MIKE; WASANII JIUNGENI NA VYAMA VYENU HUSIKA.
habari, mpya 11:30 PM
MWENYEKITI wa Chama cha Waigizaji Taifa Michael Sangu amewahimiza
wadau mbalimbali pamoja na Wasanii wote kwa ujumla kujiunga na vyama
husika katika fani za filamu, akiongea Fc Mwenyekiti huyo amesema kuwa
iwapo vyama vyote vitakuwa hai ni wazi itakuwa rahisi kwa Shirikisho
kuwafikia na kubaini matatizo yanayowakabiri katika tasnia hiyo ya
filamu kutoka Swahiliwood.
“Vyama vyote viongozi wake wapo muda wote katika kuhakikisha wanachama wapata huduma stahili kwa ajili ya kujiunga katika vyama hivyo na kutoa maelezo na michakato inayokwenda katika tasnia ya filamu kwa sasa, na lengo ni kujenga umoja na kutatua matatizo ambayo tumekuwa nayo kwa muda mrefu katika fani yetu,”anasema Mike.
Katika kuimarisha shirikisho mwenyekiti huyo amesema kuwa kwa sasa kila msanii ni lazima ajisajili katika chama kinachomhusu ili kujenga utambulisho popote na kuwa na kauli moja kuhusu harakati na changaoto zinazojitokeza katika filamu za Swahiliwood Tanzania .
Kwa wale ambao ni Waongozaji wa filamu na hawajajiunga na Chama cha TAFIDA wanaweza
kuwasiliana na Katibu wa Taifa Patrick Komba kwa namba 0714 259 526 wakiwa na Picha mbili ndogo, nakala ya kitambulisho cha Mpiga kura pamoja kiasi cha Tshs. 2,500/ tu za kitanzania kwa ajili ya Fomu.
Chama cha Wapiga picha jongefu (TCA) wanaweza kuwasiliana na Mwenyekiti au Katibu wa Chama hicho kwa namba 0715 939 999 Mwenyekiti, 0714 257 054 Katibu Mahitaji ni kuwa na picha ndogo mbili na kiasi cha Tshs. 3,000/ kwa ajili ya fomu.
Chama Cha Waigizaji (TFDAA) kuna mikoa mitatu kwa wale wanaoishi Kinondoni fomu zinapatikana kwa wahusika wafuatao pamoja na namba zao za simu katika mabano Kinondoni (Mwenyekiti Ali Baucha 0715 994 995), Ilala (Husna Mgeni 0713 317 610) na kwa wasanii wa Temeke wawasiliane na Dile kwa namba 0714 561 800. Mwigizaji atatakiwa kuwa na picha ndogo na Tshs. 3,000/ kwa ajili ya fomu.
Ni matarajio yetu kuwa wengi mtajitokeza, lakini kwa wale wa Kinondoni pia mnaweza kutembelea www.tdfaa.blogspot.com kwa mawsiliano zaidi.
Chanzo; Filamu central