WATALAAMU WA MAMBO WANASEMA PICHA HUZUNGUMZA ZAIDI ILA LEO TUONE SAUTI KIUNDANI KIDOGO
habari, mpya, slide 11:49 AM
Sauti:Ni kitu cha msingi sana kwenye filamu,sauti katika filamu inapokua nzuri inawafanya waangaliaji kuipenda filamu,unaweza kuwa na picha mbaya na watuwakaendelea kuangalia lakini inapotokea kuwa na sauti mbaya kila mtu hatamani kuendelea kuangalia filamu hiyo.hivyo basi sauti ni jambo la msingi zaidi ya video. Mojawapo ya chombo kinachotumika katika kuleta sauti kwenye filamu ni microphone au kipaza sauti. Kuna aina nyingi ya vipaza sauti lakini,katika filamu tunatumia aina 4 za vipaza sauti nazo ni:
1. Boom mics
2. Lavalier mics
3. Handheld mics
4. Wireless mics
Katika lecture room ya leo tunaangalia kwa undani Boom mics inavyofanya kazi katika uzalishaji wa filamu. BOOM MICS huwa inakuwa imewekwa kwenye mti wake maalum unaojulikana kama boom pole ambayo inakuwa imebebwa na mtu anaejulikana kama boom operator.
Ni vizuri katika boom lako uweke mic housing ambayo huwa na manyoya na kazi yake ni kupunguza upepo unaokuwepo location nah ii itasaidia kupata sauti iliyotulia.
katika kutumia boom kuna ujuzi unaotakiwa kuwa nao kama Boom Operator na hii inasaidia kuweza kupata sauti nzuri na inayotakiwa,hapa namanisha kuwa mtu yoyote akipewa boom anauwezo wa kulitumia lakini je?anatumia kwa usahihi?kwa kuzingatia hilo basi angalia au soma kwa makini kanuni za kuweza kutumia boom lako vizuri kama unataka kuwa boom operator mzuri.
kwanza kabisa ili uwe Boom Operator mzuri unatakiwa kuwa na stamina,kuwa na uwezo mzuri wa kusikia na kuona ili iwe rahisi kuweza kubadilisha position ya Boom lako.
MAMBO YA KUZINGATIA KAMA BOOM OPERATOR
Usiweke Boom lako pembeni ya mdomo,hakikisha Boom linakuwa direct kwenye mdomo unaoongea.
Haya ni mambo ya msingi sana ambayo kama unataka kuwa Boom operator mzuri unapaswa kuzingatia hivyo kupata sauti nzuri kkatika filamu zetu tunazoziandaa.
- Angalia frame line ya camera kabla ya kuanza ku shoot,kisha weka boom mic yako karibu na msanii bila kuingia kwenye frame.
- hakikisha boom yako inakuwa direc pointed kwa msanii
- mara zote vaa over-ear headphones
- zingatia visual cues na feedback kutoka kwenye mixer na camera person (mpiga picha)
- Achia XLR waya uwe mrefu kulingana na movement utakazokuwa unafanya lakini kuwa makini usijeukakutega na kushindwa kufanya movement.
- kwa kuwa utakuwa umesoma script hivyo itakuwa rahisi kujua ni movement gani zitakuwepo kwenye scene hiyo lakini hakikisha unakuwa na mawasiliano ya karibu na camera person ili usijekuingia kwenye frame line.
- funga vizuri cable zako ili kuzuia kusiwe na sauti kutokana na kujizungusha au cable kujigongagonga kwenye boom pole.
- hakikisha umepanua miguu yako kidogo ili uwe na balance,confortable kuweza kufanya movement zozote zile.
Nakaribisha maswali na maoni kuhusu tasnia hii ya filamu na sanaa kwa ujumla.