MASTAA WA FILAMU BONGO NA UMASKINI WAO KATIKA KUTAFUTA LOCATION!!


Hongera na pongezi nyingi ziwaendee Kanumba great na RJ film production company chini ya usimamizi wa Steven Kanumba na Vicent Kigosi pamoja na Blandina Chagula kwa kuiwezesha tasnia ya filamu nchini kuwa ajira kwa rika zote kwa filamu zao zinazotoka mfululizo takribani kila mwezi. Kwa sasa Steven Kanumba anatesa mtaani na filamu yake ya Devil Kingdom ambayo kwa kiingereza changu kidogo nilifikiria kwamba ilikuwa ni sahihi kuitwa DEVIL`S KINGDOM lakini hilo si tatizo naamini nilichomaanisha mimi na yeye akishirikiana na mkali kutoka Nigeria Ramsey Nouah kuziburuza scene zilizowagharimu masaa mawili kamili. Huyo alikuwa ni Steven Kanumba lakini na yeye Ray na kampuni yake ya RJ hawakuwa nyuma baada ya kumaliza filamu ya What is it sasa yupo jikoni tena kupakua filamu yake ya Unpredictable yaani isiyotabilika.


Kilichonishangaza mimi na wengine ambao wameufatilia huu ugonjwa unaowasumbua wasanii wetu wakubwa wanaweza kuniunga mkono. Steven Kanumba na Ray sina shaka kwamba tasnia hii ya filamu imewalipa sana pia imebadili maisha yao kwa hali kubwa sana,nachelea kusema kwamba wawili hawa wana uwezo wa kufanya filamu zao mahali popote pale nchini na hata nchi za jirani,lakini tatizo lililonishangaza ni umaskini wa fikra zao ama uzembe katika kuzisumbua akili zao kuhusu mandhari ambapo filamu zao zinapotakiwa kufanyika,sijui nani wa kulaumiwa katika hili je? ni location manager ama ni kujivika madaraka mengi kwa mtu mmoja?
Katika filamu hii mpya ya Devil Kingdom,madhari ambayo ameyatumia Kanumba ikiwa ni takribani wiki tatu tangu iingie sokoni yakiwa hata hayajatoka katika akili zetu huku wakazi wa mbali hasahasa vijijini wakiwa hawajui wataiona lini,madhari yale yale yametumiwa na ndugu yetu Vicent Kigosi katika filamu yake ya UNPREDICTABLE. Binafsi si mara ya kwanza kushuhudia uvundo huu wa kutumia location moja katika filamu zaidi ya moja,jambo hili lilionekana pia katika filamu za THE LOST ADAM na THE SHOCK katika eneo la Benjamin Mkapa Trade Zone,juu ya mfano wa nakshi za mlima Kilimanjaro.
Sijapata jibu sahihi hadi sasa kama waigizaji wetu wametudharau watazamaji wao na kutuona mambumbumbu tusiokuwa na kumbukumbu ya tulichokiona jana??? ama ni uzembe wao katika kutafuta location kama hilo ni tatizo mimi nashauri kwamba wawepo watu maalum kwa ajiri ya kutafuta location ili mambo yakienda ndivyo sivyo tujue nani wa kulaumiwa lakini bila kujua hilo mimi nasema huu ni utajiri wa pesa wa mastaa wetu na UMASKINI katika kutafuta location.

Na hizi picha hapo chini ni location iliyoanza kutumika kwenye kazi ya kanumba kisha kwenye kazi ya Ray.

Tizama location hii iliyotumika hapo juu kwenye kazi ya kanumba ambayo hata mwezi huja timia kabisa na ndiyo inajirudia hivyo kwenye kazi hii ya Ray hapa iliyopo jikoni ikitengenezwa kwasasa.

Na kwa kumalizia kabisa tizama nakshi zilizopo hapo juu ya meza hiyo ya chakula kwenye filamu hizi zote.
SASA MDAU MWENZANGU KAMA NDO WIVU WA NAMNA HII TUITE NI WAKIMANDELEO??????? AU NDO TUNA ZIDI KUTOKOMEZA TASNIA YETU YA FILAMU!!!
NIANDIKIE MCHANGO WAKO HAPO KWENYE KISANDUKU CHA MAONI KWA CHINI KIDOGO KAMA KUNA HAJA KUSUBIRI KUANGALIA HIYO KAZI MPYA YA VICENT KIGOSI a.k.a RAY KUONA KITU TOFAUTI NA KIPYA???????????/ TUKIACHILIA MBALI SEHEMU ZA STAREHE KAMA LAMADA NA NYUMBA ZETU WENYEWE ZA MTAANI??!!

Posted by Bongo Film Data Base on 9:48 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

8 comments for MASTAA WA FILAMU BONGO NA UMASKINI WAO KATIKA KUTAFUTA LOCATION!!

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign