MIMI NDIYO SENIOR BACHELOR BWANA!!..,TUNZO NILIZOPEWA NASTAHILI KABISA

GWIJI la uigizaji na utayarishaji wa filamu Swahiliwood, Jacob Stephen JB, amesema anawashangaa wale wanaohoji yeye kushinda Tuzo za Ziff katika uhusika tofauti mara mbili kwa filamu ambayo si yake. 

Hivi karibuni kuliibuka maswali kuwa huenda waandaaji wa Tuzo za Ziff zilizofanyika jijini Dar es Salaam walikosea katika utoaji wa Tuzo ya Filamu Bora kwa JB. 

Mtunzi wa filamu hiyo ya Senior Bachelor, Aunt Fifi, alitaka kujua ni vigezo gani ambavyo watoaji wa tuzo hizo walitumia katika utoaji wa tuzo hizo kwa kumpatia JB tuzo zote mara nyingi katika uhusika tofauti. 

Wakati mwaka huu amepata tuzo ya Filamu Bora, lakini mwaka jana filamu hiyo ya Senior Bachelor ilimpatia JB tuzo ya Mwigizaji Bora kutoka Ziff. 

Mwanaspoti ilizungumza na JB kuhusu utata huo na alishangazwa; Senior Bachelor imeshinda kama Filamu Bora na mimi nikaipokea kwa niaba ya kampuni ya Jerusalem Film, kwa njia moja au nyingine nilistahili kufanya hivyo kwa ajili ya kampuni, lakini tuzo ya kwanza nilishinda kama Mwigizaji Bora, hii ilikuwa ni haki yangu na tuzo hiyo iende kwa mtunzi ambaye ni Aunt Fifi, binafsi naheshimu utunzi wake na nimempa heshima yake katika filamu hiyo. 

Filamu ya Senior Bachelor ilitungwa na kuandikwa na Tumaini Bigirimana Aunt Fifi na kuongozwa na Single Mtambalike Richie. 

JB anasema kuwa ni wakati ambao wasani wanatakiwa kufanya kazi na si kulalamika muda mwingi, kwani hiyo haijengi bali ni kupoteza muda


Chanzo;mwanaspoti.
asante! 

Posted by Bongo Film Data Base on 1:38 PM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MIMI NDIYO SENIOR BACHELOR BWANA!!..,TUNZO NILIZOPEWA NASTAHILI KABISA

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign