MIKE; WASANII JIUNGENI NA VYAMA VYENU HUSIKA.

Michael Sangu
Mike Sangu Mwenyekiti Chama cha Waigizaji Taifa.
MWENYEKITI wa Chama cha Waigizaji Taifa Michael Sangu amewahimiza wadau mbalimbali pamoja na Wasanii wote kwa ujumla kujiunga na vyama husika katika fani za filamu, akiongea Fc Mwenyekiti huyo amesema kuwa iwapo vyama vyote vitakuwa hai ni wazi itakuwa rahisi kwa Shirikisho kuwafikia na kubaini matatizo yanayowakabiri katika tasnia hiyo ya filamu kutoka Swahiliwood.

Michael Sangu
Mike Sangu Mwenyekiti Chama cha Waigizaji Taifa.
“Vyama vyote viongozi wake wapo muda wote katika kuhakikisha wanachama wapata huduma stahili kwa ajili ya kujiunga katika vyama hivyo na kutoa maelezo na michakato inayokwenda katika tasnia ya filamu kwa sasa, na lengo ni kujenga umoja na kutatua matatizo ambayo tumekuwa nayo kwa muda mrefu katika fani yetu,”anasema Mike.
Katika kuimarisha shirikisho mwenyekiti huyo amesema kuwa kwa sasa kila msanii ni lazima ajisajili katika chama kinachomhusu ili kujenga utambulisho popote na kuwa na kauli moja kuhusu harakati na changaoto zinazojitokeza katika filamu za Swahiliwood Tanzania .
Ali Baucha
Ali Baucha Mwenyeki chama cha Waigizaji Kinondoni.
Kwa wale ambao ni Waongozaji wa filamu na hawajajiunga na Chama cha TAFIDA wanaweza
kuwasiliana na Katibu wa Taifa Patrick Komba kwa namba 0714 259 526 wakiwa na Picha mbili ndogo, nakala ya kitambulisho cha Mpiga kura pamoja kiasi cha Tshs. 2,500/ tu za kitanzania kwa ajili ya Fomu.
Chama cha Wapiga picha jongefu (TCA) wanaweza kuwasiliana na Mwenyekiti au Katibu wa Chama hicho kwa namba 0715 939 999 Mwenyekiti, 0714 257 054 Katibu Mahitaji ni kuwa na picha ndogo mbili na kiasi cha Tshs. 3,000/ kwa ajili ya fomu.
Chama Cha Waigizaji (TFDAA) kuna mikoa mitatu kwa wale wanaoishi Kinondoni fomu zinapatikana kwa wahusika wafuatao pamoja na namba zao za simu katika mabano Kinondoni (Mwenyekiti Ali Baucha 0715 994 995), Ilala (Husna Mgeni 0713 317 610) na kwa wasanii wa Temeke wawasiliane na Dile kwa namba 0714 561 800. Mwigizaji atatakiwa kuwa na picha ndogo na Tshs. 3,000/ kwa ajili ya fomu.
Ni matarajio yetu kuwa wengi mtajitokeza, lakini kwa wale wa Kinondoni pia mnaweza kutembelea www.tdfaa.blogspot.com kwa mawsiliano zaidi.

Chanzo; Filamu central

Posted by Bongo Film Data Base on 11:30 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MIKE; WASANII JIUNGENI NA VYAMA VYENU HUSIKA.

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign