''KIJIJI CHA TAMBUA HAKI YENYE WASHIRIKI 400 YA STEVEN KANUMBA YATAMBULISHWA RASMI '',

Rekodi ya Devils Kingdom aivunja mwenyewe sasa, baada ya kutoa filamu na mastaa kibao wa hapa nchini na  mmoja ya mastaa toka nigeria na kushirikishi watu zaidi ya mia moja ndani yake katika kuitayarisha filamu hiyo ambapo hapakuwahi kutokea wasanii wengi kwa idadi kama ile kukutanishwa ndani ya kazi moja kwenye historia yote ya tasni hii ya filamu hapa nchini..filamu hiyo ilifanywa kwa lugha ya kiswahili na kiingeleza kidogo kwenye sehemu kadhaa ndani yake hivyo kuipelekea ifanye vyema kwenye soko la  ndani na la nje ya nchi pia.
Baada ya filamu hiyo kutoka tulitegemea kuona watayarishaji wengine nao wa hapa nchini Tanzania kufanya kama mtayarishaji huyu kutoa ridhiki kwa watu wengi kiasi kile cha kwenye Devils Kingdom ila hapakutokea mtayarishaji mwingine kufanya hivyo, sasa  Kanumba mwenyewe ameivunja rekodi hiyo kwa kutayarisha filamu nyingine ijulikanayo kwa jina la ''KIJIJI CHA TAMBUA HAKI'' iliyo husisha washiriki mia nne (400) iliyofadhiriwa na POLICY  FORUM itakayo ingia sokoni mwishoni mwa mwezi huu chini ya usambazaji Steps Entertainment ambayo kaitambulisha rasmi katika ukumbi wa Kambarage ,Hoteli ya Regency jijini Dar es salaam..

SWALI LA KIZUSHI! ,Enyi watayarishaji wengine mwajifunza nini na mna lipi la kusema  juu ya hatua hii kubwa ya mtayarishaji mwenzenu  Bw. Kanumba?  mbali na kumsifia tu kila mwojiwapo?
The great nikisisitiza kuwa ni filamu ya kipekee hakuna mapenzi humo,hakuna majumba ya kifahari wala suti nzuri.ni maisha halisi anayoishi Mtanzania wa leo kijijini.

Posted by Bongo Film Data Base on 12:30 AM. Filed under , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for ''KIJIJI CHA TAMBUA HAKI YENYE WASHIRIKI 400 YA STEVEN KANUMBA YATAMBULISHWA RASMI '',

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign