"HIVI RUGE MUTAHABA NI NANI?"

Ruge Mutahaba
Ruge Mutahaba Mkurugenzi mwendeshaji Clouds Media Group.



UTAWALA ni kipaji na hasa pale utakapogundua kuhusu uwezo wako, si kila mtu anaweza kuwa mtawala na kuweza kufanikisha jambo linalokusudiwa iwe katika jamii hata katika familia yako, lakini kuna watu wanaweza kufanya hivyo leo nafikiri ni vema kumuongelea Mh. Ruge Mutahaba mkurugenzi mwendeshaji wa Clouds Media Group.


Ruge Mutahaba, Vick Kamata, Tudy
Ruge akiwa na Mh. Vick Kamata na Mtayarishaji wa wimbo maalum wa Mboni Yangu
Hivi Ruge Mutahaba ni nani hadi watu wote wamsikilize?
Naamini kuwa ndio maswali mengi ambayo sisi wapenda majungu, tusiona mazuri wala upendo akufanyiaye mtu mwingine wakati wa matatizo, nimegundua kuwa chuki ujengwa na watu dhaifu na wabinafsi kutokana na uvuvi wao pia kukosa ubunifu kwa yale wanayoyafanya katika jamii.
Wema Sepetu
Wema Sepetu Mwigizaji Swahiliwood akiimba wimbo wa Mboni yangu.
Binadamu kama binadamu ana mapungufu yake, lakini usimhukumu kwa sababu eti umemsikia mtu au jamaa yako akimshutumu kama ni mtu mbaya na wewe kwa ujinga wako ukiendeleza chuki maneno ya hovyo kwa sababu tu ya huyo aliyetengeneza uhasama huo, Ruge ndiye mtu pekee ambaye ana uwezo wa kutoa msaada kwa kutumia kile alicho nacho, lakini sisi ubaki na maneno yetu ya fitina na majungu tu na si kutoa hata kile kidogo tulicho nacho.
Najua wengi mtasema kuhusu makala hii lakini ukweli unabaki pale pale kuwa Bongo watu kama Ruge ni wachache sana lakini kwa sasa nahisi yupo peke yake tu, nimeshuhudia harakati zake nyingi sana akichangia wananchi mfano mafuriko yaliyotokea Morogoro kule Kilosa ni yeye tu ndio alibuni na kuratibu zoezi ambalo pengine nilitegemea wazo lile kufanywa na Serikali au taasisi yoyote ya kijamii.
.
Ali Kiba
Ali Kiba Msanii wa muziki kizazi kipya naye alikuwepo kutoa support kwa Sajuki.
Baada ya msiba wa nyota wa filamu kutokea maneno mengi yalisikika kuhusu wizi wa michango ya fedha iliyotolewa lakini wengi walimtuhumu Ruge kama mpigaji na kila sifa mbaya alitwishwa lakini kwa sababu anatujua sisi Wabongo ambao maneno mengi bila vitendo alipotezea na kukaa kimya lakini naamini kuwa hata katika nafsi yake alisema kuwa kumsaidia mtu ni shida na lawama.
Lakini nakumbuka kuwa Mwalimu wangu aliwahi kunieleza kuwa hakuna msaada utolewao bure lazima utalipia tu iwe kwa kujua au kwa kutojua kuwa umelipa au bado, hili si jambo la kusahau, linapotokea jambo linahitaji utatuzi kwetu kidogo hatuwezi kufanya hivyo, basi inapotokea mtu kufanya ni vema kumuunga mkono kuliko shutuma hilo limetokea na kuonyesha ni jinsi gani kila msanii anahitaji kufa na tai yake shingoni.
.
Suleiman Msindi, Amini, Dito
Dito, Amini, Afande Sele walikuwepo nao katika kumchangia Sajuki.
Waswahili usema kuwa Mungu hamfichi mnafiki ikifika ndugu yetu Sajuki anaumwa na ilikuwa inatakiwa fedha kwenda kutibiwa nje ya nchi yaani India, kila mwenye roho safi alitoa alichokuwa nacho pia waandishi walijitahidi kuujulisha umma kama msanii huyo anaumwa na anahitaji msaada wa matibabu, lakini michango ilikuwa ya kusuasua na hata yale makundi yanasumbua Swahiliwood yaani Bongo Movie na TAFF yalichemka kufanikisha.
.
William John Mtitu
Mtayarishaji Mtitu akiimba naye katika wimbo wa Mboni yangu.
Nilifanya juhudi kwa kila njia ili mradi tu Sajuki aweze kusaidiwa uelewa ulikuwa mdogo sana, tuliishia kumpigia simu tu huku tukimpa Sajuki matumaini hewa bila upatikaji wa hizo fedha, hata pale walipofika viongozi wa kiserikali nao bado walikuwa nyuma kuhusu maamuzi au njia ambayo ingetumika ili kupata fedha.
Kamati ziliundwa huku shutuma nazo zikitawala kila mtu akishidwa kumwamini mwingine, hadi pale mgonjwa mwenye pamoja kuumwa alikata shauri na kusema sisikii maneno majungu ya mtu nahitaji kumuona Ruge kwa msaada wangu ili nipate kutibiwa, kweli alifanya juhudi hadi alionana na Ruge Sajuki anasema kuwa alikaa na Ruge kwa muda mfupi alionyesha uwezo wake kubuni na kuratibu tukio la kumwezesha kupata fedha.
“Nilimweleza Ruge nimekuja ndugu yangu unisaidie, nahitaji fedha kwa ajili ya matibabu na siku zinavyozidi kwenda ndio naumia, hadi sasa naona ahadi tu ndio nyingi lakini hazina uhakika wa kupata fedha, nilikuwa nikiongea huku nikiwa na mke wangu na rafiki yangu Dino,”anasema Sajuki.
Baada ya hapo ndipo Ruge alipomjibu kwa kusema kuwa anaguswa na tatizo lake kwa sababu ameenda yeye atamsaidia kabla alifuatwa na wasanii wengine lakini kutokana na wasanii kutokujitambua na kumuona kama yeye ni mtu dhulumati ilimpasa kubaki kama mchangiaji mwingine tu ambaye angeweza kutoa kiasi alicho nacho kwa upendo wake au kuguswa na tukio hilo.
“Hivi sasa tunawaogopa sana nyinyi wasanii walikuja wenzako na kuniomba lakini sikuwa tayari kufanya lolote lakini kwa sababu umekuja mwenye sina budi kukusaidia na tukio hilo linaanza kuanzia sasa lazima tujue tunapata hiyo fedha ya matibabu,”alisema Ruge.
.
Ester Bulaya, Dina Marios, Asma Makau
Ester Bulaya, Dina Marios, Asma Makau wakiwa studio kwa ajili ya kuchangisha fedha za matibabu kwa ajili ya Sajuki.
Ruge alichofanya ni kubuni wazo haraka nalo lilikuwa kutumia wimbo uliokuwepo katika filamu ya wasanii hawa yaani Sajuki na Wastara kutoka katika filamu ya Mboni yangu kuimbwa na wasanii wapatao 27 wakijumlishwa na Waheshimiwa Wabunge zoezi lilofanyika siku hiyo hiyo na kila mtu alitii wito ikiwa ni Wabunge na wasanii wote hasa wa muziki kwanini Ruge asiitwe Shujaa wa Maafa?
.
Mzee Yusuf
Mzee Yusuf akiimba wimbo wa Mboni yangu.
Pamoja na hayo jambo lakusitikisha ni ushiriki wa wasanii wenye shughuli kwa maana ya waigizaji ni wasanii wane tu ndio waliotia sauti katika wimbo wa Mboni yangu ambao ni Wema Sepetu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na William Mtitu sambamba na mhusika Wastara hiyo inaonyesha ni jinsi gani tulivyogawanyika lakini siku ya siku tutakuwa wakwanza kusema Ruge kapiga hela tuache maneno haya ya kuwachafua watu wakati sisi hatuwezi kitu.
Ukisoma tu habari au kusikiliza Redio hata Televisheni utagundua kuwa wasanii wana matabaka makubwa ambayo hayawasaidii zaidi ya kuwatia umaskini tena wa kujitakia, Dina alisema kuwa kuna na wasanii wa filamu ambao wamekuwa wakijitoa hata uwaite saa nane za usiku watakuja ambao ni Mtitu, Wema na Shilole hili ni tatizo.
.
Juma kilowoko
Sajuki Mtayarishaji na Muongozaji wa filamu Swahiliwood.
Inawezekana kuna wasanii hawakuja kwa sababu hawakupigiwa simu kutokana na uzito wao lakini pia wadau hata kama wasanii ni wazito katika matukio ya kijamii tuwaite tu wasipokuja lakini ujumbe wamepata, kwani nimeamua kumpongeza Ruge kwa kuwa mbunifu hata mimi ungenipa Redio na Televisheni na kuniambia nifanye tukio litalomshawishi mtu kuchangisha fedha kama hiyo bado ingekuwa kitendawili.
Tunajifunza nini kutokana na tukio la Sajuki?
Bado safari yetu ni ndefu sana kujikomboa kutoka mikononi mwa utumwa uliotuzingira kwa sababu ya ubinafsi, wezi wanaodhulumu kazi zetu kwa bei nafuu kwa kununua haki zetu hatuwaoni, ni kweli ilimpasa Sajuki kuingia location ili apate fedha za matibabu? Kumbe wasanii hawakopesheki jambo linaloashiri mwisho mbaya.
Ruge Mutahaba
Ruge Mutahaba mratibu wa zoezi la kumchangia Sajuki.
Hatuwalaumu wasanii kwa kukosa fedha bali kwa kukosa umoja na kujenga hoja au sera zinazoweza kuaminiwa na kuonyesha thamani yenu kwa ajili ya kuwasaidia, mara nyingi usikika wasanii wakishirikiana na watu maarufu au viongozi lakini hakuna msaada wa kudumu nahisi kuwa hakuna mtu anayewa kutoa hoja na ukweli kuhusu maslahi ya jumla.
Leo hii katika tasnia ya filamu kuna taasisi mbili zinazohitaji kuongoza wasanii kila unavyongea na upande mmoja kila mtu anajitahidi kumlamu mwenzake wengi wanajiuliza malumbano haya ya Bongo Movie na TAFF ni lini yataisha na kuwa wamoja watakaokaa na kujadili kwa kauli moja na kusema biashara ya filamu iende hivi?
Yaliyojitokeza katika msiba ni aibu kuyasema lakini ilikuwa doa kubwa kulisafisha yahitaji muda sana maana tulishuhudia watu wakipiga picha au kutawala uongozi huku hata mitafaruku ikiendelea chini kwa chini kama vile kutengenezwa Beji zilizotaka kutambulisha pande moja bila sababu ya msingi, lakini pia wasanii kugombana kutokana na makundi hayo ni aibu sana.
Hivi ni kweli unaweza kupendwa na mtu mwingine bila ya wewe kujipenda?
Hili tumeliona kwa Sajuki msanii anahitaji kupata fedha za matibabu lakini ilikuwa ni utata hadi pale mtu anayelaumiwa kuingia na kufanya harambe, kwa wasanii kubuni kitu chochote lakini haikutokea hivyo wasanii waliojitokeza ni watatu tu, duh,,,
.
Wastara Juma
Stara alishiriki kuimba wimbo wa Mboni yangu kwa ajili ya kumchangia mumewe.
Binadamu kama binadamu hayupo aliyekamilika kwa asilimia mia moja, lakini kama kuna mtu anaweza kufanya kazi au tukio la kijamii apimwe kwa jambo hilo haina maana kuwa wasanii wote hawajielewi bali kuna wachache wanaowapeleka wengine shimoni, tujadili kuhusu mustakabali wa tasnia ya filamu Tanzania na wasanii wake.


Chanzo; filam central.
Asante!

Posted by bongofilmdatabase on 6:06 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for "HIVI RUGE MUTAHABA NI NANI?"

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign