''VITU SABA DIRECTOR WA FILAMU ANAPASWA KUZINGATIA''.

DIRECTOR WA FILAMU

Tunapoongelea Mwongozaji(Director) katika filamu moja kwa moja tunamuangalia mtu ambaye ndiyo nguzo ya msingi sana katika uzalishaji (production) yoyote ile ya filamu.na leo katika jicho langu tunamuangalia mtu huyu katika misingi mikuu mitatu.

1. Director ni nani?
2. sifa za director.
3. Anaumuhimu gani katika filamu?

Director
ni mtu aneyeongoza jopo zima litengenezalo filamu kuanzia mwanzo wa production hadi mwisho,ambapo anatakiwa kukodi watu wa kufanya nae kazi,nikiwa na maana ya crew nzima ya production kuanzia mpiga picha na wengine wote ili aweze kufanya kazi na watu aliowazoea na wenye ufanisi anaoupenda yeye,hii si lazima sana lakini ni vizuri ili kuweza kuchangia kupata kazi nzuri itakayovutia machoni kwa mtazamaji.












Director kama director anatakiwa awe na jicho linaloona mbali (vision eye),yaani awe na uwezo wa kuona mbele zaidi ya mtu yoyote katika production,busara pia ni jambo la msingi sana katika kutoa uamuzi wowote,katika pita pita yangu nimewahi kuongea na baadhi ya wasanii juu ya tabia za ma director wetu wa hapa Tanzania wengi sana wameongelea upande wa pili wa ma director kuwa wanakosa busara katika production na imefikia wakati wanapiga makofi actors/actress kipindi cha shooting kiasi cha kuwapotezea mood,kwa hali hii director anatakiwa awe na busara za kutosha,sifa nyingine ya director ni elimu ya kutosha katika suala zima la filamu yaani aina ya shots,angles,lights na ujuzi wote wa uzalishaji wa filamu kwa ujumla,vile vile awe na uwezo wa kuongoza watu au kundi la watu katika Nyanja ya filamu na maisha kwa ujumla kipindi chote cha utengenezaji wa filamu.









Director ni mtu wa muhimu sana katika filamu kwa sababu anaongoza crew nzima kuanzia uchambuaji wa mswada,kuchagua waigizaji na crew nzima ya filamu,pia anajukumu kubwa katika kubadilisha mswada na kuwa vitendo vinavyokuja kuzaa filamu yenyewe,ana jukumu la kusimamia mazoezi (rehersals) kabla ya kurekodi ambapo baadhi ya directors wanafanya mazoezi kabla ya kurekodi matukio (scene) pindi wanapokuwa eneo la kurekoia (location), hili ni jambo la msingi kwa sababu linaonyesha jinsi tukio (scene) itakavyorekodiwa na kama kuna marekebisho yoyote ni rahisi kufanyia kazi,mbali na hilo pia director anajukumu la kusimamia movements na blocking,director anajukumu kubla kipindi cha ukataji (editing)wa filamu ili kuhakikisha hisia na shots zote zimezingatiwa na vilevile anaweza kuongeza mchango katika rangi ya picha inayotakiwa kutumika katika filamu,na upande wa mziki (sound track) unaotumiwa kwenye filamu.

Director siku zote hafanyi kazi peke yake ni lazima ashirikiane na watu wengine katika production (Key collaborators),hivyo basi anafanya kazi na watu wafuatao:
-Msaidizi wa director(AD)
Anafanya kazi na director kama msaidizi wake katika
-Director of photography (DP)
ambaye ni msimamizi wa mambo yote ya picha mara nyingine anaweza kuwa ndiyo mpiga picha au watu wawili tofauti.















-Art Director,
huyu ni msimamizi wa taswira na jinsi zinavyowakilisha au kufikisha ujumbe,yeye anachagua taswira zinazoweza kuamsha moods,na artistic style zinazotakiwa kutumika ili kufikisha ujumbe kwa mtazamaji.
-Kuna crew ya production designers ambao wanafanya kazi kwa karibu sana na director kama vile Costume designer ambaye kazi yake kubwa ni ku design au kuchagua nguo gani anayotakiwa kuvaa msanii (character) kwa muda na wakati gani,lakini pia inajumuisha mambo kama mask kama inahitajika kwa mfano filamu kama ya superman.



-Lighting designer: (LD)
Kazi yake kubwa huyu ni kuhakikisha taa zinafungwa kutokana na moods na kitu kinachotakiwa kuonekana hii inategemeana sana na aina ya filamu yenyewe,kwa hiyo anatakiwa kusoma mswada na kuuelewa ipasavyo ili ajie ni jinsi gani ata za set kwa kila tukio (scene) hata kama ni mchana wakiwa nje pana weza kuwa na uhitaji wa kivuli au hapana hivyo uhitaji wa reflector unaweza ukatokea. katika kazi yoyote ya filamu LD anafanya kazi bega kwa bega na set designer, costume designer, sound designer choreographer kama kuna sehemu kwenye filamu kunahitaji choreography na director ambaye ndiyo msimamizi wa wote,lakini pia anafanya kazi kwa karibu sana na location manager ili aweze kuona kama sehemu hiyo ni sahihi kutokana na mood ya filamu yenyewe.




Sound Designer(Director of Audiography ) Ni mtu anayehusika katika kusimamia suala zima la kutengeneza sauti kuanzia katika kurekodi na vile vile kutengeneza sound effects zinazotumika kwenye filamu,anatakiwa pia kujua stori inayorekodiwa ili kuweza kuelewa nini afanye,anafanya kazi karibu sana na Boom Operator.
Kwa ujumla director ana vitu saba vya kuzingatia katika production
• Kuchambua mswada
• Kuchagua wasaidizi wake katika kazi ( key collaborators)
• Kutoa mtazamo wake kautokana na story
• Kutoa mtazamo wake katika picha na sauti
• Kuchagua characters( casting roles)
• Kufanya mazoezi ya mchezo( rehearsaling the production)
• Kuwa na busara katika maamuzi.
Katika jicho langu leo tumemuangalia director ambaye ni nguzo ya muhimu kwenye production yoyote ya filamu.

ALRIGHT STUDENTIIIIIIIII NASIKIA KENGELE INAGONGA SASA. MPAKA SIKU NYINGINE TENA, NI MIMI KIRAJA WENU KUU WA DARASA LA LEO. na KAMA UTAKUWA NA MASWALI KWA SOMO LA LEO USISITE KUNIANDIKIA KWENYE EMAIL YETU (bongofilm@hotmail.com) AU YAACHE HAPO CHINI KWENYE COMMENTS BOX YETU NA WENGINE WAPATE KUYAONA PIA NA MAJIBU YATATOKA KABLA YA DARASA LIJALO...

Posted by Bongo Film Data Base on 3:23 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

1 comments for ''VITU SABA DIRECTOR WA FILAMU ANAPASWA KUZINGATIA''.

  1. HADHIMA YETU SISI NI KUIKOMBOA TASNIA HII YA FILAMU HAPA TANZANIA KWA NAMNA MOJA HADI NYINGINE,NA ELIMU HUPATIKANA SEHEMU YEYOTE ILE PALIPO NA UTARATIBU MZURI NA MAELEWANO PIA WASANI NA WADAU WENZANGU HUYU HAPA MKOMBOZI WETU SASA...KARIBUNI NYOTE NDANI YA DARASA HII

    .....ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA,SASA WAKOLONI WAMEBADILISHA KUFULI....

    NDUGU ZANGU SANAA BILA YA TAALUMA YAKE HATUTA FIKA TUNAKO KUOTA KILA KUKICHA NA KUPASEMA KATIKA MAHOJIANO YETU KWENYE VYOMBO VYA HABARI(interviews)

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign