''KUMI BORA MWAKA 2011 NDIYO HAWA HAPA''
habari 12:39 AM
Kama ilivyo kawaida katika nyanja na medani mbali mbali hapa duniani za kisiasa, muziki,dini,elimu,na vingine nyingi kama michezo wadau wake kupeana pongezi kwa mchango wao mkubwa wa kuelimisha ,kuliwaza na kuburudisha jamii yetu katika viwanja vya fursa zao ndani ya tasnia zao husika.
Kwa upande wa tasnia ya michezo hususani filamu hapa nchini kumekuwa kukitolewa tunzo tofauti tofauti kwa tayarishaji,wachezaji,wahariri,waandishi miswada na waongozaji bora wa filamu hapa tanzania kila mwaka kutoka asasi na vyombo vya habari mbali mbali kama redio,television,websites,kampuni za usambazaji kazi za wasani na kurasa za kijamii kama facebook kwa kadri inavyotambua mchango wa watayarishaji bora wa filamu hapa nchini.
Baada ya kupambanua upatikanaji au utolewaji tunzo hizo moja kwa moja naiangazia mwanga kumi bora ya mwaka huu zilizo wezeshwa na Redio Uhuru kupitia kipindi chake cha FILAMU ZETU moja kwa moja Bongo Film Database ilizungumza na mmoja ya wa husika wakuu katika utayarishaji tunzo hizi ambaye ndiye mtangazaji wa kipindi hicho cha Filamu Zetu, Suzan Lewis (Natasha). na bila ya kusita akatupa orodha ndefu sana ya wasani waliyo ingizwa kwenye kinyang'anyilo hiki kwa mwaka huu...
ORODHA YA BAADHI YA WASANI WALIOTAJWA KUWEPO KATIKA KINYANG'ANYILO HIKI NI HAWA HAPA.
HIYO HAPO JUU NI BAADHI TU YA WASANII KWENYE MCHAKATO
NA HII NDIYO ORODHA YA WASANI KUMI BORA WA MWAKA HUU WA 2011 KULINGANA NA KURA ZAO.
10.JUMA KILOWOKO (SAJUKI) kura 36
9.AUNT EZEKIEL kura 42
8.ROSE NDAUKA kura 66
7.CLOUD kura 106
6.BLANDINA CHANGULA kura 109
5.VICENT KIGOSI kura 110
4.RIYAMA ALY kura 143
3.JACOB STEVEN kura 166
2.YVONNE CHERYL kura 264
1.STEVEN KANUMBA kura 279
kituo hiki cha redio chenye kufika mbali zaidi hapa tanzania kwenye kurusha matangazo yake kwa jina huitwa UHURU FM..kiliendesha zoezi zima la kuwasaka wasani kumi bora wa mwaka huu wa 2011 katika tasnia ya filamu ambapo kwa ndani yake akapatikana msani bora wa kike na wakiume kuligana na idadi ya kura alizopata msanii ambao ni Steven Kanumba kwa upande wa kona ya wanaume na Yvonne Cheryl kwa upande wa kona ya wasani wa kike.
Naomba ni malizie na angalizo hapa pasije tokea maneno kabisa kwa wasani wenyewe na hata watu wengine ambao hakusikiliza kipindi cha filamu zetu. majina ya wasanii wote hawa yalipendekezwa na wadau wa filamu hapa nchini na hata hizo kura zilipigwa na wadua hao hao wenyewe na mfumo wa utafutaji wasani hawa kumi ulikuwa ni wa wazi kabisa yaani mahakimu(judge) walikuwa ni wadau na si mtu mwingine.
KWA WEWE MDAU AMBAYE HUKUSIKILIZA REDIO UHURU, BOFYA HAPA KUSIKIA WASANII BORA WA MWAKA HUU.
(Shukrani nyingi ziwafikie jopo zima la Filamu Zetu)
Asante!