H. BABA: NDIKUMANA SI WA KUONEWA HURUMA.

MWANAMUZIKI Hamis Ramadhani Baba ‘H-Baba,’ amemvaa mume wa msanii wa filamu nchini, Irene Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ akidai kuwa yanayomkuta sasa katika ndoa yake amejitakia.
Akizungumza na Ijumaa juzikati, H-Baba alisema Kataut aliingia kichwa kichwa kwa kuvutiwa na muonekano wa Irene lakini hakujua kuwa ni mwanamke anayestahili uvumilivu wa hali ya juu.
“Mi namjua Uwoya vizuri sana, mkitaka mapenzi yenu yadumu milele na milele basi umpe uhuru wa kufanya mambo yake siyo kujifanya una wivu sana, sasa angalia Kataut anavyoteswa na mapenzi, kwa hilo hastahili kuhurumiwa maana kayataka mwenyewe,” alisema H-Baba.
Huko nyuma Uwoya aliwahi kuwa mpenzi wa H-Baba kabla hajaolewa na Kataut na kwa sasa ndoa yao haijatulia.

Chanzo;global publisher

Posted by Bongo Film Data Base on 11:22 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for H. BABA: NDIKUMANA SI WA KUONEWA HURUMA.

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign