KELELE ZA USIMAMIZI KAZI ZA WASANII MBONA HATUZIONI NA KUZISIKIA TENA?
kinyemi, mpya, slide, workshop 1:08 PM
HII ni sehemu ya Hotuba iliyosomwa Bungeni na Mh. Dr. Fenela Mukangara kipengere kinachowahusu wadau wa filamu moja kwa moja kama kuna swali au mjadala utashiriki nasi kuhusu mustakabali wa tasnia ya filamu Swahiliwood.
.
.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2011/12 Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza imekagua jumla ya filamu 98 ambapo filamu za ndani 48 zilikaguliwa na kupewa madaraja. Kati ya hizo, 1 ilipewa daraja R ikimaanisha filamu hiyo hairuhusiwi kuoneshwa mahali pa hadhara.
Filamu zilizokaguliwa kutoka nje ya nchi ni 50, kati ya hizo, 3 zilipewa daraja R ambapo moja ni kutoka Liberia na mbili kutoka Norway. Aidha, Bodi imeweka alama maalum kwenye filamu zilizokaguliwa ikiwa ni moja ya njia ya kuhakikisha filamu zote zisizokaguliwa zinajulikana na wahusika kuchukuliwa hatua.
Katika kipindi cha mwezi Julai, 2011 hadi Juni, 2012 Bodi ilitoa vibali 21 vya kutengeneza filamu kwa Watanzania, na 84 kwa wageni.
Mheshimiwa Spika, Bodi ya Ukaguzi wa filamu na Michezo ya Kuigiza iliandaa na kufanya mafunzo elekezi kwa Maafisa Utamaduni wa Wilaya nchini kwa lengo la kuboresha Bodi za Filamu za Wilaya.
.
Mheshimiwa Spika, Bodi ya Ukaguzi wa filamu na Michezo ya Kuigiza iliandaa na kufanya mafunzo elekezi kwa Maafisa Utamaduni wa Wilaya nchini kwa lengo la kuboresha Bodi za Filamu za Wilaya.
.
Bodi ilisambaza Sheria na Kanuni za Filamu na Michezo ya Kuigiza kwa Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Wilaya nchini. Bodi imeendesha mijadala mitatu kwa wadau wakiwemo watengenezaji filamu na wasanii wa filamu. Vilevile, imefanya mkutano kuhusu Mustakabali wa Tasnia ya Filamu katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru na mkakati kwa kipindi cha miaka 50 ijayo.
.
.
Mkutano huu umesaidia wadau walioshiriki kubuni mikakati mbalimbali ya kuboresha tasnia hii. Mikakati hiyo ni pamoja na kuhakikisha kuwa filamu na michezo ya kuigiza vinalenga zaidi katika kutangaza utaifa, uzalendo, maadili na utamaduni wa Tanzania. Nia ni kuondokana na filamu ambazo zimemezwa na tamaduni za nje.
Vile vile, kuhakikisha kuwa tasnia ya filamu inakuwa rasmi ili ichangie pato la taifa na la msanii binafsi.
Mheshimiwa Spika, Bodi ya Filamu ilizindua Kanuni za Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ambapo nakala 4,200 za Kanuni na nakala 4,200 za Sheria zilisambazwa.
.
Mheshimiwa Spika, Bodi ya Filamu ilizindua Kanuni za Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ambapo nakala 4,200 za Kanuni na nakala 4,200 za Sheria zilisambazwa.
.
Aidha, utafiti uliofanywa na Bodi kwa kushirikiana na wadau wa filamu umebaini kuwepo kwa Makampuni 127 yanayojihusisha na uongozaji, utengenezaji, uzalishaji na usambazaji wa filamu kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee. Makampuni hayo yameajiri watu kati ya watatu (3) na kuendelea na kwa pamoja yanatoa wastani wa ajira 508.
ASANTE CHANZO: FILMU CENTRAL
ASANTE CHANZO: FILMU CENTRAL