WADAU WA FILAMU KUKUTANA KESHO LEADERS CLUB.

KESHO siku ya Jumatano tarehe 15/08/2012 kuanzia muda wa saa tano kamili asubuhi kutakuwa na mkutano mkubwa kwa Wadau wa filamu Jijini Dar Es Salaam utakaofanyika katika viwanja vya Leaders club, mkutano huu unatarajia kuwakutamisha wadau karibu wote wa tasnia ya filamu Swahiliwood, akiongea na FC Rais wa shirikisho la filamu Simon Mwakifwamba ameomba wadau wote kufika mapema kwa ajili ya mkutano huo.


“Kesho ni siku muhimu sana kwa kila mdau wa tasnia ya filamu kufika katika mkutano huu ambao tumeitisha kwa siku hiyo, kila msanii, muongozaji, msambazaji, anatakiwa kuwa amefika katika viwanja vya Leaders Club na kuhudhuria mkutano huo ambao kutakuwa na mambo mengi ya kujadili kwa siku hiyo,”anasema Mwakifwamba.
Makundi yanayotarajia kuwepo katika mkutano huo ni Waigizaji, Watayarishaji wa filamu, Waongozaji wa filamu, Waandishi wa muswada, walimu wa vikundi vya sanaa, watafuta mandhari, wapiga picha za filamu, wapambaji, Wasambazaji, wachekeshaji, na wadau wa filamu kwa ujumla.
Mnaombwa kuwahi mapema kwa ajili kwenda na muda ili ajenda zilizopangwa ziweze kuongelewa zote kwa maslahi ya tasnia ya filamu kwa ujumla wake nyote mnakarishwa.
 CHANZO; FILAMU CENTRAL

Posted by Osxarguder • The Creator • on 9:29 PM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for WADAU WA FILAMU KUKUTANA KESHO LEADERS CLUB.

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign