KUJUA KUANDAA MISWADA NI SILAHA MUHIMU LAKINI KUJUA MBINU ZA KUTAFUTA MASOKO, KUIMARISHA UHUSIANO NA WATAYARISHAJI NI MUHIMU PIA

Kuanzia tarehe 13 mpaka 15 mwezi wa pili mwaka huu Idara ya Sanaa na sanaa za maonyesho Chuo kikuu cha Dar es salaam ikiwakilishwa na Dr Vicensia Shule kwa kushirikiana na wahitimu wa idara hiyo John Mwakilama na Debora Jingu,waliandaa warsha ya uandishi wa miswada ya filamu ngazi ya kwanza (level 1) lengo kubwa ikiwa ni kusambaza elimu ya uandishi wa miswada ya filamu kwa wasanii na wapenzi wa filamu, pia kuwaweka karibu wasanii na Idara ya Sanaa na sanaa za maonyesho, ili kuweza kupata msaada wa kisanaa watakaohitaji, kama ilivyosemwa na Mkuu wa Idara Dr Herbert Makoye alipoongea na washiriki kuwa wasanii wajisikie huru kutumia idara kwa shughuri zao mbalimbali za kisanii na kuweka wazi milango ya ushirikiano.

Warsha ilikuwa na washiriki 14 kutoka sehemu na asasi mbalimbali,wengine wakiwa ni wasanii na wengine wakiwa ni wapenzi wa filamu wanaofanya kazi tofauti na filamu,washiriki hawa waliweza kuelekezwa jinsi ya kuandika miswada ya filamu kwa utaalam zaidi na pia waliweza kutoa mawazo yao ya jinsi gani walivyokua wanafanya kazi mtaani kabla ya hii warsha. Wengi wao waliona kuwa kuna changamoto kubwa kwakua hadithi zetu nyingi haziandikwi kwa utaalam na hivyo tunashindwa kuzalisha filamu bora zitakazo tupeleka katika ngazi za kimataifa.

Licha ya kuelekezwa uandishi wa miswada pekee washiriki walipata nafasi ya kuelekezwa juu ya kutafuta masoko ya kazi zao,jinsi ya kushirikiana na asasi mbalimbali zinazohusiana na mambo ya sanaa kama BASATA,TAFF,TASA,TAFIDA,COSOTA na kufahamu kanuni mbalimbali za Bodi ya Filamu, Baada ya warsha washiriki waliweza kukabidhiwa vyeti vyao vya ushiriki na mkuu wa Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonyesho Dr Herbert Makoye.

Naamini kuwa warsha hii imeweza kuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa sana kwakua washiriki hawa 14 walioshiriki hii warsha watakua ni chachu kubwa kwa maendeleo ya tasnia ya filamu na taifa kwa ujumla, Pia warsha hii imeweza kutufumbua macho na kujua kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na warsha za aina hii mara kwa mara kama ambavyo washiriki wenyewe walivyopendekeza,kwani kuna uhitaji mkubwa wa elimu ya namna hii.

Changamoto kubwa niliyoiona katika warsha hii ni kuwa bado tunahitaji kuweka nguvu kubwa ili kuwashawishi wasanii wetu waweze kujiendeleza kwa kutafuta elimu mbalimbali zinazohusu tasnia ya filamu kwani wale wasanii na wadau wakubwa wa sanaa ni wachache sana walioweza kujitokeza,na hii ni mbaya kwakua kuna kundi la wafanyakazi wasio kwenye tasnia hii ambalo lilijitokeza katika warsha kama litaamua kujiingiza katika tasnia hii basi itakua ni kazi kubwa sana kwa wasanii kushindana nao kwani wao wameonyesha uchu wa kutaka kufahamu mambo mbalimbali kuhusiana na filamu.

Mwisho kabisa napenda kutoa wito kwa wasanii na wadau wa filamu kuwa huu ni wakati wa kufanya mabadiriko makubwa katika tasnia hii ambayo kama tutaifanya kitaalam itakua ni chanzo kizuri cha ajira na pia kipato cha Taifa.
John Mwakilama
 
Imeandaliwa na John na kuletwa kwenu na  BFDB
Asante!

Posted by Bongo Film Data Base on 11:15 AM. Filed under , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

2 comments for KUJUA KUANDAA MISWADA NI SILAHA MUHIMU LAKINI KUJUA MBINU ZA KUTAFUTA MASOKO, KUIMARISHA UHUSIANO NA WATAYARISHAJI NI MUHIMU PIA

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign