RAQEY ; HAKUNA JIPYA BONGO MOVIE
11:32 PM
KATIKA utayarishaji wa filamu kila tukio lina umuhimu wake, wakati tasnia ya filamu ikiendelea Bongo
kuna watu muhimu katika tasnia hii ambao ni wabunifu wa makava kwa ajili ya filamu zetu, lakini kumekuwa na tatizo moja tu la baadhi ya makava kufanana je sababu ni mtengenezaji mmoja?
kuna watu muhimu katika tasnia hii ambao ni wabunifu wa makava kwa ajili ya filamu zetu, lakini kumekuwa na tatizo moja tu la baadhi ya makava kufanana je sababu ni mtengenezaji mmoja?
Moja kwa moja FC ilinaongea na mbunifu mahiri wa makava ya filamu Bongo Raqey Mohamed kutoka kampuni ya I- View Media naye anafafanua zaidi kwa kusema, mara nyingi kabla ya kufanya kazi hiyo ya ubunifu wa makava hayo anatumia muda kwa kuongea na wahusika ili kujua mtiririko wa hadithi husika, jambo ambalo linampa wakati mgumu katika utayarishaji wa makava hayo,
“Awali kabla sijaanza kufanya kazi na wasanii wa filamu nilikuwa ninachukia sana kazi zao, nikawa nahitaji kuboresha katika ubunifu wa makava, kwani sehemu mojawapo inayoweza kumvutia mteja kabla ya kununua hata hiyo filamu yenyewe, filamu nyingi unakuta wasambazaji wanakuwa na mitazamo yao hasa kupenda lazima sura za watu fulani zionekane hata kama ushiriki wao ni kidogo,”
“Lakini baada ya kuingia na kufanya nao kazi, nimegundua mambo mengi kuna tatizo moja kubwa ambalo naliona katika filamu za Bongo kuwa na hadithi zile zile, mara nyingi wanajitahidi kubadili majina na wahusika, na mimi ninatengeneza cover kulingana na wazo la mtu mwenye filamu, sasa kila mtu akija akinisimulia hadithi kama ya mteja wa kwanza lazima ujue idea itaangukia sawa na mwingine,”anasema Raqey.
Aidha kuna wasanii wanapofika kwake umsimulia hadithi tofauti kabisa na filamu yenyewe ili tu waweze kukaa katika kava, pia anasema kuwa hata sera za wasambazaji zinachangia makava kufanana, kila kava linakuwa na wasanii watatu watatu kwake ni changamoto. Raqey alikuwa akijibu swali ambalo Aliulizwa na wasomaji wa ukurasa wa FC kuhusu kava la UNPREDICTABLE ya Ray na BECAUSE OF YOU ya Kanumba inakuwaje kuwa katika staili moja?.
SHUKURANI ZA KUTOSHA ZIFIKE KWA JOPO LA UKURASA WA FILAMU CENTRAL KWA HABARI HII.
Posted by Bongo Film Data Base
on 11:32 PM.
Filed under
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0