''BONGO MOVIES FC YA NYAKUWA KIKOMBE CHA TUWASAIDIE WAHANGA WA MAFURIKO DSM''

''TUWASAIDIE WAHANGA WA MAFURIKO DSM'' ni mechi iliyokuwa imejaa utani mwingi toka milango yote miwili ya timu zilizo kutana kuwania kikombe cha tuwasaidie mahanga wa mauriko yaliyotokea jijini Dar es salaam mwishoni mwa mwaka 2011 siku nne kabla ya siku ya Noel ali maarufu ijulikanayo kwa jina la krismas ambapo jiji la dar es salaam lilipokumbwa na janga hili la mafuriko  lililopelekea na watu makumi kupoteza maisha na mamia waliobaki kuhalibikiwa na hata kupotelewa kabisa mali zao kuanzia makazi na vifaa vyote vya ndani pamoja na chakula na pesa...

Compact Media kwa kushirikiana na Times Fm na kikombe chenye kauli mbiu ya TUWASAIDIE WAHANGA WA MAFURIKO DSM walifanikiwa kuwaingiza uwanjani wahasimu wawili Bongo Movie Fc na Kadansi Fc za Tanzania  kukishindania kikombe hicho kwa lengo moja tu la kuchangia pesa kwenye mfuko maalumu utakao ongozea katika kuwasaidia wahanga wa mafuriko jijini dar es salaam, mtanange huu ulifana kwa kiasi chake kwani uligubikwa na mazingira ya kisanii zaidi pande zote mbili,mara hawa kuwamwagia maji wengine kila mmoja alipofungwa ambapo hiyo ilikuwa ni kuashilia kuwa wanaloa magoli na wataendelea kuloa magoli zaidi na zaidi..
Ugeni rasmi ulikuwa mkubwa sana kwa siku hiyo kwa ni walihudhulia na wakubwa wa jiji hili la Dar es salaam tukianzia utande wa serikali alikuwepo mkuu wa mkoa huu ndugu,Said Meck Sadik na upande mwingine alikuwa  kamanda wa jeshi la wananchi kanda maalumu ya Dar es salaam Bwana Suleiman Kova msimazi wa timu ya bongo kadansi fc na wao ndiyo waliwakabidhi kombe washindi wa mechi hiyo...

Tukianza na timu iliyokuwa imependeshwa na uzi mweupe na michilizi mwekundu ''Bongo Movie Fc'' waliingia uwanjani wakiwa wamejiamini kwa kiasi kikubwa sana yaani kama walijua wanakwenda kushinda vile, Mungu si athumani vijana hawa wakaibuka kidedea na kulinyanyua kombe hili la TUWASAIDIE WAHANGA WA MAFURIKO DSM juu kabisa tena kwa mbwembwe zote za hatari...

Wakati upande wa pili wa shilingi twauita hivyo kwenye duara wa kamali ila kisoka zaidi tutasema upande wa pili wa goli ama wapinzani ''Bongo Kadansi Fc'' waliyojitundukia jezi za rangi ya majano na weusi kidogo waliokuwa katika hali ya kutoamini kabisa wanachokiona pale uwanjani wa kuplekeshwa pelekeshwa kimchezo na wapinzani wao na kutawaliwa na majeruhi mengi kupita maelezo kupelekea hata kukosekana kwa wachezaji kufidiya mapengo ya wote waliyo umia na kuachukua uamuzi wakumwingiza goli kipa toka timu pinzani ili liende tu ila zoezi za hatua na maamuzi hayo yaligonga mwamba mara baada ya mwamuzi (refa) kupinga uamuzi huo na hatimaye matumaini kupotea sasa na  kupoteza mchezo huo na kuruhusu kombe liangukie mikononi mwa club ya Bongo Film kwa kulala na bao tatu(3) dhidi ya wapinzani wenzao kuondoka na wamewanyuka bao nne(4).

Magoli matatu ya  Bongo Kadansi Fc yalipachikwa kwenye  nyavu na kijana toka Fm Academia,na Jose Mara kutoka Mapacha wa tatu wakati magoli ya washindi na mabingwa wa mechi hii ya Bongo Movie yalitingisha nyavu ya Bongo Kadansi mara nne, magoli  yaliyofungwa na Rado,Kupa,wiliamu mtitu na kijana mwenye jezi nambari nane mgongini kwa jina la uwanja aliitwa Mes ndani ya dakika za awali, katikati na mwishoni mwisho mwa mchezo huo....


 ''Habari, taarifa, matukio na vimbwanga vya kwenye mechi hii vitaendelea kukuijia kwa kila kadri ya uwezo wetu wangalau kila siku''

Picha na Habari; Oscar Mpejiwa.

Posted by Bongo Film Data Base on 12:55 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for ''BONGO MOVIES FC YA NYAKUWA KIKOMBE CHA TUWASAIDIE WAHANGA WA MAFURIKO DSM''

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign