MJUE OUSAMANE SEMBENE- BABA WA FILAMU AFRIKA
nyota, slide 8:28 AM
Huyu anaitwa OUSMANE SEMBENE kutoka Senegal yeye ndiyo anaitwa baba wa Filamu Afrika. Filamu yake ya kwanza aliifanya miaka ya 60 alizaliwa munamo mwaka 1923 pale Casamance, kusini mwa nchini ya Senegal ambako baba yake mzazi aliahmia tu amabaye alikuwa ni mvuvi samaki kutoka Dakar, Ousmane Sembene ama mwite Sembene tu kama wachambuzi wa sanaa tunavyopendelea kumwita. Mzee huyu alivikwa taji la heshima kubwa sana la kuwa miongoni mwa waandishi wa kiafrika waliotoa ama kuandika makala na miswada mingi na mizuri ya filamu hapa barani afrika na hatimaye heshima hiyo akaambatanishwa na jina moja la ''BABA WA FILAMU ZA KIAFRIKA'' kabla haja maliza elimu yake a sekondari Sembene alifukuzwa shule mwaka 1936 kwa utovu wa nidhamu. mbali na kushindwa kumudu mazingira ya shule hakuweza kuungana na baba yake pia kumsaidia shughuli za uvuvi kwani alikuwa ni mwoga wa mawimbi ya maji kupita maelezo hivyo baba yake akachukuwa uamuzi wa kumpeleka kwa kwa nduguze huko Dakar mji mkuu mwa miji mikuu ya wafaransa hapo afrika maghribi.
Mwaka 1938 mpaka 1944 alifanya kazi kama fundi makanika ambaye aliyejifunzia pale pale kazini kwa maana ya kutokuwa na elimu ya fani hiyo, Sembene alijijengea tabia na kuipenda tabia hiyo ya usomaji vitabu vya aina ya Comics na vitabu vile vilivyo elezea filamu bora kwenye majumba ya sinema pale Dakar. hivyo Sembene aliteuwa kufanya kazi kwa muda wa wote wa mchana ama saa chache tu na muda mwingine alikwenda kusoma vitabua ,kutizama filamu na kukuaa kijiweni na marafiki aliokuwa akiishi nao pale mtaani kwa lengo la kusimiana hadithi, kucheza michezo ile ya jioni watoto na vijana wadogo hupenda kucheza na mambo mengine ya kitamaduni yaliyo julikana kwa jina la Senegalese cultural events kama raiya wa ufaransa kutoka na sehemu aliyokuwa akiishi. kwenye miaka ya 1944 kama wengi ya vijana afrika kwenye rika lake akaitwa kwenye jukumu la kuikomboa ufaransa toka kwa maguvu ya Ujerumani ambao ulitoka na kuelekea viunga vyake huko Niger. mara baada ya kurejea Dakar kwenye mwaka 1946. baada ya hapo Sembene aliishi na maisha ya kisiasa zaidi.
.