JON MYUZIK; NATAKA KUCHEZA FILAMU !!

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Jon Myuzik, amesema anafikiria kucheza filamu lakini siyo za mapenzi kama ilivyo kwa wasanii wengine ambao wengi hawana mabadiliko ya kazi wanazocheza.

Akizungumza na DarTalk, Jon alisema anaweza kucheza filamu lakini hatofanya kazi na nyota ambao wanamaringo kwa mafanikio yao waliyoyapata. Alisema anaamini kazi hiyo haina mwenyewe lakini wapo wasanii wanaofanya vizuri.

“Nitafanya kazi hii ambayo hivi sasa ina idadi kubwa ya wasanii ambao wengi wao wanauza sura, bila kujua Watannzania wanahitaji nini hasa kipindi hiki ambacho kuna matatizo katika jamii zetu,” alisema.

Jon alisema hata hivyo tayari ameshaanza mazungumzo na baadhi ya wasanii ambao anaamini wataweza kucheza katika filamu yake ya kwanza.

“Mazungumzo yanafanyika na baadhi ya wasanii ambao naamini nitaweza kucheza nao, lakini kabla ya yote lazima kwanza wanipe kwanza mfumo wa filamu  unavyokuwa,” Aliongeza.


Chanzo; Dartalk
asante!

Posted by Bongo Film Data Base on 7:16 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for JON MYUZIK; NATAKA KUCHEZA FILAMU !!

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign