WATU WAZIMIA KWENYE UTAYARISHAJI FILAMU YA RAULA
Posted by bongofilmdatabase
mpya,
slide,
udaku
7:30 AM
|
Nyota wa
filamu wa kike nchini Chuchu Hansi alijikuta akiangua kilio kizito baada
ya kuingizwa kwenye jeneza katika ujio wa filamu mpya ya Raula.Katika
filamu hiyo Chuchu ilimbidi aigize kama mtu aliyekufa na kuagwa kwenye jeneza wakati akiandaliwa kwenda
kuzikwa. Kasheshe
ikaja pale alipolala kwenye jeneza, baada na watu kuja kuga mwili wake, ndipo mwanaye kipenzi Faria
ambaye ameigiza kama Star wa movie hiyo na ndiye Raula mwenyewe, alipopita karibu na jeneza hilo huku akilia
kwa uchungu.Raula alilia
kwa hisia kali huku akiita mama!! Mama!!, na kung’ang’amia jemeza huku
akitiririkwa na machozi. Hisia kali
zilipenya maskioni mwa mama yake na kujikuta akiangau kilio kikubwa na
kushindwa kutoka kwenye jeneza hadi aliponyanyuliwa msobemsobe, ili kujaribu kumweka katika hali
ya utulivu. Lakini
tofauti na watu walivyodhani, kwani hali hiyo iliendelea takribani nusu saa
kabla ya kukaa sawa na kurudi tena katika hali yake ya kawaida. Si kwa
chuchu Hansi ambaye mauzauza yalimkuta ila
mwigizaji mwingine, alikutwa na mkasa wa ajabu na kupoteza fahamu papo
hapo wakati akiaga maiti hai ya Chuchu Hansi. Mwigizaji
huyo alipita eneo la karibu na jeneza la Chuchu, akiigiza kulia lakini ghafla
aliregea na kudondoka chini, hali
iliyopelekea watu kwenda kumuokota na kumweka vizuri.
Tofauti
ilivyokuwa kwa Chuchu, kwani mwanamama huyo alipooza kabisa fahamu na kupata
tabu katika upumuaji.
|
|
(Kazi ilianza kama masihala)
Ilimbidi
kumchukua na kuandaa chumba maalum kwaajili ya kuweka waliozidiwa, ili kumrudisha katika hali yake ya kawaida. Ilimchukuwa
zaidi ya dakika 45 katika kuzinduka na kuwa katika hali ya kawaida huku maombi
makali yakipigwa katika kuhakikisha anarudi kuwa sawa. Mauzauza hayakuishia hapo, hadi kwa mwigizaji maarufu
na mkongwe Rachel ambaye alishaigiza filamu nyingi za kulia, lakini hapo
alijikuta akizidiwa kiasi cha kulia mpaka kupata maumivu makali ya kichwa. Naye ilibidi achukuliwa haraka na kupelekwa
kwenye chumba maalum kwaajili ya kupata huduma, kwani alikuwa akilalama kwamba
hali yake sio nzuri kabisa, kutokana na maumivu ya kichwa. |
|
(Chuchu akiwekwa kwenye jeneza huku akicheka)
Hali
hiyoilitokana na Rachel kuwa miongoni mwa watu waliyopita katika kuaga maiti
hai ya Chuchu.
Mambo
hayakuwa mazuri kwa waigizaji takribani wote, ila msanii Shemsa Salum alisema igizo hilo lilimkumbusha
kifo cha mdogo wake mpendwa. Maswali mengi
watu wakajiuliza pamoja na wasanii wenyewe, kwamba nini kilipelekea hisia kuwa kali mpaka
kuwashinda, wakati walishaigiza mara nyingi? |
|
(Hapa akiwekwa vizuri)
Je! Kulikuwa
na nguvu za ziada katika part hiyo, maana inasadikiwa Chuchu alipandisha
mashetani.
Pili huenda Chuchu
Hansi watu wanampenda sana kiasi cha kushikwa na hisia kalian a kufananisha
siku ambayo itakuja kuwa kweli? Chuchu Hansi
naye alisema anafikiria jinsi mwanaye alivyomlilia, je siku akitoweka kweli ni
je atamlilia kama hivyo, jambo ambalo lilimuongezea uchungu. Wakati
mwogozaji wa filamu hiyo Single Mtambalike almaarufu kama Richie rich, alisema uigizaji
huo, siku zote unakuwa ngumu sana mtu kuingia kwenye jeneza lakini Chuchu na
Msuya waliweza. Seleman
Barafu naye alisema haikuwahi kutokea tukio kama hilo, kubwa na lakushangaza. Mimi na wewe
wote tungoje kuona ujio wa filamu hiyo kuona nini cha ziadi kilichoteka hisia za waigizaji maarufu
kulia hadi kupoteza fahamu. |
|
Chuchu akiwa amelala kwenye jeneza,kabla ya kuwekwa pamba |
|
Tayari msaraba wake ukiwa tayari pamoja na picha yake. |
|
Tayari akiwa ameshawekwa pamba na watu wakipita kwaajili ya kuomboleza kwa kuaga. |
|
Kilio sasa kilizidi maradufu |
|
Ikafika zamu ya
familia yake ambayo aligiza nayo na ndiyo ilikuwa familia yake ukweli,
Esha Muheti,akiwa na mwanye Faria 'Raula' |
|
Mtoto alilia mpaka akawa mwekunduuu, sauti yake ikapenya kwa mama yake hasa. |
|
Ndani ya Jeneza alijikaza kidogo,lakini baada ya kuisha kwa ibada ghafla kilio kikashuka kikubwa. |
|
Hapa akiinuliwa na kupelekwa ndani baada ya kuona mambo si mazuri sana |
|
Libert akijaribu kumsaidia katika kumpa huduma ya kwanza. |
|
Huyu nayealiliampaka akaanza kulegea na hatmaye kuanguka, watu wakajitoa kwenda kumpokea. |
|
Alilazwa pembeni kwaajili ya kupata upepo lakini mambo yalikuwa bado. |
|
Akabebwa huku na kulekisha akapelekwa kwenye chumba kwaajili ya mapumziko.
|
|
Wakati huo huo Rachel naye alizidikulia ingawa igizo lilisimamishwa, hadi kichwa kikaanza kumuuma. |
|
Hatrmaye ikaandaaliwa chumba kwaajili ya kuwekwa wagonjwa. |
|
Ikabidi kutumika nguvu za ziada katika maombi. |
|
Shemsa akilia kwa uchungu ingawa igizo liliisha. |
|
Hii ilikuwa Part nyingine ya ambaye ilibidi azikwe kabulini. |
|
|
|
|
|
|
John ilibidi kwanza kuaga, alikuwa muoga kulikokawaida. |
|
Aliingia kwenye jeneza huku masharti kibao. |
|
Akawekewa pamba, ilifunikwe. |
|
Wee!! dakika mbili nyingi akainuka, |
|
Familia yake ilikuwa imeshika picha, walikuwa wakimwangalia jinsi alivyokuwa hatulii. |
|
Watu makabulini wakaendelea kutizama jinsi filamu inavyoenda |
|
Kila kitu kilikuwa tayari bado kufukiwa. |
|
Add caption |
|
Watu wakamrudisha ndani. |
|
wakamweka sawa kwaajili ya kumfunika.
|
Hapa akitumbukizwa kwenye kabuli... kwa picha zaidi BOFYA HAPO CHINI ( Kwenye Comment)
|
Huyu anaitwa Boom man, kila mtu anakazi yake kwenye filamu anaitwa Salum Shaban
Hapa kilammoja alikuwa amemshika mwanaye wa ukweli, namaanisha mwanaye wa kuzaa na sio film kama mlivyozoea.
Watu walijua kulia..
Wanamwita Koba matephone, hapa akiwa na simu karibu kumi lakini zote za watu,pembeni ni Hammada Script Writer
jamani pozi hilo
Wanamwita Libert akiwa na kimwana nddani ya pozi
Hammada naye ni muhimu sana ila haonekani, ni Script Write wa filamu hiyo.
Saidi yeye mwenyewe anajiita kama kiraka
Barafu akiwa na mchungaji Mafuvu na Shamsa
Hii ilikuwa bendi ya kwaya, ilikuja maalum kwaajili ya kuzika na kuimba
Nani alikuambia kuchukua video rahisi, hapa Richie akiwa na Kabuti Onyango
Koba akipewa mkate na Shamsa
Hawa ni watu muhimu lakini hawaonekani sana ni Cameraman Kabuti
Barafu akihusika kama ndugu wa marehemu
Watu walijua kulia
Mwisho kabisa kutana na mimi mwenyewe, hapa nikiwa kwenye pozi
lakusafiri kutoka nyumbani kwa marehemu kwenda makabuli. Tukamzima
kweli. CHANZO CHA HABARI HII NI BONGO UNIT | | | | | | |
Posted by bongofilmdatabase
on 7:30 AM.
Filed under
mpya,
slide,
udaku
.
You can follow any responses to this entry through the
RSS 2.0