KUIMARISHA MWONEKANO WA WASANII WA KIKE HUCHUKUA SEHEMU KUBWA YA BAJETI YA MAPATO YETUMUIGIZAJI wa filamu anayefanya vizuri katika tasnia hiyo Latifa Idabu ‘Badra, anaamini kuwa uzuri kwa akina dada unachangia katika uigizaji ndio maana msanii wa kike anapoanza kufanya vizuri lazima awe mrembo kwa kiwango kikubwa, tofauti na fani nyingi ambazo unakuwa kazini lazima uwe katika hali
yoyote na watazamaji wanakuona kawaida tu bila hata kuwa na hofu au kuchukizwa na muonekano wako katika kazi hiyo.

Inasemekana sehemu kubwa ya Bajeti ya wasanii wengi kwa Bongo inaingia katika mavazi na vipodozi ikiwa na ukodishaji wa magari, kwani moja ya kishawishi kwa mtayarishaji ni msanii mwenye uwezo kimavazi kwa kila kipande (Scene) anachoshiriki katika filamu husika, hali hii inatokana na hali ya bajeti wakati wa uaandaaji kuwa finyu, jambo linalofanya mtayarishaji kumhitaji msanii mwenye mavazi ya kutosha.“Msanii bwana lazima uwe mrembo, kuanzia mavazi yako na muonekano wako katika jamii na kazi yako kwa ujumla, huwezi kuwa msichana au msichana upo upo tu utacheza filamu gani na kuwateka watazamaji? Jiweke safi na kuigiza katika kiwango cha juu, kama naringia umbo langu mashallah si haba na hasa kama kuna nguo zake ambazo nazipatia kuvaa utanipenda,”anasema Badra.
Latifa Idabu
Badra katika pozi.
Badra ni moja kati ya wasanii wanaofanya vizuri katka tasnia ya filamu kwa sasa, filamu yake iliyong’arisha nyota yake ilikuwa ni Sanda Nyeusi, filamu iliyoigiza nje ya Jiji la Dar es Salaam huku msanii akiigiza katika uhusika wa aina mbili yaani mzimu na mtu hai, tayari msanii huyu ameshiriki filamu nyingi kama Home Village, Tifu la Mwaka Alfajiri na filamu nyingine nyingi zikiwepo zilipo mtaani na zilizo studio zikisubiri foleni.CHANZO; Filamu Central.

Posted by Bongo Film Data Base on 9:16 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for KUIMARISHA MWONEKANO WA WASANII WA KIKE HUCHUKUA SEHEMU KUBWA YA BAJETI YA MAPATO YETU

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign