JACK WA CHUZ; FILAMU YA ‘QUEEN SPEAR’ ITANITOA KIMATAIFA !!

MSANII wa filamu bongo Jackline Pantezel, almaarufu kama ‘Jack wa Chuz’, amesema ubunifu aliyouonesha  katika filamu ya ‘Queen Spear‘, ni wa hali ya juu hivyo anaamini itamsaidia kumtoa kimataifa.

Akizungumza na DarTalk, msanii huyo alisema kuwa filamu hiyo ni kati ya anazozitengemea katika kumtangaza zaidi kwani zina matukio mengi ya kusisimua amabyo yamebeba ujumbe za kutosha.

Alisema kuwa anajua amecheza katika kiwango kikubwa lakini anaamini bado kuna makosa machache ambayo yanaweza kuonekana hivyo anahitaji kukosolewa pale ambapo amefanya vibaya.

“Makosa yapo hivyo hatuoni kama yatakuwa ni mengi kiasi kwamba filamu haitafanya vizuri, kazi imetulia na itakuwa moja ya filamu ambazo zitashika kasi baada ya kutoka,” alisema.

Filamu hiyo imetungwa na mtunzi mahiri nchini Aunty Fifii, ambaye ndiye mtunzi wa filamu ya ‘Senior Bachelor’ iliyochukua tuzo ya ZIFF, mara mbili.

Chanzo;Dartalk
asante!

Posted by Bongo Film Data Base on 7:22 PM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for JACK WA CHUZ; FILAMU YA ‘QUEEN SPEAR’ ITANITOA KIMATAIFA !!

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign