AIBU GANI HII JARIDA LA BABKUBWA?!INCISIVE MEDIA KUPITIA UKURASA WAKE WA BONGO FILM DATABASE  INAYOFURAHA KUONA UKURASA WAKE UKITIMIZA VYEMA SEHEMU YA MALENGO NA VIAPO VYAKE  KWA TASNIA YA SANAA UHUSUSANI  SANAA ZA MAIGIZO AMA KWA JINA FUPI WAWEZA KUITA FILAMU KWA HAPA NCHINI TANZANIA. BONGO FILM DATA BASE SASA  INAKUWA NDIYO  KIINI NA CHANZO CHA TAARIFA NA HABARI  ZIHUSIANAZO NA WASANII WA FILAMU , KAZI ZAO PAMOJA NA WADAU WAIZUNGUKAYO KWA UJUMLA KWA SASA .

 KUNA MENGI SANA JOPO LA LETU LINANUWIYA KUYAFANYA KWA LENGO LA KUTIMIZA AZIMA  YETU KUU YA KUUNGANA NA WADAU WENGINE WALIO KUSUDIA KUIKUZA NA KUIENDELEZA SANAA HII KUPITIA TASNIA YA FILAMU HAPA NCHINI KWA KUFIKIRI NA KUTAFAKARI MAWAZO YAO KABLA HAWAJA YAWEKA WAZI KWA JAMII..

TUMEKUWA TUKIANDIKA KILA KUNAKOKUCHA NA HATA KUFANIKISHA MALENGO YETU YAKUUFANYA UKURASA WA BONGO FILM DATABASE UNAKUWA NDIYO KIINI NA CHANZO CHA TAARIFA NA HABARI ZA TASNIA HII YA FILAMU HAPA NCHINI TANZANIA, NA HII IMEJIZIHILISHA MIEZI KADHAA ILIYOPITA KWA MAKALA ZAKE KUTUMIKA KWENYE VIPINDI VYA REDIO UHURU CHA FILAMU ZETU NA CLOUDS FM KUPITIA KIPINDI CHAKE CHA MOVIE LEO NA HATA KUPITIA TELEVISHENI YA CLOUDS KWENYE KIPINDI CHA TAKE ONE NACHO KUTUMIA MAKALA ZETU KITU AMBACHO ILIKWA FARAJA KUBWA SANA KWETU.
AWALI WA YOTE HAYO KUNA JAMBO AMBALO LINATUSIKITISHA MPAKA SASA LA HAWA WADAU WENZETU KUTUMIA MAKALA ZETU PASIPO KUTOA TAARIFA , WALA KUTOA SHUKRANI KWETU KWA HATA KUTOTUTAJA JINA LETU AU  NI WAPI WAMEZIPATA MAKALA HIZO.


NA HIVI JUZI JUZI HALI HII IMEJIRUDIA TENA YA KUTUMIKA KWA MAKALA ZETU BILA YA SISI KUPEWA TAARIFA WALA KUTAJWA KUWA NDIYO CHANZO CHA MAKALA [HADITHI] HIYO  KITU AMBACHO NI UKIUKAJI WA MAADILI YA UAANDISHI WA HABARI KWA VIFUNGU VYA SHERIA TOKA TCRA.SUALA HILI LIMEFANYWA NA WAHARIRI WA JARIDA LA BABKUBWA  MWEZI WA NNE TOLEO MAALUMU LA MAREHEMU STEVEN KANUMBA...

MRATIBU MKUU NA MMOJA YA WADAU WAKUBWA WA KURASA WA BONGO FILM DATABASE Bwn.MPANGALA TUKAONELEA KULIFUATILIA SUALA HILI KWA UKARIBU ZAIDI KUONA NI NAMNA GANI WATAWEZA FANYA JUU YA HILI SUALA ILA TUKASHINDWA WAFIKIA WAHARIRI WA JARIDA HILI KUTOKANA KUKOSA MAWASILIANO YAO KITU AMBACHO NI UPUNGUFU MKUBWA SANA  NA NI UKIUKWAJI  WA SHERIA ZA UTARATIBU WA CHOMBO CHA HABARI WA KUTOKUWA NA MAWASILIANO WALA ANWANI YA CHOMBO HUSIKA KWENYE MACHAPISHO YAKE. 

PIA TULISITA KUANDIKA MAKALA JUU YA HILI HAPO MWANZO KWA KUHOFIA KUHAMASISHA WATU KWENDA KULINUNUA JARIDA HILI KUTHIBITISHA HILI SUALA   KWANI TUTAKUWA TUNAFAIDISHA WAO TU KWA MARA NYINGINE TENA  KITU AMBACHO HATA WAO HUZAMILIA KUONGEZA MAUZO YA JARIDA LAO KWA KUJIFAIDISHA WAO TU KWA KUTUMIA MAKALA ZA WATU WENGINE BILA YA HATA KUONESHA UMUHIMU WA VYANZO VYA MAKALA WANAZOCHAPISHA NA NINAWASIWASI YA KUWA HAWA WADAU SIKU ZOTE HUCHAPA MAKALA AMBAZO HAWAJATAFITI WAO. NA KAMA TUTAKUWA TUMEWAONEA AMA KUWASINGIZIA KWA HILI TAFADHALI TUNAWAOMBA MJITOKEZE KUKANUSHA HILI HADHARANI..SHUKRANI NYINGI ZIWAFIKIE WADAU WETU WA KARIBU SANA TUNAOSHIRIKIANA NAO  KUUENDELEZA UKURASA HUU KILA SIKU AKIWEMO KAKA RAMA MSANGI ,MPANGALA, HAULE, EMMANUEL, NA DADA TINA.

REJEA KIUNGO CHA MAKALA HII YA APRI 15 KWA KUMBUKUMBU ZAIDI

Posted by Osxarguder • The Creator • on 10:43 AM. Filed under , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for AIBU GANI HII JARIDA LA BABKUBWA?!

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign