MIAKA HAMSINI YA UHURU NA MASHUJA WETU KWENYE TASNIA YA FILAMU(MKWAWA)

Tumeshuhudi kwa macho wetu makavu kwenye viwanja mbalimbali kote bara na visiwani na hata kuona na kusikia kupitia vyombo vya habari tofauti tofauti  hapa nchini kwa taasisi, mshirika na makampuni ya kiserikali na yasiokuwa ya kiserikali  ya kisherekea na kujipongeza  matunda yanayo ambatana na  mafanikio waliyoyatimiza tangu tuupate uhuru wa bendera miaka hamsini iliyopita  mpaka sasa...

Taifa kwa taklibani  nyaja zake zote  imetoa hamasa ya kutosha sana kiasi cha kila sikio la mtanzania kusikia shangwe kutoka kila pembe ya ardhi ya hapa kwetu nchi zikiimba miaka hamsini ya uhuru wetu...siku hadi siku mmoja baada ya mwingine  tulipokezana wimbo huu unao pambwa  na kila aina ya mapambo kulingana  na kiwanja  cha washerehekeaji..

Kutoka katika tasnia ya filamu hapa nchini tanzania kupitia taasisi za kiserikali na zile za binafsi zimekuwa nyuma sana kupokea wimbo huu na kuueneza kama wenzao walivyofanya, kitu  ambacho hakikuwa  kizuri kabisa..kampuni moja binafsi kabisa imejitokeza na imeanda FILAMU inayo onesha sehemu ya maisha ya mmoja wa mashuja wetu ambao daima tutawakumbuka na kuwaenzi maisha yetu yote.

Kwa ufupi, CHIEF MKWAWA wa HEHE ambayo kwa sasa ndiyo panaitwa Iringa  ni mmoja  ya mashuja wetu hapa nchini Tanzania wa waliyo simamia mila na desturi zetu kabla ya ukoloni, MKWAWA alitawala himaya kubwa sana ambayo haikuwa na historia ya kushindwa mapigano ya aina  yoyote ile.. mnamo mwaka 1898 ngome  ya MKWAWA ilianguka dhidi ya majeshi ya kijerumani (GERMANY) kitu ambacho kimpelekea ajitoe uhai wake kuliko kutiwa nguvuni ama mikononi mwa utawala wa kijerumani (GERMANY)  akiwa hai.

Kutoka na historia ya utawala na ngome yake kuwa imara na  yenye nguvu isio pinduliwa na mtu yoyote na hata  wajerumani wenyewe kuliwatoka kijasho  kwa miaka mingi sana mpaka walipo kuja kulishinda jeshi la mfalme MKWAWA. mara baada kumwangusha Mfalme huyu moja kwa moja wachukuwa uamuzi wa kulisafirisha   fuvu la kichwa chake  na kulipeleka katika moja ya nyumba za kumbukumbu huko BREMEN nchini  UJERUMANI kama kumbukumbu yao muhimu toka katika mataifa waliyo ya tawala hapa Afrika kwa utata mkubwa mpaka kufikia  mwaka 1954 ambapo familia yake na  msaada wa serikali ya Tanzania kulirejesha fuvu lake hapa nchi.

Sehemu ya maisha ya MKWAWA yanayosimuliwa kwa namna yake ya kipekee katika picha nyogofu zimetumika kwa maana ya picha zinazotembea (filamu) ipo tayari kuwafika watanzania wote na ulimwengu wote kwa ujumla hivi karibuni..


                                             ONA TRAILER YA FILAMU HII HAPO CHINI




Shukrani za dhati zilifikie jopo zima lilofanikisha filamu hii ya shujaa wetu hapa nchini Tanzania kama kuenzi Mfalme huyu na kuazimisha miaka hamsini ya uhuru na kitu cha kitofauti  kwenye tasnia ya filamu hapa kwetu, tumeupokea wimbo huu wa kusherehekea uhuru wetu na tunaupaza kwa taifa kwa namna hii . much respect to mkwawa filming crew.

Mdau wa Bongo Film DataBase kaa sambamba nasi kwa taarifa na habari nyingi kuhusu filamu hii ya kwanza ya kihistoria kwenye miaka hii ya karibuni tangu tasnia ya filamu toka Tanzania  kuanza kujichora katika ramani ya saana duniani. 

Posted by Bongo Film Data Base on 7:35 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MIAKA HAMSINI YA UHURU NA MASHUJA WETU KWENYE TASNIA YA FILAMU(MKWAWA)

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign