Dodoma, 0718433131
DINO: Ni maongezi ya aina gani kwanza, je, ni ya kikazi au kimapenzi? Kama ni ya kikazi, nitakutafuta.

Nje ya fani
Kaka hongera kwa kipaji chako, je, tofauti na sanaa unafanya kazi gani nyingine? Mage, Muheza, 0713486286
DINO: Mimi ni mfanyabiashara.

Wanawake aliotoka nao
Umelala na wanawake wangapi na unapenda kufanyiwa nini na mpenzi wako ukiwa faragha? Msomaji, 0756207716
DINO: Idadi ni siri yangu, nikiwa faragha huwa napenda mke wangu anifanyie masaji.

Ufagio
Kaka Dino napenda sana unavyomudu kuigiza, yaani uko juu pia napenda siku moja nikuone kwa karibu. Msomaji, 0719166722
DINO: Karibu sana, tafuta muda nami nikiwa na muda tutaonana.

Posted by Bongo Film Data Base on 12:41 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for DINO: NAPENDA SANA KUFANYIWA MASAJI

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign