CHAIBA KOMBO ; UUNDAJI WA FILAMU BORA NI HUU (SEHEMU YA KWANZA )

UUNDAJI WA FILAMU BORA 
Uundaji wa  filamu ni kazi inayofanywa na watu wanaoitwa ‘Producers’ kwa lugha ya wenzetu, kwetu sisi tunawaita ‘Waundaji’ ambao wamegawanyika kwenye makundi mengi lakini uandaaji yaani ‘Production’ unasimamiwa na waundaji wa aina mbili  nao ni Executive Producers na ‘Producers’.

Watu hawa ni wataalamu wa fani hii kitaalam nikiwa na maana wameisomea kwa elimu ya juu na wanaijua kila kipengele chake kutoka utayarishaji mpaka uundaji wa filamu lakini pia wanatofautiana sifa zao kwa mujibu wa sheria za uundaji wa filamu bora.


Kwanza kuna mtu anayeitwa Executive Producer kwa lugha nyingine humuita ‘Mungu Mkubwa’ yeye anaweza kuwa msomi au hajui chochote kwenye fani ila yeye anaipenda fani hii na antaka kuiendeleza kwa kuchangia kifedha au ni biashara anayotaka kuifanya. Executive Producer ambaye sio msomi kwenye fani hii, ili aweze kufainya kazi yake vizuri hata kama ni msomi wa fani, pia kutokana na majukumu mengi aliyonayo kuanzia kwenye ‘Wazo’ mpaka filamu ikamilike hawezi kusimamia kazi yote peke yake na hapo ndio atatafutwa Producer ‘Mungu Mdogo’ ambaye ndie atakaye kua msimamizi wa kila hatua ya filamu nzima mpaka kuingia madukani yeye ni msaidizi wa Executive producer. Yeye ni lazima awe msomi wa fani.


Producer anapopatikana yeye anshirikiana na E.P. (Executive Producer) kumtafuta Mwandishi kwani yeye anamjua mwandishi mzuri atakayemhoji na kujua uwezo wake wa uandishi, endapo tayari wazo lilikwisha patikana, na kama wazo bado halijapatikana basi yeye atashirikiana na E.P kulipataa. Kisha yeye kwa vile ni mtaalamu atashirikiana na Mwandishi kuliendeleza hilo wazo. Ushirikiano wake na Mwandishi huku wakipitia kwenye vipengele vyote vinane vya uandishi wa filamu hadi kupata Mswaada wa majadiliano ambao sasa kazi ya Mwandishi itakuwa imekwisha na atatafutwa Director.

Director atashika usukani nae pia akishirikiana na Producer kutengeneza kitu kinaitwa na wenzetu ‘screenplay’. Ni lazima Director awe na ujuzi wa Uandishi wa filamu na misingi yake yote minane mpaka kuupata muswaada wake, maana yake awe ni mbunifu maana yeye ndie atakaye tuonesha hadithi katika picha iliyoandikwa na Scriptwriter, nayeye ndie mlaumiwa iwapo filamu itatoka vibaya pia Producer anaweza kumchagua Mwandishi yule yule kuwa Director au akachagua mtu mwingine kabisha. Kuchagua mtu mwingine husaidia kugundua mapungufu yatakayokuwa yamefanywa na Mwandishi kwenye mswaada wa majadiliano kwani akichaguliwa Director mwingeine atakuwa haijui hadithi ile na atakuwa na mawazo yake ambayo pengine yanaweza kuboresha hadithi zaidi. Hivyoi ni vema kuchagua mwingine ili kugundua mapungufu yaliyotokea haswa kwa sisi ambao bado wachanga kwenye fani.


Ndipo tunaingia kwenye hatua ya ‘Producion’ ambayo sasa makundi yangawanyika kwenye wizara kuu nne. 1.Production Department,
2.Technical Department,
3.Sound Department na
4.Art Department.

  Hivyo Producer atawatafuta viongozi wa wizara hizi ambao ni Production Designer, D.O.P Director of Photography, Sound Engineer na Art Director.


EWE MDAU MWENZANGU USIKOSE TOLEO LIFUATALO KUJUA NINI KINAFUATA MARA BAADA YA PRODUCER KUTAFUTA NA KUWAPATA WATU WA WIZARA HIZO KUU KWENYE UTAYARISHAJI FILAMU NA JE? KAZI IPI HASA  HASA  ATAFANYA NAO KUKAMILISHA FILAMU BORA YENYE VIWANGO ITAKAYO REJESHA PESA ZOTE ALIZO WEKEZA HUYU EXCUTIVE PRODUCER?!.....
    Karibu sana mdau na tafadhali wafahamishe wadau wengine pia.
IMEANDALIWA NA
Chaiba Kombo
Binti Wakubhubha

Posted by Bongo Film Data Base on 10:22 AM. Filed under , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

2 comments for CHAIBA KOMBO ; UUNDAJI WA FILAMU BORA NI HUU (SEHEMU YA KWANZA )

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign