NJOO NA UWE MTAYARISHAJI FILAMU WA KIMATAIFA LEO
Posted by Bongo Film Data Base
habari,
mpya,
workshop
11:30 PM
TASNIA ya filamu kila siku inazidi kukua na kuelekea katika anga za
kimaifa ili kukabili changamoto za soko la kimataifa watarishaji,
waongozaji, wasanii na wadau wote kwa ujumla wanahitaji kufahamu,
kujifunza zaidi mambo mengi ya utayarishaji na utengenezaji wa filamu
bora ili kuweza kuingia katika ushindani zaidi.
Kwa kuliona hilo kampuni ya Wegos works ltd kwa kushirikiana na Ramoji
Film City ya nchini India imeandaa mafunzo kwa ajili ya watengeneza
filamu (Filmmaking & Acting workshop ) Tanzania, ni fursa nyingine
kwa wadau wa filamu kutumia nafasi hiyo adimu ya kupata ujuzi zaidi
kutoka kwa watalamu wa filamu kutoka Bollywood.
(Picha ya wapiga picha wakiwa kazini.)
Muongozaji na mkufunzi wa filmmaking mwenye uzoefu zaidi ya miaka
kumi na mbili ataongoza mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na fursa za
kutafuta masoko kimataifa na njia za kufika sehemu zilizofanikiwa katika
tasnia hiyo ya filamu, kama Bollywood na Hollywood, kwa wale wote
wanaotakakushiriki katika mafunzo hayo WAWASILIANA na Mraibu kwa simu :
+255715 520 520. TAFADHARI USIBEEP.
.
NYOTE MNAKARIBISHWA KWA MAENDELEO YA TASNIA YA FILAMU TANZANIA.
CHANZO;FILAMU CENTRAL
Posted by Bongo Film Data Base
on 11:30 PM.
Filed under
habari,
mpya,
workshop
.
You can follow any responses to this entry through the
RSS 2.0