BIFU NA UTATA MWINGINE TENA HUU HAPA WATENGENEZWA NA MAGAZETI
habari 12:34 PM
Hadithi hiyo iliambatanishwa na kuwepo kwa picha za utupu za Jackline wolper ila mpaka sasa picha hizo hazipo hewani wala gazeti lolote lile....
Inazidi kudaiwa kwamba Wema alijaribu kumfanya Diamond atulie lakini ikashindikana, ilipodhihirika Jokate ameshika mpini, alianza kupata mateso ya moyo na hisia kwa jinsi alivyofanywa ‘spea tairi’.
Madai ‘yanahiti’ pia kwamba Wema alithibitisha kuwa Diamond na Jokate wanamchezea ‘ukuti ukuti’ baada ya kuwafumania wakiwa ‘vere klozi’ kimahaba kwenye Hoteli ya Picolo, Masaki, Dar es Salaam.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa Wema alipowakuta Diamond na Jokate, hakuangusha varangati kama mmiliki, badala yake alinywea utadhani yeye ndiye mwizi kisha akawaambia: “Samahanini sana kwa kuwaingilia kwenye starehe zenu.”
Wema na Jokate, walipambana kwenye vita ya kuwania Taji la Miss Tanzania mwaka 2006 lakini safari hii wanapambana kwa ajili ya penzi la mwanaume.
Mwaka 2006, Wema aliibuka kidedea kwa kuchukua taji, wakati Jokate alishika nafasi ya pili, safari hii inaonekana kibao kimegeuka, kwani Miss Tanzania huyo bila kulazimishwa, mwenyewe kainua mikono na kutimka.

Mrembo huyo alisema, anaumia kwa sababu aliamua kutulia na Diamond kwa mapenzi yote na uaminifu, kumbe mwenzake hakuwa na utulivu.
“Unajua watu wengi wanajua mimi situlii na mwanaume mmoja kitu ambacho nakipinga kabisa, kwa maana kuna wakati navumilia ninayofanyiwa na wanaume lakini inashindikana,” alisema Wema.
Staa huyo aliendelea kusema kuwa baada ya kujua uhusiano unaoendelea kati ya Diamond na Jokate, aliamua kujifanya mjinga ili mchumba wake huyo ajirekebishe lakini bado akawa anasikia habari hizo.
“Nimeona bora nirudi nyumbani kwetu nikapumzike kwanza, kwa maana nyumbani kwetu sijafukuzwa wala hakuna shida yoyote,” alisema Wema.
JOKATE NAYE PICHA KUTOKA UKURASA WA CHOKA
“Sijatembea na Diamond, nilikuwa karibu naye kikazi. Wimbo mpya wa Diamond unaoitwa Mawazo, video yake na mimi nimecheza.
“Ni kweli kuna maeneo kadhaa nilikuwa naambatana na Diamond lakini siyo kimapenzi. Nilikuwa naye kikazi, siyo kimapenzi hata kidogo,” alisema Jokate.
KWA WALE WANAPENDA KUSHIRIKI KWENYE HII TAMTHILIA TUAACHIE KOMENT ZAKO HAPO KWENYE KISANDUKU CHETU CHA MAONI....
WEE ACHA TAMAA UMEONA WEMA ANAFAID SANA KUWA NA MSIMAMO KAMA MWANAMKE USIPENDE KUVURUGA MAPENZI YA WATU MUNGU HAPENDI HIVYO DO YOU UNDERSTAND
hivi hawa wasanii wa Bongo hawawezi kuokoka na kumkabithi Bwana yesu awe mokozi wa maisha yao?hawaoni kwamba mwenendo wa maisha yao utabadirika na bado wataendelea kung'aa zaidi katika kazi zao.....
Jamani Watanzania haijarishi kama wewe ni msanii ama la ukweli unabaki palepale kwamba wewe ni mtanzania hebu tuwe na hofu ya Mungu japo kidogo halafu tuone jinsi Mungu atakavo tuinua.
Mrs. Mwakyusa