''KIJIJI CHA TAMBUA HAKI YENYE WASHIRIKI 400 YA STEVEN KANUMBA YATAMBULISHWA RASMI '',
habari, mpya, slide, sokoni 12:30 AM
Rekodi ya Devils Kingdom aivunja mwenyewe sasa, baada ya kutoa filamu na mastaa kibao wa hapa nchini na mmoja ya mastaa toka nigeria na kushirikishi watu zaidi ya mia moja ndani yake katika kuitayarisha filamu hiyo ambapo hapakuwahi kutokea wasanii wengi kwa idadi kama ile kukutanishwa ndani ya kazi moja kwenye historia yote ya tasni hii ya filamu hapa nchini..filamu hiyo ilifanywa kwa lugha ya kiswahili na kiingeleza kidogo kwenye sehemu kadhaa ndani yake hivyo kuipelekea ifanye vyema kwenye soko la ndani na la nje ya nchi pia.
Baada ya filamu hiyo kutoka tulitegemea kuona watayarishaji wengine nao wa hapa nchini Tanzania kufanya kama mtayarishaji huyu kutoa ridhiki kwa watu wengi kiasi kile cha kwenye Devils Kingdom ila hapakutokea mtayarishaji mwingine kufanya hivyo, sasa Kanumba mwenyewe ameivunja rekodi hiyo kwa kutayarisha filamu nyingine ijulikanayo kwa jina la ''KIJIJI CHA TAMBUA HAKI'' iliyo husisha washiriki mia nne (400) iliyofadhiriwa na POLICY FORUM itakayo ingia sokoni mwishoni mwa mwezi huu chini ya usambazaji Steps Entertainment ambayo kaitambulisha rasmi katika ukumbi wa Kambarage ,Hoteli ya Regency jijini Dar es salaam..
SWALI LA KIZUSHI! ,Enyi watayarishaji wengine mwajifunza nini na mna lipi la kusema juu ya hatua hii kubwa ya mtayarishaji mwenzenu Bw. Kanumba? mbali na kumsifia tu kila mwojiwapo?

The great
nikisisitiza kuwa ni filamu ya kipekee hakuna mapenzi humo,hakuna
majumba ya kifahari wala suti nzuri.ni maisha halisi anayoishi Mtanzania
wa leo kijijini.