KUJUA KUANDAA MISWADA NI SILAHA MUHIMU LAKINI KUJUA MBINU ZA KUTAFUTA MASOKO, KUIMARISHA UHUSIANO NA WATAYARISHAJI NI MUHIMU PIA
Posted by Bongo Film Data Base
habari,
mitandao,
mpya,
slide
11:15 AM
Kuanzia
tarehe 13 mpaka 15 mwezi wa pili mwaka huu Idara ya Sanaa na sanaa za
maonyesho Chuo kikuu cha Dar es salaam ikiwakilishwa na Dr Vicensia
Shule kwa kushirikiana na wahitimu wa idara hiyo John Mwakilama na
Debora Jingu,waliandaa warsha ya uandishi wa miswada ya filamu ngazi ya
kwanza (level 1) lengo kubwa ikiwa ni kusambaza elimu ya uandishi wa
miswada ya filamu kwa wasanii na wapenzi wa filamu,
pia kuwaweka karibu wasanii na Idara ya Sanaa na sanaa za maonyesho,
ili kuweza kupata msaada wa kisanaa watakaohitaji, kama ilivyosemwa na
Mkuu wa Idara Dr Herbert Makoye alipoongea na washiriki kuwa wasanii
wajisikie huru kutumia idara kwa shughuri zao mbalimbali za kisanii na
kuweka wazi milango ya ushirikiano.
Warsha ilikuwa na washiriki 14
kutoka sehemu na asasi mbalimbali,wengine wakiwa ni wasanii na wengine
wakiwa ni wapenzi wa filamu wanaofanya kazi tofauti na filamu,washiriki
hawa waliweza kuelekezwa jinsi ya kuandika miswada ya filamu kwa utaalam
zaidi na pia waliweza kutoa mawazo yao ya jinsi gani walivyokua
wanafanya kazi mtaani kabla ya hii warsha. Wengi wao waliona kuwa kuna
changamoto kubwa kwakua hadithi zetu nyingi haziandikwi kwa utaalam na
hivyo tunashindwa kuzalisha filamu bora zitakazo tupeleka katika ngazi
za kimataifa.
Licha ya kuelekezwa uandishi wa miswada pekee
washiriki walipata nafasi ya kuelekezwa juu ya kutafuta masoko ya kazi
zao,jinsi ya kushirikiana na asasi mbalimbali zinazohusiana na mambo ya
sanaa kama BASATA,TAFF,TASA,TAFIDA,COSOTA na kufahamu kanuni mbalimbali za Bodi ya Filamu, Baada ya warsha washiriki waliweza kukabidhiwa vyeti vyao vya ushiriki
na mkuu wa Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonyesho Dr Herbert Makoye.
Naamini kuwa warsha hii imeweza kuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa sana
kwakua washiriki hawa 14 walioshiriki hii warsha watakua ni chachu
kubwa kwa maendeleo ya tasnia ya filamu na taifa kwa ujumla, Pia warsha
hii imeweza kutufumbua macho na kujua kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwa
na warsha za aina hii mara kwa mara kama ambavyo washiriki wenyewe
walivyopendekeza,kwani kuna uhitaji mkubwa wa elimu ya namna hii.
Changamoto kubwa niliyoiona katika warsha hii ni kuwa bado tunahitaji
kuweka nguvu kubwa ili kuwashawishi wasanii wetu waweze kujiendeleza kwa
kutafuta elimu mbalimbali zinazohusu tasnia ya filamu kwani wale
wasanii na wadau wakubwa wa sanaa ni wachache sana walioweza
kujitokeza,na hii ni mbaya kwakua kuna kundi la wafanyakazi wasio kwenye
tasnia hii ambalo lilijitokeza katika warsha kama litaamua kujiingiza
katika tasnia hii basi itakua ni kazi kubwa sana kwa wasanii kushindana
nao kwani wao wameonyesha uchu wa kutaka kufahamu mambo mbalimbali
kuhusiana na filamu.
Mwisho kabisa napenda kutoa wito kwa wasanii na
wadau wa filamu kuwa huu ni wakati wa kufanya mabadiriko makubwa katika
tasnia hii ambayo kama tutaifanya kitaalam itakua ni chanzo kizuri cha
ajira na pia kipato cha Taifa.
John Mwakilama
Imeandaliwa na John na kuletwa kwenu na BFDB
Asante!
Posted by Bongo Film Data Base
on 11:15 AM.
Filed under
habari,
mitandao,
mpya,
slide
.
You can follow any responses to this entry through the
RSS 2.0
well said,tathmini nzima ya mafunzo yaliyotolewa ni nzuri ila tungependa kufahamu ni lini mnatarajia kutoa mafunzo kama hayo tena na gharama zake ni kiasi gani?
Hayo mafunzo ya siku mbili na cheti juu, basi watu waingeenda kusomea miaka mitatu.