SERIKALI YATOA NEMBO YA KUZITAMBUA KAZI ZA WASANI SASA...
habari 11:47 PM
BODI ya ukaguzi wa filamu Tanzania kuanzia sasa itakuwa ikitokea alama ianyoonyesha kuwa filamu husika kuwa imekaguliwa na kupewa daraja husika, Wakiongea na FC mtendaji wa Bodi hiyo amesema kuwa alama hiyo ni muhimu sana kuonekana katika filamu yoyote inayoonyeshwa kwa jamii, na iwapo filamu itakosa alama hiyo basi ni filamu batili.
“Nembo ambayo bodi inatoa ni kwa ajili ya utambuzi, inatakiwa ionekane katika filamu inapoaanza mwanzo, na mwisho wa filamu inapoisha, lakini pia alama inatakiwa kuonekana juu ya kava la filamu husika jambo litamtambulisha mnunuzi na mtu mwingine kuwa filamu hiyo imekaguliwa na kupewa daraja,”anasema mtendaji huyo.
Baada filamu kukaguliwa upewa daraja na kupewa kibali cha mwaka mmoja kwa ajili ya kuingia sokoni, wengi wanasema faida ya ukaguzi ni kupata filamu zenye maadili mema, pamoja na kutambua uwepo wa tasnia hii ya filamu Tanzania.
Gharama za ukaguzi ambayo imewekwa na Serikali ni Tshs. 1,000/= kwa dk. Lakini kwa filamu zinazotengenezwa na wageni hutozwa kwa fedha za kigeni, ni fursa nyingine kwa watayarishaji kuweza kupeleka filamu zenu zikaguliwe, kwani filamu hizo nyingi zimetengenezwa kwa kukiuka sheria ya utengenezaji filamu.
Kabla ya kutengeneza filamu ni lazima mtayarishaji apeleke muswada kwa ajili ya ukaguzi, baada ya ukaguzi wa muswada hatua inayofuatia ni uombaji wa kibali kwa ajili ya kurekodi filamu husika ambacho gharama yake ni TShs. 500,000/= na baadae tena filamu inarudishwa kwa ajili ya kukaguliwa na kupewa daraja.
CHANZO CHA HABARI; FILAMU CENTRAL
Asante!