AIBU GANI HII JARIDA LA BABKUBWA?!
habari, slide, udaku, workshop 10:43 AM
INCISIVE MEDIA KUPITIA UKURASA WAKE WA BONGO FILM DATABASE INAYOFURAHA KUONA UKURASA WAKE UKITIMIZA VYEMA SEHEMU YA MALENGO NA VIAPO VYAKE KWA TASNIA YA SANAA UHUSUSANI SANAA ZA MAIGIZO AMA KWA JINA FUPI WAWEZA KUITA FILAMU KWA HAPA NCHINI TANZANIA. BONGO FILM DATA BASE SASA INAKUWA NDIYO KIINI NA CHANZO CHA TAARIFA NA HABARI ZIHUSIANAZO NA WASANII WA FILAMU , KAZI ZAO PAMOJA NA WADAU WAIZUNGUKAYO KWA UJUMLA KWA SASA .
KUNA MENGI SANA JOPO LA LETU LINANUWIYA KUYAFANYA KWA LENGO LA KUTIMIZA AZIMA YETU KUU YA KUUNGANA NA WADAU WENGINE WALIO KUSUDIA KUIKUZA NA KUIENDELEZA SANAA HII KUPITIA TASNIA YA FILAMU HAPA NCHINI KWA KUFIKIRI NA KUTAFAKARI MAWAZO YAO KABLA HAWAJA YAWEKA WAZI KWA JAMII..
AWALI WA YOTE HAYO KUNA JAMBO AMBALO LINATUSIKITISHA MPAKA SASA LA HAWA WADAU WENZETU KUTUMIA MAKALA ZETU PASIPO KUTOA TAARIFA , WALA KUTOA SHUKRANI KWETU KWA HATA KUTOTUTAJA JINA LETU AU NI WAPI WAMEZIPATA MAKALA HIZO.
SUALA HILI LIMEFANYWA NA WAHARIRI WA JARIDA LA BABKUBWA MWEZI WA NNE TOLEO MAALUMU LA MAREHEMU STEVEN KANUMBA...
MRATIBU MKUU NA MMOJA YA WADAU WAKUBWA WA KURASA WA
BONGO FILM DATABASE Bwn.MPANGALA TUKAONELEA KULIFUATILIA SUALA HILI KWA UKARIBU ZAIDI KUONA
NI NAMNA GANI WATAWEZA FANYA JUU YA HILI SUALA ILA TUKASHINDWA WAFIKIA WAHARIRI
WA JARIDA HILI KUTOKANA KUKOSA MAWASILIANO YAO KITU AMBACHO NI UPUNGUFU MKUBWA
SANA NA NI UKIUKWAJI WA SHERIA ZA UTARATIBU WA CHOMBO CHA HABARI WA KUTOKUWA
NA MAWASILIANO WALA ANWANI YA CHOMBO HUSIKA KWENYE MACHAPISHO YAKE.
PIA
TULISITA KUANDIKA MAKALA JUU YA HILI HAPO MWANZO KWA KUHOFIA KUHAMASISHA WATU
KWENDA KULINUNUA JARIDA HILI KUTHIBITISHA HILI SUALA KWANI TUTAKUWA TUNAFAIDISHA WAO TU KWA MARA
NYINGINE TENA KITU AMBACHO HATA WAO HUZAMILIA KUONGEZA MAUZO YA JARIDA LAO KWA
KUJIFAIDISHA WAO TU KWA KUTUMIA MAKALA ZA WATU WENGINE BILA YA HATA KUONESHA
UMUHIMU WA VYANZO VYA MAKALA WANAZOCHAPISHA NA NINAWASIWASI YA KUWA HAWA WADAU SIKU ZOTE HUCHAPA MAKALA AMBAZO HAWAJATAFITI WAO. NA KAMA TUTAKUWA TUMEWAONEA
AMA KUWASINGIZIA KWA HILI TAFADHALI TUNAWAOMBA MJITOKEZE KUKANUSHA HILI
HADHARANI..
SHUKRANI NYINGI ZIWAFIKIE WADAU WETU WA KARIBU SANA TUNAOSHIRIKIANA NAO KUUENDELEZA UKURASA HUU KILA SIKU AKIWEMO KAKA RAMA MSANGI ,MPANGALA, HAULE, EMMANUEL, NA DADA TINA.
REJEA KIUNGO CHA MAKALA HII YA APRI 15 KWA KUMBUKUMBU ZAIDI