MKONO MWINGINE WA UPANGAJI PICHA ZA MAKASHA YA FILAMU
kinyemi, mpya, slide, udaku 1:24 PM
Katika pita pita tumekutana na kava moja matata sana inayoashiria ni Movie ya kibongo iitwayo A LONDON GIRL! Moja kwa moja kutokana na ubunifu mzuri wa kava ya filamu hiyo tukapata jibu kuwa hii kitu ikiingia street lazima iuze.
Kava hiyo imetengenezwa na kampuni changa ya Kibongo iitwayo I-Dentity Designs. Kwa kutaka kujua zaidi kuhusiana na movie hiyo ambayo kava lake linaashiria kuwa ni high-budget movie kibongobongo tukaipigia simu kampuni hiyo kutaka kujua zaidi kuhusiana na project hiyo.
Hata hivyo taarifa ya mbunifu wa kazi hiyo ikatuambia kuwa kumbe amedesign tu kama sample ili kuonesha uwezo wake. Hakika ni kwamba kama kweli kukiwa na idea ya movie kama hii Bongo tunahisi itafanya vizuri sana hasa kama story ikiwa kwa mfano msichana huyo wa London labda kaja Bongo na kukimbiza sana kitaa then kunakuwa na story ya mapenzi inayomzunguka binti huyu.
Ama inaweza kuwa mbongo ameenda London na akakutana na msichana mrembo wa London ambaye anajikuta akimzimia kinomanoma! Sounds like a catchy synopsis right?
Chanzo;Leotainment