JE? UNADHANI FILAMU ZA KIBONGO ZINAUZA ZAIDI KUTOKANA NA SKENDO ZA MASTAA WAKE MAGAZETINI?!


Imekuwa ni hali ya kawaida na iliyozoeleka kwa wanamuziki kutoa album zao mpya na kutengeneza vituko ama skendo ifahamikavyo hivyo kwa jina lingine ili kuipalilia njia album yake kufanya vizuri sokoni, tabia hii imekuwa ikitumika  sana kwa  mataifa mengine yaliyokuwa kimafanikio kwenye upande wa muziki kama marekani na bara la ulaya. kwa nchini hizi za ukanda wa afrika mashariki  hususani Tanzania, Kenya, Uganada,Rwanda na Burundia imekuwa ni tofauti sana kwani mwendo huo wa vituko haujafanikiwa kivile isipokuwa nchi  ya Uganda kidogo vituko vya mastaa vimeweza kuongeza mauzo ya album zao mafano Bebe cool kukwaluzana na Bob wine ama Jose chamillion kwenye uzinduzi wa album zao. nchini  ya Tanzania  haijafanikiwa kwa hilo kutokana na mapokeo ya vituko hivyo kwa wana nchi vimekuwa ni tofauti sana na kuonekana  ni kupoka kwa maadali ya huyo atakaye fanya hivyo...

Huo ulikuwa ni upande wa pili wa shilingi kutoka sarafu ya taifa moja la burudani kwa maana ya hakuna filamu bila muziki na hakuna muziki bila filamu. Filamu sasa imekuwa ni tofauti sana kwa wenzetu walio endelea huko marekani kwani wa huuza filamu zao kutokana na ubora wa filamu zilizowahi kutengenezwa na kampuni husika mfano filamu zilizotengenezwa na DREAM WORK ,filamu nyingi zitokazo toka hapo zitafanya vizuri sana, filamu zilizotoka DREAM WORK  ni kama TRANSFORMER 1 ambayo ikaitendgenezea vyema njia ya TRASNFORMER 2 alikadhalika hiyo nayo imeitengenezea njia inayofuata  ambayo ni TRASNFORMER 3 inayosubiliwa kwa hamu sana na watizamaji wa filamu ulimwenguni kote..

Mauzo mazuri yanatengenezwa na kampuni  ambayo hutoa filamu bora zaidi hata kwa mara ya kwanza ama kwa mara kadha ila hakiwezi patikana filamu nzuri kama hakuna jopo zuri la utayarishaji filamu hiyo tukianzia na mwongozaji (DIRECTOR) ambapo hapa kwa wenzetu mwongozaji amekuwa ni mtu muhimu sana  katika utayarishaji hizi filamu mfano  filamu ambazo zimeongozwa na  MICHEAL BAY (Transformer1,2 na 3 itakayokuja ), zimekuwa zikipendwa sana na kufanikiwa kutengeneza klabu za wadau wake ambao daima husubili na kuzifuata popote pale filamu zake zitaoneshwa kama sio kuzinunua kabisa.

MICHEAL BENJAMIN BAY (Director)



Na JAMES CAMERON mwongozaji mahiri chini ya kampuni ya DIMENSION FILM amefanya vizuri sana kwenye filamu zote alizohusika  kuziongoza yeye na kufanya vizuri zaidi sokoni na hata kupigiwa kura nyingi na mashabiki wake kuomba zichezwe sehemu ya pili ya filamu mfano AVATAR sehemu ya pili  ambayo ipo mbioni kutoka. ukiachilia mbali hiyo filamu ya AVATAR ya hivi karibuni James Cameron aliongoza filamu nyingi sana ambazo zilimpa  jina kubwa na kumwingizia fedha za kutosha mpaka sasa kwenye akiba zake, miongoni mwa filamu ambazo zilivutia mamilioni ya watazamaji ulimwenguni kote ni hizi hapa chini;

TitanicAliensAvatar
Terminator 2: Judgment Day










             Asilimia kubwa ya watazamaji kuwa na kiu ya kutaka kuangalia sehemu ya pili ya filamu duniani kote kumetokana na filamu kuwa ni nzuri zaidi ambayo umetengenzwa na kampuni kubwa inayojitosheleza na kitekinolojia pia chini ya jopo zuri la utayarishaji lenye mwongozaji mzuri pia ambapo watu wasikiapo filamu fulani imeongozwa na mwongozaji aliyeongoza filamu ambayo ilimvutia na kuipenda  chini ya kampuni nzuri anakuwa na shahuku ya kutaka kuona filamu hiyo mpya...ila kwa nchi za ukanda huu wa Afrika mashariki sijui ni mfumo gani wanatumia kupalilia soko la filamu zao.Tanzania  imekuwa tofauti sana kwa hili kwani filamu zao hufanya vizuri ama kupalilia njia ya soko lao kutoka na vituko vya mahusika waliyocheza filamu hizo hususani wa dada amabo skendo zimekuwa ndiyo chachandu ya kucheza filamu nyingi zaidi kwani watu huenda kununu filamu baada ya kumwona staa kwenye magazeti sana.. sasa swali kwa hawa mastaa wanaotengemea skendo za magazetini siku watu wamechoka kusoma vituko vyako kwenye hayo magazeti utapata kazi kweli?


IRENE Uwoya  mwigizaji na mtayarishaji filamu za kitanzania anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine baada ya kusema kuwa mbali na mwanaye Krish, yupo tayari kuzaa mpaka basi hata kama watafika watoto 10.

 Irene alisema kuwa hakuna kitu anachopenda kama kuitwa mama kila wakati akiwa na mtoto mchanga.na Krish sasa anahitaji wadogo zake na kwa kuwa bado anatamani kuzaa, ni ishu ya muda tu kwani anapenda watoto.
Irene alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa kuna wakati baadhi ya watu walidhani mapenzi yake kwa Ndikumana yamehamia kwa mtoto kutokana na kumjali zaidi kuliko kitu kingine chochote. kipande cha hadithi ya Irene Uwoya tumeinukuu toka sehemu fulani(gazetini )  ambako tuliliona hili ni jambo  ni mbinu ya dada huyu kutafuta namna ya kupalilia filamu mpya ijayo chini ya kampuni yake  jina la filamu hilo tumelihifadhi kwa sasa...

SASA KITUKO KAMA HIKI KITAONGEZA MAUZO YA FILAMU YAKE IJAYO? NA  JE? KUTAMWONGEZEA KAZI ZAIDI!!


Posted by Bongo Film Data Base on 12:51 PM. Filed under , , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for JE? UNADHANI FILAMU ZA KIBONGO ZINAUZA ZAIDI KUTOKANA NA SKENDO ZA MASTAA WAKE MAGAZETINI?!

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign