EXCLUSIVE!!:PATCHO MWAMBA KUVUMISHIWA KUFA KWA MARA YA NNE MPAKA SASA NA KITUO KIKUBWA CHA TELEVISION HAPA NCHINI

Mwaka huu wa 2011 kwa wadau na wasani wa filamu na muziki hapa nchini unaonekana kuishilizia  na matukio ambayo si mazuri kabisa kwa upande wao, siku za katikati kumekuwa kukivumishwa vifo vingi  vya wasani wetu tukianzia na Mzee Kipara, Bi Kidude, Vengu wa kundi la Ze Komedi, Sajuki, na sasa ni Patcho Mwamba.


Kwa upande wa Patcho Mwamba mwaka huu mpaka kufikia hapa tayari inatosha kwa yeye kuufunga mwaka kwa majonzi makubwa zaidi ya wote iliyowataja  hapo juu ijapokuwa hata hao wengine wameandika historia ya tofauti ndani ya maisha yao kwa mwaka huu ya kuzushiwa wamekufa kitu ambacho si jambo la mzaha  na tena ni hatari kwa maisha ya binadamu yeyeto yule kwani  huwezi jua mtu unapomvumishiwa amekufa kuna kuwa na hali ya hatari sana na hata uwezekano wa kuamsha maladhi mengine kama ya kushituka moyo au  kuuchokonoa ubongo na kuathiri saikorojia ya mtu huyo  na watu wamzungukaye pia.


Patcho Mwamba mmoja ya wana familia ya Fm Academia a.k.a wazee wa ngwasuma anafikisha mara ya nne (4) sasa anavumishiwa kuwa amekufa na kibaya kuliko yote habari hizi zinarushwa hewani ama kufikishwa  kwa jamii na kituo kimoja cha television chenye kauli mbiu yenye kutia hamasa na kuonesha ni kwa namna gani mambo na matangazo yao yameaandaliwa kiumakini na kisomi zaidi, kauli mbui hiyo ni ''ELIMU KWANZA'' basi mpaka hapo natumai zijamwacha mtu kwenye hiyo kauli mbiu ya kituo cha television hicho cha  MLIMANI kilichopo hapo chuo kikuu cha Dar es saalam.


Sakata, tamthilia hii ama kwa jina rahisi kabisa twiite uvumi kama tulivyo zoea kuita jambo kama hili ulianza kumkumba Patcho Mwamba kwa  mara ya kwanza baada tu ya kufariki dunia baba yake mzazi huko Congo tarehe tano (5) ndani ya siku za mwanzoni kabisa za mwezi wa tano mwaka huu ndipo habari za namna hii zilitapakaa kwa mara ya kwanza kupitia chombo cha habari hicho hicho cha hapo mlimani kutangaza ya kuwa Patcho Mwamba kaaga dunia na  kipindi chenye tangazo hilo kikarudiwa kwa taklibana siku tatu bila kufuatilia kwa kina na ukweli wa jambo hilo, baada ya kugundulika taarifa hiyo haikuwa na ukweli ndani yake wahusika hawa wakuthubutu kulekebisha kauli hiyo kwa jamii..


Jana usiku  kulienea kwa taarifa ya msiba wa Bwana Patcho Mwamba tena  kufariki dunia kitu mbacho kimemkela sana Patcho kiasi cha kuchukuwa uamuzi kuandaa taratibu za  sheria ichukuwe mkondo wake  na iwe funzo kwa  vyombo vya habari hapa nchii vyenye tabia ya kutaarifu jamii habari zisizokuwa na ukweli ndani yake kama hizi tena zenye kushtusha kwa kiasi kikubwa sana. .


Bongo Film DataBase ilipotonywa na mmoja ya wadau wetu kwenye huu ukurasa moja kwa moj dawati la uhariri likafuatilia kiukaribu na kufanya mahojiano ya moja kwa moja na Patcho Mwamba kwa njia ya simu na kuzungumza naye kwa kirefu juu uvumi huu, tuna shukuru Mungu Patcho alipokea simu mwenyewe bila msaada toka kwa mtu yeyote akiwa hai na mzima kabisa tena mwenye afya njema kama siku zote kabla hajapanda jukwaani kutumbuiza kwenye band yake ya wazee wa ngwasuma.  


SIKILIZA SAUTI ZA MAZUNGUMZO YETU NA PATCHO MWAMBA AKIKANUSHA NA KURAANI  KITENDO HIKI CHA KUVUMISHIWA NA KITUO CHA TELEVISION CHA HAPO MLIMANI NA AMEAHIDI KUKICHUKULIA HATUA ZA KISHERIA KITUO HIKI JUMATATU(Shukurani nyingi kwa Tico toka Timamu Effects)

Posted by Bongo Film Data Base on 3:09 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for EXCLUSIVE!!:PATCHO MWAMBA KUVUMISHIWA KUFA KWA MARA YA NNE MPAKA SASA NA KITUO KIKUBWA CHA TELEVISION HAPA NCHINI

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign