''CHANGA LA MACHO LA NAMNA HII TASNIA YETU HAITA VUKA MIPAKA''


Enzi zile nikirejea miaka kama saba huko nyuma nilipendezwa sana na kutazama filamu za ughaibuni hasahasa bara la Asia,nchi za India na Japani sio kwamba ni kwa kuwa nilikuwa naelewa lugha hiyo hapana wala nilikuwa sielewi ila uwepo wa filamu zao kwa wingi ndio ilikuwa chachu,hizi zikuwa filamu za mapigano makali sana. Uwezo wa kununua mkanda mmoja unaoisha ladha yake baada ya masaa kadhaa haukuwepo na hata kama ulikuwepo tulipendelea sana kuazima. Nilikuwa sielewi maana ya `synopsis` kwamba ni ufupisho wa kitakachoonekana ndani na hata kama ningejua bado lugha ilikuwa tatizo kubwa sana kuna wakati iliandikwa kichina au kihindi kama sio kijapani. Ili kuujua ubora wa filamu husika tulitazama kava lake,kama kava lilikuwa linavutia basi na sisi tuliazima filamu hiyo. Na kwa hakika mbinu hiyo tuliyotumia ilikuwa inazaa matunda kwani kama kava limewekwa picha ya Jetli ameshika panga basi na ndani ilikuwa vilevile na kama ni mtu anapigwa ngumi damu emetapaka chini na ndani alikuwa anaonekana akipigwa ngumi vilevile kwa nyoka kama ni mkubwa na ndani ataonekana mkubwa na ingekuwa ni kichekesho kama kava linaonesha kunguru halafu simulizi ya ndani iwe ya paka. Mifano halisi(anakonda
)
Nyoka mkubwa kiasi hicho ataonekana ndni ya filamu.
Enzi hizo kiwanda cha filamu bongo hakikua kimetanuka kama ilivyo sasa,hivyo mara nyingi wasanii wetu tuliwatazama kupitia maigizo/michezo ya kwenye luninga kama vile Mambo hao,Maisha na Kidedea huku kwa nchi jirani ya Kenya wakitesa na tamthiliya ya Tausi.
Mabadiliko makubwa ndani ya miaka michache yaliyoletwa na wanaharakati kadhaa hatimaye yakazihamisha akili zetu katika kuhangaikia madukani kutafuta filamu zilizochezwa hapa Bongo. Mazoea hujenga tabia kama tulivyozoea kwa filamu za uchina uhindini na kwingineko kwamba kilichopo kwenye kava kinasadifu yaliyomo ndani basi kasumba hiyo tukaihamishia katika filamu za bongo. Mwanzoni hali ilikuwa shwari lakini kwa sasa ni uozo mtupu. Enzi zile King Majuto na filamu yake vichekesho Mjini Shule akiwa na mkali mwenzake wa enzi hizo Mzee Small,hakika kilichokuwepo kwenye kava ndani kilikuwepo,hivyo hivyo kwa filamu ya AUGUA iliyotamba na kuwatangaza wanafunzi wahitimu wa Bagamoyo. Nachelea kusema kwamba kwa miaka ile muhusika rasmi wa kunakshi kava la filamu alikuwa anapitia simulizi nzima halafu anashauriana na wahusika wa hiyo filamu ni vipi kava lionekane na kusadifu yaliyo ndani.



Kuanzia mwaka 2008 hadi sasa,ubunifu katika upande wa makava umepungua kama si kutoweka kabisa,nadhani hata wasanii wenyewe wamegundua kwamba watanzania ni walevi wa makava ya filamu zao wanazocheza hivyo kwa kadri kava linavyokuwa bora na mauzo ya filamu hupanda juu zaidi hata kama kazi ndani ni bomu. Na jambo kubwa zaidi ni uwepo wa sura ya staa yeyote katika kava. Sipingi ubunifu huo kwamba ni biashara ama mbinu ya kuvuta wateja lakini je? Ukitulaghai leo watanzania kwa kava lako zuri halafu ndani kazi mbaya,kesho utamlaghai nani kwa kazi yako hiyo mpya?? Hivyo jambo hili linampa msanii kazi ngumu sana ya kufikiria ni vipi atunge uongo wa kuteka soko badala ya kutunga filamu bora.
Mifano halisi katika kipindi cha miezi sita iliyopita imeegemea pande zote lakini kwanza ni upande wa filamu za vichekesho ambazo naweza kusema kwa ujasiri kwamba zinasadikiwa kuwa nyepesi sana katika utayarishaji yake yaani “PRODUCTION” na hivyo hivyo katika malipo ni wasanii hao wa vichekesho (komedi) ambao hulipwa kiduchu sana. Nilipata nafasi ya kupitia makava takribani kumi na tano ya filamu hizi za vichekesho,hakika yalikuwa yananivunja mbavu zangu hasahasa kutokana na sura za hao wachekeshaji (komedians) kuwa za kuchekesha hata kabla sijaangalia ndani kuna nini,lakini jambo lililokuja kunishangaza ni kwamba kati ya makava hayo,matano kati yao yalinifanya niyatenge pembeni na kulazimika kuiwasha deki yangu na kuanza kupitia moja baada ya mwingine. Kilichofanya nifikie hatua hiyo ni ile hali ya msanii maarufu anayetikisa katika vichekesho,maarufu kwa jina la MBOTO ,DIFENDA,ZIMWI na wengine wengi tu kuwa wameonekana katika kava zaidi ya mbili akiwa katika muonekano unaofanana,ama kwa hakika nilishangaa sana kwani ndani ya hizo filamu ni moja tu alionekana akiwa vile hivyo walichofanya wale wengine ni kuichukua ile picha na kuanza kuipachika katika hizo kava nyingine,jamani uzembe kiasi gani huu.

Tizama hii kitu hapa;;

(ZIMWI)huyo hapo juu amejirudia makadha wa kadha kwenye kava tofauti tofauti.

(DIFENDA)huyo pia amejirudia makadha wa kadha kwenye kava tofauti tofauti.


Hao hapo juu ni wachekeshaji maarufu ambao picha zao zimejirudi kwenye kava kadha kama inavyoonekana na nyingi zipo mitaani mwetu…
Uozo huu ulinipelekea kuhamia katika filamu za `serious` huku nikiwatetea hawa waandaaji wa komedi kwa hoja hafifu kwamba wana kipato hafifu sana.
Jiwe langu nalitupa kwa wasanii ambao kama wewe ukilia mtaji yeye anao tena wa kutosha. Lakini kitu cha kushangaza bado na wao hawatutendei haki kabisa wateja wao. Mimi naamini kwamba iwapo sisi hatupo basi kazi zao hazina maana hata kidogo,kama ni hivyo basi wanatakiwa kutupa heshima yetu japo kidogo. Lakini ni malipo gani haya mnatupatia kwa kutudanganya na makava mazuri huku ndani pakiwa hakuna lolote jipya na la maana. Moja kwa moja kwa kaka Vicent Kigosi “Ray” hivi kaka unaelewa ni kiasi gani kava la filamu yako ya ‘HANDSOME WA KIJIJI’

lilivyoweza kukuongezea mashabiki halafu wakakushushia heshima baadaye???
Kwa kweli inashangaza sana baadaye unacheka mwishoe unakwazika. Ubunifu uliotumika kulitengeneza kava la filamu ya Handsome wa Kjiji siwezi kusema ulikuwa wa hali ya juu,maana haukuendana na jina la filamu hiyo,maana pale kwenye kava walionekana mabinti wakiwa wamemzunguka mfalme wao tofauti na jina la Handsome wa Kijiji,hilo nalimezea mate huenda kaka Ray hadi sasa anaamini vijijini kuna watu wanavaa vile japo sijazunguka sana je ni kijiji gani Tanzania hii?? Haya hata kama kipo hicho kijiji je ndani ya filamu hiyo Mandhari hayo yameonekana?? Jibu ni jepesi sana kama umepata fursa ya kuitizama hii filamu HAPANA!!!. Sasa kama hakuna location hiyo kwanini tudanganywe na kukimbia madukani kujiwahia kupata kopi zetu tumwone Ray amevaa kimila!!! Hadi sasa sijapata mantiki yoyote juu ya hili.
Si kwamba ni Ray na filamu yake ya HANDSOME WA KIJIJI pekee bali ni wengi sana hutengeneza makava ya kupendeza halafu upuuzi mtupu ndani yake,kama ningekuwa na nyundo ya kutoa hukumu juu ya kesi hii basi bila aibu basi ningewaacha huru wasanii na badala yake ningekabana koo na waandaaji,ambao kwa ushauri wangu ningeshauri afadhali kama wangekuwa wanatengeneza kava kwa kutumia vipande (scenes) husika katika filamu husika. Tazama filamu ya FAMILY DISASTER anaonekana Lulu na mwenzake wakinyonya pipi Kijiti yaani Lol pop lakini ndani ya picha hata jojo hawakutafuna.


Chondechonde hebu tuheshimuni mashabiki wenu. Ubora wa kazi zenu ndio furaha yetu,filamu za ufilipino zinakuja juu,halahala tutahamishia macho yetu huko huku sanaa ya ndani tukiipa kisogo. Siwatishi hata kidogo na wala sina lengo baya lakini hata soka la bongo wadau walikimbia taratibu baada ya longolongo kuzidi,uko wapi ushabiki wa mpira bongo!? Naamini mtatafakari na kuchukua hatua upesi.
kutoka dawati letu habari hatuna la ziada mpaka hapo ila team yetu imeangazia kwa baadhi ya wasani hao tu kwa ukaribu wa aina yake na tuna draft kubwa ya kazi nyingi za wasanii zenye kuonesha vitu kama hivyo vinavyo didimiza tasnia yetu hii inayokuwa kwa kasi kila kunapokucha na kutoa ajira kwa vijana wengi kwa sasa hapa Tanzania....

Posted by Bongo Film Data Base on 8:23 PM. Filed under , , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

6 comments for ''CHANGA LA MACHO LA NAMNA HII TASNIA YETU HAITA VUKA MIPAKA''

  1. JUKWA LA BONGO FILM DATA BASE SASA LIPO WAZI KUPOKEA MCHANGO WAKO...karibuni wadau

  2. I appreciate the work of revealing the truth to the concerned, ni bora kumwambia mtu ukweli ili aufahamu hata kama utamuuma, ili ukweli huo umsaidie baadae. Hakuna msanii asiyependa kazi yake iwe na mauzo mawili, lakini kumbukeni, ukinidanganya leo na kazi ya uongo, kesho ukifanya kazi ya maana, sitajishughulisha nayo kwa sababu, ulinidanganya mwanzo.. NOTE; FIRST IMPRESSION IS THE BEST IMPRESSION IF IT'S NOT A LIE.......

  3. Eeeebana nakubaliana nawe 100%, sijui kama hata namna ya kuweka makasha ye2 ime2shinda. Anyway, vijana 2changamke kuweza okoa jahaz hil la sanaa tz

  4. Pesa zilizotawaliwa na njaa nyingi ndiyo chanzo cha yote haya wala si kitu kingine kwa wasanii wetu hasa hawa wachekeshaji na ukilinganisha pesa wanayopewa pia inakuwa ni kidogo sana na mliki wa kazi hizo wanazo cheza...

    kingine hawa wasanii wetu wa tanzania mara nyingi huitwa kucheza filamu tu kama ni matukio ni mawili au moja na kwenye suala zima la kava hawahusishi kabisa, hivyo mwenye filamu anachokifanya kuepuka gharama ni kuchukuwa picha iliyotumika kwenye filamu iliyopita na kupachika kwenye kava jipya...

  5. sasa hapo ndipo 2napoua fani hii, kama mwenye filam anaona ni bora aokoe gharama ndogo 2 ya kava, duh? ni hatar kwelkwel,,,,labda elimu itasaidia,,japo sidhan kwa hao wakongwe,,,mayb cc vijana twaweza badilika

  6. Elimu itasaidia endapo watahudhulia darasani kama sanaa inavyo takiwa iwe kwa dunia ya sasa ukiachilia mbali kipaji walichopewa na Mwenyezi. lakini kama hata kwenda tu kwenye hivyo vyuo vidogo hawaendi kuhofia kushuka kwa chati majina yao ambayo hu jengwa kila mwezi kwa msukumo wa soko litakalo filamu kila tarehe moja ya mwezi kama sio kila wiki kama tuonavyo sasa sidhani kama mabadiliko haya yataonekana hapa...kuhusu gharama wanazo ziepuka iko wazi ndiyo chanzo cha yote haya.

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign