MAENDELEO YA MASTAA WA BONGO NI WA NGUVU ZA GIZA?!


NYOTA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, anadaiwa kutumbukia kwenye vitendo vya kishirikina,

Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Aunt, mwigizaji huyo huwa ana mganga wake anayemwekea mambo sawa yanapoyumba.
“Najua mkimuuliza atabisha, lakini kwa taarifa yenu Aunt Ezekiel ni mshirikina, ana sangoma wake maalumu ambaye ni kibogoyo, anaishi Mkata mkoani Pwani.
“Huyo ndiye anayemsafishia nyota ili ang’ae kila wakati,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Kwanza Aunt akichacha huwezi kumuona mjini, huwa yuko Mkata kwa ‘babu’ kufanyiwa ‘mavituz’ na akirudi mambo yake huwa ni ng’aring’ari kwani madili yanakuwa ya kumwaga.
“Kama akibisha, muulizeni huwa anakwenda kufanya nini Mkata kwani alishanaswa mara kibao akiingia na kutoka kwa mganga wake huyo.”
Baada ya kudakishwa ‘infomesheni’ hizo, gazeti hili lilimweka ‘mtukati’ Aunt na kumwagia ‘upupu’ wote ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kila mtu ana maisha yake hapa duniani ya namna ya kufanikiwa ambayo hayaingiliani na mwezake, yaani kwa mganga waende wao tu, tukienda sisi kwa sababu ni wasanii, basi inakuwa ni ishu?”
Hata hivyo, majibu hayo ya Aunt ndiyo yaliyozua maswali zaidi kwani hayakuweka bayana kama kilichosema ni cha kweli au la.
Skendo ya Aunt kuhusishwa na ushirikina imekuja katika kipindi ambacho kuna madai mazito kuwa tasnia ya filamu Bongo imeshikiliwa na baadhi ya mastaa wanaokesha kwa sangoma ili kukubalika na kukimbiza kwenye soko la muvi.

chanzo;global publisher.
asante!

Posted by Bongo Film Data Base on 9:11 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MAENDELEO YA MASTAA WA BONGO NI WA NGUVU ZA GIZA?!

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign